Huwezi kujuwa wanataka nini kwasababu wakati wewe mwenyewe hujuwi kitu gani kilichopo!
Wewe unajua nini kilichopo!
Huwezi kujuwa wanataka nini kwasababu wakati wewe mwenyewe hujuwi kitu gani kilichopo!
Kwani baraza la mawaziri la Tanzania haliwahusu Wazanzibari? Haya ndiyo matatizo yanayotakiwa kuwekwa sawa katika katiba mpya.Huwezi kuwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano yenye mawaziri kutoka pande zote, baraza la mawaziri lipitishe jambo halafu useme upande mmoja haujashirikishwa.
Hao mwaziri na wabunge wa JMT kutoka zanzibar wanafanya nini kama siyo kuwawakilisha?
Nafikiri si kweli kwamba ilivyo sasa muungano ni vigumu kuanguka, hapana tungekuwa na serikali moja hapo sawa lakini mbiliii. Kwa muundo ulivyo leo Zanzibar wanaweza tangaza kujiondoa na kusema tangu leo muungano kwishaaa.
Mie kweli nawashangaa wazanzibar wanalalamika wakati uwezo uko ndani yao, Kwa waTanganyika ndo kugumu ku declare kuvunja muungano maana serikali yao ni virtual.
Angalia, makamu wa Rais wa serikali ya Muungano akiwa mzanzibari , waziri wa ulinzi mzanzibari, waziri wa mambo ya ndani mzanzibari nk, unafikiri hawa watadeclare kuvunja muungano wakale wapi?? Hata maalim self akiwa rais wa muungano hatokubali kuvunja muungano akale wapi?
Serikali ya mapinduzi iliyo na wazanzibari kwa asilimia 100% ndo yakuvunja muungano, utawashangaa nao wanajumuika kulalamika wakati guts zimo kitandani mwao zakufanya watakalo.
Mkuu.Siungi mkono zanzibar kuondoka kwenye muungano ila nasema kuwa kama hawa jamaa wana kero zinazowasumbua kitu ambacho naju kipo basi ni vizuri sana zijadiliwe mapema sana. Zanzibar ni sehemu muhimu sana kwetu..
Mkuu.
Tufungue macho na sisi hapo nilipo-highlight nyekundu.
Kivipi?
Sisi tunaiona kuwa ni toto tundu tu.
Tunawabeba na hawana shukrani. wanatutia hasara tu.
Na hatuna serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kama wao.
Mkuu..vipi Zanzibar inakuwa ni sehemu muhimu sana kwetu?
Zanzibar yenyewe hata haina ukubwa wa jimbo la Ubungo la Mnyika!!!
Tueleweshe umuhimu wa Zanzibar kwa Tanganyika, Mkuu.
Natanguliza shukrani zangu kwako.
Chamajani.Kama mtoto mchanga aliyezaliwa leo anakuwa muhimu kwa wazazi wake atakosaje kuwa muhimu sana mtoto wa std one!
Huwezi kujuwa wanataka nini kwasababu wakati wewe mwenyewe hujuwi kitu gani kilichopo!