Muswada kuahirishwa: Serikali Imesoma Alama za NYAKATI?

Kuahirishwa kwa mswada kutamaanisha jambo moja tu kwa CCM na CCM-B, CDM na wanaharakati wameshinda. Hii itakuwa ni aibu kubwa sana kwa sababu wamewaponda sana na kuwadharau. Itaonesha kuwa wabunge hao wa CCM A,B walikuwa wanachangia jambo wasilolielewa.

CCM itaonekana imeogopa madhara ya maandamano yasiyo na kikomo, maana inaweza ikawa ndiyo mwanzo wa kuuondoa utawala dhalimu ulioiba kura. Kwani hata rais mwenyewe hajui kama askari wote watalalia upande wake.
 
Natamani mtu yeyote anayekutuingiza kwenye ghalama mpya sisi masikini achukuliwe mapema na mwenyezi Mungu
 
Katiba tunayoitaka ni muhimu iwe ya WATANZANIA, sio ya chama fulani---CCM/CDM/CUF. Tunataka katiba ya Watz. Sasa kumeibuka kundi ambalo linajiona ndio TZ, Tutafika kweli namna hiyo. kesho vurugu zikitokea utawasikia wachochezi hao wachochezi hao akina, nani?
hakuna majibu, hivi CCM wakiruhusu wananchi wakatoa maoni yao namna wanavyotaka watawaliwe, wao (CCM) kinawauma kitu gani?

Sana sana tunachoshuhudia sasa ni kampeni za udini tu,
.
Kweli kabisa
Isitoshe Celina kombani (Waziri wa sheria) na Mwanasheria mkuu ndio walikuwa wa kwanza kusema tanzania haihitaji katiba mpya. Hakuna sehemu waliwahi kukanusha usemi wao wala kuomba radhi kwa watanzania juu ya kauli zao. Leo hii wao ndio waratibu wa mswada wa katiba bungeni. Inawezekana kweli kitu usichokipenda ukakisimamia ua ni unafiki tu. Tunamuomba JK kama anania ya dhati ya kuleta katiba mpya awatoe watu hawa katika nafasi zao au wafute kauli zao kwa sababu hawawezi kusimamia wanachokiamini. Wananiudhi kweli
 
Binafsi sijaona sababu ya msingi kwa spika kuahirisha bunge hadi kesho. Hao mawaziri watajibu nini ikiwa wabunge karibu wote hawakuchangia hoja ya msingi. Badala yake wametumia muda wao mwingi kwa ajili ya kumshambulia Tundu Lisu. Tutafika tu.
 
Hili ni suala linalohusu mstakabali wa taifa hili, hii mizaa mizaa ya kudulaghai kwa VICHWA vizuri vya habari ili hali hakuna uthibitisho patakuja chimbika hapa jamvini. Watu tunauchungu na taifa letu halafu wengine mnaleta soft stories hapa. Toa uthibitisho ndugu, acha uzushi. Ni uchungu tu wa taifa langu ndio unanifanya niwe mkali plz mtoa mada usinielewe vibaya maana inawezekana lugha yangu imekuwa kali sana. Sina baya rohoni but Ni-Utanganyika ndio unaniifanya niwe kama nilivyo.
 
Ni maandalizi ya kuahirisha mjadala baada ya kuona Lisu ana hoja ya msingi.
 
Kama walisema siku 3 wanasubiri nini kama siyo woga na kusubiri amiri jeshi awaabie la kufanya! Kete za kucheza zimeisha!
Wakipitisha tu nikama ile ndege ya rais wa rwanda habyarimana ilipopigwa. Kazi kazi
 
nani zaidi.

Mkuu hapa hatupimani nguvu kuwa nani zaidi. Kinachotakiwa hapa ni kutengeneza mazingira ya watanzania kutafuta katiba yao mpya bila kuwa monopolised na kikundi au chama chochote kile. Waswahili husema safari ni mguu wa kwanza...

