Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Tukatae tukubali muungano wetu hauko sawasawa,na kuukataza kuujadili hii serikali ya ccm inazidi kumwagia petroli kwenye moto unaoanza kuwaka..,!
 
Hapa tuwache ushabiki wa kichama, kiitikadi au kikanda. "The fate of Tanzania as a nation is at stake". Tupiganie kila ambacho ni bora kwa Tanzania. Tukiwa na katiba imara, vizazi vijavyo vitatushukuru, tukiwa na katiba ya ushabiki na viraka tunawaandalia vizazi vyetu uwanja wa maonevu na vurugu.

Muungano wa 1964 kama ulivyowekwa na kuchakachuliwa baadaye leo hauna nafasi. Nyerere na Karume hawapo tena. Ingawa walianzisha Muungano kwa nia njema na mpaka sasa hakuna asiyetaka Muungano, lakini ni haki ya wananachi kuchagua wanataka Muungano wa aina gani.
 
Nimejaribu kusoma makala kadhaa kuhusu Muungano ikiwa pamoja na kero zake nimegundua kwamba matatizo makubwa ya Muungano ni pamoja na:-
  • Tanganyika kujiona wakubwa katika muungano
  • Wazanzibari kujiona waarabu zaidi kuliko waafrika
  • Wazanzibari wenye asili ya arabuni kuamini kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Watanganyika, ndio maana kwa kila kosa linalofanywa na Mtanganyika zanzibar ni kubwa na linachukiza mno kuliko kosa hilohilo likifanywa na mtaliana, mganda, mkenya, mhindi na mwarabu ndo kabisa si kosa abadan
  • Watendaji wa taasisi za Muungano (TRA) wana choyo na roho mbaya mno dhidi ya wazanzibari maana kila wakiambiwa juu ya kunyanyasa wafanyabiashara pale bandarini hawataki kuelewa
  • Wazanzibari kuamini kuwa watanganyika wote ni makafiri kiasi cha kutowaamini hata waislamu wa tanganyika
  • ................
ntarudi tena naona bosi wangu kaingiya ofisini kwangu, so ngoja niue sooo
 
Zinedine na mammamia nimekubali hoja zenu sana,,mi naona kama kuna haja ya kutengana na zanzibar ili wajue maisha yakoje,,wanatubabaisha bure tuu ukiacha all the favors we do for zanzibar for the sake of nationality,,LET THEM GO,THEIR Part in the story is over. . .
 
Inaonekana wazanzibar wanajua zaidi muungano na faida za muungano,ndio maana wameupinga kwanza huo mjadala tena kwapoints,sio watanganyika munapinga kwa mawe,tutumieni usomi wetu na haki zetu ili tuende kisheria.

Hapa zanzbar hakuna majadiliano hatu tuirudishe tanganyika,na majadiliano hata ni baina ya tanganyika na zanzbar sio bunge la muungano,nafikiri kimeeleweka mpaka hapo.

Nimependezwa sana na wazanzbari na washasema kuwa wao ni vijana wa leo sio wa mwaka 1964.
 
Jamani nilitaka kuangalia ile thread ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mkowa wa Mbeya kuhamia CCM, ili tujue tatizo nini mpaka wa Kahama.
 
@donmzushi.
Kama wewe ni mkweli andika hizo favour ambazo tanganyika imeifanyia zanzibar.kuwa makini na maneno yako usiropoke. Unajua chanzo cha muungano? Unajua znz ilikuwa na hali gani kiuchumi na kielimu na kiafya wakati tunaungana?nyinyi hata tv mmekuja kuiona baada ya miaka 22 baada ya znz. Favour ipi labda kupeleka majambazi znz na machangudoa.
 
Kuwe na kura ya maoni kuusu uwepo wa muungano kabla hatujaendelea na swala la katiba.
 
CHADEMA+ wanaharakati + wanataaluma + Watanganyika wakibainisha mapungufu makubwa ya mchakato mzima wa KATIBA wanadharauliwa na kubezwa, Mungu Mkubwa sasa Wazanzibari wameweka utaifa wao mbele tuone sasa kama kina Makamba + Mathias Chikawe + JK watafua dafu kwa ndugu zetu hawa wa-Zanzibari na mikakati yao(CCM) ya kuendesha 'mchakato' huu wa katiba kwa 'dharula' ya kasi ya ajabu.

CCM njama zao zitashindwa kwa nguvu ya umma kwenye hili zoezi.
 

Mwenyekiti wa maimam Zanzibar amesabisha kuvunjika kwa kikao cha kujadili muswada wa rasimu ya katiba pale alipoamua kuuchana muswada huo mbele ya kamati na kutoka nje.... vurugu a kelele zilitawala na watu kuanza kutoka huku wakiimba "hatutaki muungano".

pia imam aligusia swala za kura za maoni juu ya muungano kwanza kabla ya Zanziba kujadili katiba mpya....!

ni wazi kwamba serikali ili-under estimate response ya watu wa Zanzibar juu ya muungano, pia inawezekana serikali illitambua hili na ndio maana hawakutaka wazanzibari wajadili wenyewe bali waje bara (Dar au Dodoma)

Tafakari....

