Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Nimejaribu kusoma hoja mbali mbali katika makala hii ilioanzishwa na HMaster na nimebaini kwamba kilichomo zaidi ni dharau, kejeli na mazungumzo yasio na ukweli au yanayotokana na wazungumzaji kutojua au kuukubali ukweli kuhusu huu Muungano. Muungano huu ulikuwa ni baina ya nchi mbili huru, yaani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Wakati huo, Zanzibar ilikuwa ni Mwanachama wa Jumuiya ya Madola na Umoja wa Mataifa na baadhi ya Agencies zake kama vile ILO, WHO na UNCTAD.

Wakati Nyerere alipokuja na proposal ya Muungano kwa Karume, alitumia vitisho hivyo hivyo vya kwamba Waarabu watarudi na mambo kama hayo. Hio ilitumika kwa muda mrefu na ukawa ni wimbo kwa Viongozi wa Zanzibar mpaka mara moja, Mwalimu akamwambia Marehemu Dr. Omar,

"Viongozi wetu hawana la maana kuwaeleza wananchi wao, isipokuwa Hizbu,imefanya hili na Sultani alikuwa akifanya lile na lile.Jee, jamani vijana wetu tuliokuwa nao, hivi sasa ni nani anaeijuwa Hizbu ni nani anaemjuwa Sultani? Hivi kweli hamna zaidi ya haya kuwaeleza wananchi?"

Muungano huu tangu kuanza kwake una mashaka na ndio maana kila uchao tunazungumzia kero ambazo hata viongozi wote wa pande mbili wanajua kuwa hazitakwisha. Kuna mambo kadhaa ambayo yalitakiwa kufanyika hayakufanyika kama vile kuitisha Mkutano wa Katiba na pia Muungano huu haukuridhiwa na Baraza la Mapinduzi ambalo wakati huo lilikuwa na executive na legislative powers.

Muungano huu una matatizo tangu mwanzo kufahamika. Hebu jiulizeni, nchi ilioungana na Zanzibar yaani Tanganyika iko wapi? Sisi tunajua kwamba Tanganyika ndio hio hio Tanzania kutokana na mfumo uliopo. Tatizo linalojitokeza ni kwamba kila mambo ya Muungano yanapoongezeka, mamlaka na madaraka ya Zanzibar yanapungua kiasi cha kwamba imekuwa tegemezi kwa Tanganyika, jambo lililoandaliwa kwa ufundi mkubwa. Muungano una matatizo kiasi cha kwamba hata muasisi wake aliliona hilo na aliwahi kusema,

"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand"

Muungano huu umedumu kwa muda wote huu kutokana na Chama Dola cha CCM/SMZ/SMT na matumizi mabaya ya hizo nguvu za Dola.

Mbinu nyengine ni zile zilizotumika kuwagawa Wazanzibari kwa misingi ya Ukabila, Kivyama (baada ya kuja mfumo wa Vyama vingi) na Umajimbo.

Wazanzibari sasa wamelitambua hilo na wanajitahidi kumaliza tofauti zao na matokeo yake ni GNU ingawa bado wako Wahafidhina wachache wanaofaidi peke yao wanaleta tabu. Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ni kielelezo chengine cha umoja wa Wazanzibari ambapo Mswada huo wa Sheria ulipita kwa asilimia mia moja. Kura ya Maoni kuunda GNU ni kielelezo chengine.

Kwamba maoni yaliotolewa juzi, ni maoni ya wachache, ni kujifurahisha kwenu tu lakini ukweli mnaujua kwamba Wazanzibari wa rika zote bila ya kujali itikadi zao wamedhamiria kujipapatua na ukoloni wa Tanganyika. Kama hujui, mpaka Mawaziri, Watendaji Wakuu wa Serikali akiwemo Mwanasheria Mkuu walipinga huu udhalilishaji unaofanywa na Tanganyika dhidi ya Zanzibar. Hata muasisi wa CCM ambae amewahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Vyama vya ASP/CCM na Serikali zote mbili za SMZ/SMT, Mzee Hassan Nassor Moyo, alisema,

"Ule wakati wetu na Nyerere tlikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hwakubali, Bw. Sitta, ITS OVER".

Jee huyu mzee wenu wa CCM nae ni mlevi? Ni vizuri kujadili hoja kwa hoja na wala si kwa jazba na dharau.

Napenda kumalizia kwa kukunukulia tena maneno ya Mwalimu aliposema,

"Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga"

by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Wazanzibari wanatumia njia za kistaarabu kutaka kujipapatua katika huu "Muungano" feki na wanaona kuwa 'saa ya ukombozi ni sasa'. Kama kutakuwa na utaratibu mwengine wa kuungana basi uwe unatokana na kuheshimiana

Mwisho kabisa napenda kuwajuulisha kuwa Zanzibar itakuwepo bila Tanzania lakini Tanzania haiwezi kuwepo bila ya Zanzibar.