Kama wale wanaodhania kuwa wanaumiliki wa mchakato huu wameona kuwa busara ni bora itumike litakuwa ni jembo la kheri kwa mustakabali wa Taifa. Watu wanataka mabadiliko, kuendelea kuwanywesha mawazo wanayoamini si yao ni kuwachefua roho na wakianza kutapika wakulaumiwa ni mnyweshaji.
 
yap,possibility nikubwa,naona dr.salim na warioba wamemfata dr.slaa (raisi) nyumbani kwake wanayamaliza.

source:zitto kabwe on twitter page



sahihisho::

zitto alijikwaa kama alindika kuwa walimfata nyumbani kwake...pale ni makumbusho dsm nasio nyumbani kwake...
 
Yoote haya ni sababu ya huyo zao la UFISADI Bi Kiroboto! Ameingilia Mchakato mzima kwa kuilazimisha Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba kufanya anavyotaka yeye. Wananchi hawajapata nafasi ya kuujadili ule Muswada, umepelekwa puta mjengoni, vilaza wa CCM wanaupigia chapuo, sio kwa kuchangia hoja, bali kwa mipasho ya taarabu kama mtunga nyimbo wao tumbotumbo. Halafu watajidai wametuwakilisha! SHAME, SHAME, SHAME ON ALL OF THEM. mungu ibariki Tanzania.
 
Katiba tunayoitaka ni muhimu iwe ya WATANZANIA, sio ya chama fulani---CCM/CDM/CUF. Tunataka katiba ya Watz. Sasa kumeibuka kundi ambalo linajiona ndio TZ, Tutafika kweli namna hiyo. kesho vurugu zikitokea utawasikia wachochezi hao wachochezi hao akina, nani?
hakuna majibu, hivi CCM wakiruhusu wananchi wakatoa maoni yao namna wanavyotaka watawaliwe, wao (CCM) kinawauma kitu gani?

Sana sana tunachoshuhudia sasa ni kampeni za udini tu,
Mkuu tatizo la CCM, kubwa ni kuwa ubovu wa katiba una wanufasha wao zaidi lakini wana sahau kesho nao wanaweza kuwa wapinzani....la pili ni ubabe na kutaka kutunishiana msuri na Chadema hawajui kama CHADEMA inaungwa mkono na wananchi na NGO mbalimbali....
 
KUELEKEA KATIBA MPYA, ZANZIBAR MOJA -TANZANIA VIPANDE VIPANDE!!!

Mambo yakienda kama yalivyo kuelekea kupata Katiba mpya tunashuhudia Zanzibar ikiwa na Umoja na Mshikamano katika kutetea Maslahi ya Zanzibar............ lakini tofuati na huku Bara tunakwenda kwenye meza tukiwa na makovu ya kurushiana vijembe na kuonyesha umwamba kati ya CHADEMA na CCM. CCM imesahau kwamba yenyewe ndiyo ilitakiwa iwe kiongozi wa kutuunganisha watanzania lakini yenyewe imekuwa ya kwanza kuubomoa umoja wetu..... Kwa Muswada unaoendelea utawanufaisha zaidi Wazanziabar kwa sababu yote waliyokuwa wanadai yameingizwa. Sisi Wabara tunakwenda kuandaa Katika tukiwa vipande vipande. CCM imekuwa ikijitahidi kuchakachua ili iendelee kutawala bila hata kuangalia maslahi ya Wabara. NI bora usitishwe ili Tanzania Bara tuwe na Mwafaka wa Kitaifa la sivyo ile ndoto ya Katiba mpya na Tanzania mmoja haitakuwepo......... CCM situkeni mmeingizwa mkenge na wazanzibar!!!!!!!!
 
thibitisha hili mkuu ili comment kitu cha maana

Ni kweli Bunge lilihairishwa hadi kesho ili kuwapa wabunge muda wa kutafakari juu ya muswada huo, i think haijawahi kutokea mambo haya yakasimamishwa kwa sababu za namna hiyo. Lets wait and see the next move for CCM.

source; Taarifa ya Habari ya saa 10:00 Alasiri: Redio Free Africa.
 
Back
Top Bottom