Muswada wa Katiba Mpya: Hotuba ya Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (Tundu Lissu)

lililo wazi na bila kutafuna maneno ni kuirejesha Tanganyika, wazo la katiba mpya lisimame ili kutoa nafasi kwa Taifa la Tanganyika kuzaliwa upya. kisha kujadili katiba au muungano baina ya wananchi wa nchi mbili na kuamua wanataka muundo upi ?

maaana kiukweli huu muundo tulionao una mkanganyiko mkubwa, Lissu( Lussu kama wazanzibari wanavyomuita) yeye siku zote anajaribu kuonesha kuwa watanganyika wanapaswa kuwa na nguvu zaidi ya wazanzibari na kutoa fursa sawa ni kuwapendelea wazanzibari. lakini na wazanzibari na wao wana mengi zaidi ya alioyaeleza bwana Lussu
 
Ningependa kupata hotuba ya mh. Lissu aliyoitoa bungeni jana kuhusu mswada wa katiba. Mwenye kuwa nayo naomba aiweke kwenye jukwaa hili. Natangulisha shukrani zangu.

Macinkus
 
Ningependa kupata hotuba ya mh. Lissu aliyoitoa bungeni jana kuhusu mswada wa katiba. Mwenye kuwa nayo naomba aiweke kwenye jukwaa hili. Natangulisha shukrani zangu.

Macinkus

jaribu web ya bunge, kisha tujuze
 
kuna ukweli mgumu ambao wazanzibar hawataki kuuelewa, anachokizungumza lissu ni jambo la msingi kwa mustakabali wa Taifa kwa siku zijazo, kwa mfano iweje wazanzibari washiriki kutunga sheria za mambo yasio ya muungano? jamani TUTAFAKARI kwa umakini. kuhusu CUF kuendelea kushabikia mambo ya CCM ni wazi Julius Mtatiro atakuwa anaumizwa na hawa CUF Zanzibar.
 
Lissu anawasemea wengi tu. Hata KIPOFU anaona ZANZIBAR hawautaki MUUNGANO. Tuwaache wakaunde Jamhuri ya Unguja na Pemba ili maneno ya Mwalimu yatimie.
 
viva Tanganyika viva,viva Tanzania viva.Suala lilipo mbele yetu ni suala la wakati.Zama za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama zimekwisha,Watanzania tuondokane na mawazo mgando,uaminifu umekwisha hakuna anayemuamini mwenzake hata wenyewe wa magamba hawaaminiani sembuse sisi.Tuna uzoefu wa kutosha juu ya uendeshaji wa serikali katika nchi hii.uzalendo na utaifa umetoweka hakuna wa kumfunga paka kengele.Leo hii ukizungumzia Muungano unaonekana msaliti,ifike wakati tuseme imetosha kutokana na mawazo mgando ya wala nchi hii.Ni lazima tuwakatae kwa maneno na vitendo.Kwanza kabisa nichukue fursa hii kuwasifu wabunge wa kambi ya upinzani kwa kukata kwao kufanywa mbuzi wa shughuli.Uamuzi wao upo sahihi kabisa,wote ni mashahidi tumeona mengi ya kiburuzwa ndani ya bunge hili lakini wadau wa nchi hii ambao ni wananchi wamekaa kimya.Bunge hili hili ndo lililotumika kuzima hoja ya kuwashughulikia mafisadi wa RICHMOND,Leo hii wanakuja na hoja ya muswada wa katiba,wajinga tu ndiyo waliwao.Kwa staili hii ni bora kutokuwa na bunge kuliko serikali kuliburuza bunge itakavyo.laiti ningekuwa na nafasi ya kupeleka hoja binafsi ningepeleka hoja ya kulivunja bunge hili lisilo na meno.

big up sana Tundu Lissu kwa kuwachana live wao na muswada wao magumashi.Nakupongeza kwa kutotafuna maneno haswa kwa suala la muungano na kusema ukweli bila kificho.Haingi akilini kuwafanya watanzania wote ni wajinga kiasi hicho.Urafiki huu wa mashaka kati ya wananchi na serikali utaendelea mpaka lini.Serikalini unapohoji mambo ya muungano unaonekana msaliti.Kuna kila sababu ya kuweka mambo hadharani nakujadili mpasuko huu wa muungano unasababishwa na nini bila kumung'unya maneno.

Nasema hivi kwasababu yanayotendeka bungeni ni kinyume na majukumu ya bunge kama mhimili unaoisimamia serikali.Leo Spika na wabunge wenzake wa chama cha magamba wamekuwa watetezi wa serikali?huu ni udhalimu wa wazi kwa wananchi waliowapa dhamana ya kuisimamia serikali.Tunajua wazi suala hili ni la wakati la sivyo wasingekubali mfumo wa vyama vingi nchini.Bunge lisilo na meno kiasi cha kushindwa kuwalinda watunga sheria wake wanapotendewa udhalimu na serikali.Hatuna imani na serikali ya chama cha magamba kwa staili hii.Hatuwezi kuendesha mambo kwa staili ya zima moto.Leo hii wasomi ni wangapi katika nchi tofauti na wakati wa kati tunapata uhuru,kwanini changamoto zao zinapuuzwa tu bila sababu ya msingi.Kaburi hili la fikra litaisha lini?Sisi wote mashahidi nchi nyingi zinaingia kwenye machafuko wakati wa mchakato wa katiba lakini kwanini serikali inashindwa kuexpirience kutokana na wenzetu!Mfano mzuri ni jana wakati wanapitisha sheria ya manunuzi ya umma,wameshindwa kuweka adhabu kali kwasababu wanajua wahusika wakuu waufisadi wa mali za umma ni wao wenyewe,kiasi wanashindwa kujuitia kitanzi wao wenyewe hii ni hatari sana kwa mustakabali wa kujenga taifa lenye utawala bora.
 