Source: TVZ
 
Hahahahha! Nacheka siyo kwa furaha ila kwa masikitiko na hapo ndo patamu, Zanzibar ni nchi Tanganyika siyo nchi. Kwa nini wajadili katiba wakati muungano hauko wazi kwa wananchi wenyewe? Heko Imamu, liwe fundisho kwa viongozi wetu kuendelea kukumbatia uozo unaotoa harufu kali katika karne ya 21. Too bad, everyone knows that Zanzibar ya leo iko kwenye muungano kwa kulazimishwa, hata Watanganyika leo hii wameshachoka kulazimishwa kuwa kwenye muungano.
 
hapa ni mwanzo tu wa pilika zenyewe, muda wa ndio mzee unakwisha, wakubwa hawa watajua tu kufikiri kwa maslahi ya nchi na vizazi
 
well, mimi natamani muungano uwe na nchi tatu kila nchi i deal na mambo yake na nchi zote mbili zichangine kwa usawa. Ni ukweli japo wa ZNZ hasa wanaoishi bara wanaweza kukataa kwa sababu wamejisahau, kuwa Kiuchumi Bara ina fulsa nyingi za kupiga hatua kuliko inavyodhaniwa. Na tukiwa na nchi mbili kutakuwa na fulsa ya ushindani na wakati huo ndio tutajua nani alibebwa na muungano.
 
kwa kweli hata mimi huu muungano sijawahi kuuelewa vyema. na wamezuia hilo kujadiliwa, sijui wanataka kutuambia kuwa sisi ni sawa na watumwa? mtu huru atazuiwaje kujadili jambo linalomgusa kila siku?

hongera sana imam na wazanzibari wote, tuko pamoja angalau katika hili
 
Kama dr. Mvungi, prof baregu, advocate mpoki wa TLS na justice Thomas MIhayo walivyosema jana kupitia TBC kuwa mswada huu ni big disaster na inaashiria kuzama kabisa kwa ccm, leo zanzibar saa moja iliyopita sio tu wazanzibar wameukataa mswada bali wameuchanachana live mbele ya vyombo vya habari.

Hawa ccm kweli sikio la kufa halisikii dawa, wanataka kuleta fujo kulazimisha interest zao, chondechonde ccm watuepushe na fujo watanzania hatutakubali uzandiki huu, hongera wanzibari sisi watanganyika tulishaukataa.

Hongereni saana wazenji kuepuka unafiki,
 
kwa kweli hata mimi huu muungano sijawahi kuuelewa vyema. na wamezuia hilo kujadiliwa, sijui wanataka kutuambia kuwa sisi ni sawa na watumwa? mtu huru atazuiwaje kujadili jambo linalomgusa kila siku?

hongera sana imam na wazanzibari wote, tuko pamoja angalau katika hili
wenzio WANAFUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE!
 
Public Hearing imezua mambo huko Zanzibar! Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu akitoa mchango wake kuhusiana na muswada wa kuandaa katiba mpya mchana huu pale shule ya Haille Selasie amesema nyakati za udikteta wa Mwl. Nyerere zimepita na sasa watu wanaweza kusema kwa uhuru na haki na kuwahoji waliohudhuria kama wanataka Muungano au la. Kwa wingi kama ilivyo kauli moja wakasema hawataki, hapohapo jamaa akachana muswada huo mbele ya Mh. Sitta na wanakamati wengine na kutoka ukumbini na wengi wa watu waliohudhuria wakimfuata.
Sijui huko nje ya ukumbi kiliendelea nini lakini mambo si shwari sana kuhusiana na katiba mpya miongoni mwa Wazenji. Tangu Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo jirani waseme hawakuhusishwa kiasi cha kutosha kama serikali hapo jana, mjadala umeonekana kuwa mchungu sana kwa wenzetu pengine kuliko huku.
Kama ni kweli walipuuzwa kiasi hicho kabla ya kuandaa muswada huo wakati na wao wanayo Wizara ya Sheria ni jambo la ajabu sana kwa upande wa serikali hii ya Rostam. Nashawishika kukubaliana nao kama wako serious kuuvunja Muungano kwanza endapo CCM hawajaona umuhimu wa kuhoji uwepo wake hali inaonekana wananchi walio wengi upande huo wa Nchi jirani hawaupendi.
Nawaomba wana-jamvi wenzangu tuifuatilie hali inayoendelea kwa makini ili tuwe na nafasi ya kuuchambua kwa makini Muungano huu na itakapobidi tuandike makala nzuri ili kuwashauri wahusika kuona umuhimu wa kujua wananchi wengi wanataka Muungano huu kweli au waliopo madarakani wanalazimisha.
Wakati mwingine najikuta nawashangaa Rostam na serikali yake. Kama wanataka Muungano udumu ili wavune huku na kule kwa nini hawashughulikii kero ambazo zimedumu muda mrefu? Umuhimu mkubwa sana wa Muungano ni nini hata watu wabanwe kiasi cha kujidhania wanalazimishwa na si hiari yao.
Muungano ukivunjika nitamwomba Mzee Yussuf, Mfalme wa Modern Taarab aniachie vyombo vyake vya muziki akiamua kurejea kwao Unguja. (Just a little Joke!)
 
Kuiba kulaaniwe milele ..hii ni dhambi,dhambi ya kuiba kura na haki za watanzania,sasa serikali yake inakumbana na deadlocks kwa kila kitu,inapingwa sijawahi kuona ..utadhani ni ya shetani,ameruka mkojo akayakanyaga,hapa alipofika ndo mwisho wake vingnevyo nchi inatoweka
 
Back
Top Bottom