Kamwe wazanzibari wanaotuita sisi machogo hawawezi kutuamlia mstakabari wa taifa letu ,hawawezi kututungia sheria mama yaani katiba ya nchi tunaitaka Tanganyika yetu hatumng'unyi maneno ,Katiba itawezeshwa na wananchi wenyewe sio kikundi kidogo cha watawala na chama chao cha CCM,ni heri tufe wote tukipigania heshima ya utu wetu,nafsi zetu na utaifa wetu hauwezi kuwekwa rehani kwa mabishoo wa Zanzibar
Wao sasa wana nchi yao,katiba yao,wimbo wao wa taifa ,bendera yao yote haya wameyafanya bila kushirikisha watanganyika leo hii Kikwete anakasimisha uandaaji wa uratibu wa uandikaji wa katiba kwa wazanzibari haya ni matusi ya nguoni

kama ni matusi ya nguoni basi aliyewatukana ni huyo baba wenu wa taifa ambae kaificha tanganyika nyuma ya pazia la tanzania..simple mathematics, fichueni tanganyika yenu kila kitu mtajiamulia wenyewe watangayika na sisi mutuache na ubishoo wetu nyie muendelea na ufisadi wenu
 
Mimi namuona Lissu ni mkia tu. Hana lolote njaa inamtesa tu.

Ni kwlei kada njaa inamtesa Lisu kwani wewe mwenye shibe huwezi kutujua sie wenye njaa!

Afadhali mwenye njaa mwenzetu anatuona na kutujua, wewe kila la heri na shibe yako. Ila usisahau aliyeko juu mungoje chini, kuna siku utatukuta tunakusubili, dawa yenu iko jikoni.
 
jamaaa jana kaongea pointi kubwa sana wazee wa magamba badala ya kuchanganua mswada wana weka umbea tu
 
good move....I hope and pray that Watanzani tutashikamana na Kambi ya upinzani kuhusu Katiba Mpya...tusilazimishiwe katiba bali katika itokane na wananchi...
 
" The point must be made that ultimately the safeguard of a people's right, the people's freedom and those things which they value, ultimately the safeguard is the ethic of the nation.

When the nation does not have the ethic which will enable the Goverment to say: ' We cannot do this, that is un- Tanganyikan'. Or the people to say: ' That we cannot tolerate, that is un-Tanganyikan'. If the people do not have that kind of ethic, it does not matter what kind of constitution you frame. They can always be victims of tyranny....... What we must continue to do all the time, is to build an ethic of the nation, which makes the Heads of State whoever he is to say, ' I have the power to do this under the Constitution, but I cannot do it, it is un- Tanganyikan'. Or for the people of Tanganyika, if they have made a mistake and elected an insane individual as their Heads of State, who has the power under the Constitution to do XYZ if he tried to do it, the people of Tanganyika would say, 'We won't have it from anybody, President or President squared, we won't have it'.

I believe, sir, that is the way we ought to look at this constitution. We have got to have a little amount of faith, although I know that some Members have been questioning the idea of faith. But, sir, democracy is a declaration of faith in human nature, the very thing which we are struggling to safeguard here, the very idea of democracy is a declaration of faith in mankind. And every enemy of democracy is some person who somewhere has no faith in human beings. He doubts. He think he is all right, but other human beings are not all right.

28 June 1962 Hansard, 1st Session
Goverment Motion- Proposal for a Republic
 
Mi nimependa sana kauli aliyoitoa Mh. Vuai Nahodha leo asubuhi ambalo ndilo jambo la msingi kabisa ambalo watu tunatakiwa kuliangalia sasa hivi. Watanzania wa sasa sio wale wa miaka kumi iliyopita........... we should look into this
 
good move....i hope and pray that watanzani tutashikamana na kambi ya upinzani kuhusu katiba mpya...tusilazimishiwe katiba bali katika itokane na wananchi...

haya magamba yanalazimisha muswada wa katiba!!!!!!!!!!!!!!!!
Hakika magamba yatashindwa!
Watanzania bila kujali itikadi,ukabila,wala dini tujiunge kupinga huu muswada wa magamba!
Hakika mungu yupo upande wetu>
na hakika kifo cha magamba kimekaribia tena kinakuja kwa haraka
magamba tafadhali magamba tafadhalini!!!!! Musituamulie mustakabali wa nchi yetu
wapeni wa tz haki yao....
Hakika hata kama magamba wameupitisha kwa mara ya pili tutaukataa mpaka kieleweke
hakika katiba ya magamba haitasimama katu !
 
Back
Top Bottom