Isitoshe Zanzibar imekuwepo kabla ya Tanganyika (refer to the old map of Africa below)




Nadhani mtanielewa.
 
Kitu kimoja nimekubali wenzetu Wazanzibar wana spirit ya ajabu linapokuja suala la utaifa wao,wanapingana nusu kuuana kwenye vyama lakini wanaungana zaidi ya kitu chochote kwenye mambo ya taifa lao ...nawapenda sana na hiki kitu wabara hatuna,tunapiga kelele sana kumbe tuko waoga tu na wanafiki ni wengi,kwa nini nasi tusijieunze kujisimamia na kuyasimamia mambo yetu kama Watanganyika(wabara)?
 
Tazama hii video kuanzia dakika ya 27

 
Last edited by a moderator:
Siasa mara nyingi wale wanaofuata mkumbo huwa wanaonekana ni watu wanao jua sana na wenye uerevu na upeo mkubwa kwenye masuala hayo kwa upande wa viongozi ndio maana hata ukiwa na viongozi mia wa chama kimoja katika mifumo ya kwetu tuliyoizowea wote huwa wengi kwa idadi tu lakini maamuzi yao na jinsi wanavyofikiri ni sawa na sawa na kuchukua mawazo ya mtu mmoja tu ukayajumlisha mara tisini na tisa basi itakuwa umejirahishia kazi badala ya kukusanya umati.

sasa uamuzi aliouchukua mwanasheria huyu ni jambo la ajabu kwa viongozi wa nchi yetu na wamejidhihirisha wazi kuwa walichokitarajia wao ni kinyume na kilichotokea hili alilofanya mheshimiwa huyu sio jambo la ajabu lakini hatukuzowea kutumia vichwa vyetu kwa miaka zaidi ya hamsini sasa kwa nini huyu bwana ameamua ghafla kuvunja utaratibu walio jiwekea ccm tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

ccm wametumia nafasi waliyo nayo vibaya wakitegemea taifa hili ni lile lile na watu wake ni wale wale walicho sahau hawa ni watu wengine kabisa ambao ni vijana na wana fikiri tofauti na wazee wao pia mazingira na dunia wanayoishi imebadilika ndio maana huwezi kuwadanganya au kutumia mbinu za kale kutawala koloni jipya.

mwanasheria othman masoud huwezi kumfananisha na yule mbunge wa dimani ailyekata viuno hadharani dodoma pamoja na wale walio kata vyumbani peke yao au na wapenzi wao kusherehekea ushindi wa rasimu iilyopitishwa na bwana sitta na bibi samia suluhu kwa kuwatumia wajumbe waliokuwa hijja,mahospitali,nayule wa tanganyika bibi zakia meghji aliyerudishwa kwao mara moja kwa kupiga kura tu halafu akarudishwa kwao tanganyika,pamoja nayule mjumbe marehemu shida aliyefariki tangu july 2014 lakini alihudhuria na kupiga kura oct 2014 ukiwa mjumbe au mwanachama wa ccm hata ukifa bado hajasalimika.

Rasi kikwete ameanzisha mchakato huu makusudi akijua kuwa hautofanikiwa lakini alisema wazi kuwa hataki tanzania imfie mikononi mwake sasa kama kuna njia ya kuhakikisha anaondoka salama na balaa la kuzaliwa upya au kufariki kwa nchi hii litawakuta hao wanao gombani urais wa nchi na kwa muda ulio salia tutazumgumza rasimu mpaka aondoke lakini hakutokuwa na katiba wala kura ya maoni kwani hilo sio kusudio la kiongozi wetu.

Wengi tulikurupuka tukifikiri kuwa tunajipanga kwa katiba bora,mpya na taifa jipya lenye baraka za raia wake na mpaka jaji msataafu warioba ana maliza kazi yake na tume yake hilo lilifanyika lakini hapo ndio mwenyekiti wa ccm aliposhituka na kuona hii kazi ina kwenda sivyo alivyokusudia hapa kuna uwezekano ikapitkana katiba nzuri na bora ndio akafunga safari kwenda dodoma kuamrisha na kulihutubia taifa na kuzikana rasimu zote za warioba alizozibariki na kuzikubali awali kwa kisingizio cha jeshi kuchukua nchi ili tuingie woga na kukubali rasimu ya ccm inayoikandamiza Zanzibar na kuivesha joho sio koti tena sasa joho Tanganyika la muungano.

Zanzibar na Tanzania itakapoandikwa historia ya nchi zetu hizi atakumbukwa bwna othman Masoud kuwa ni kiongozi aliyekataa kuweka maslahi yake mbele,cheo chake na uslama wa maisha yake pia kwa kutetea kile alichokiamini kuwa ni haki yake na wajibu wake kama raia huru na mwanasheria mkuu wa serekali mwenye jukumu la kusimamia sheria na haki zote za sehemu moja ya mshirika wa muungano huu sasa siwaelewi kabisa wale wote waliomzomea na kumbeza kwa sababu jukumu alilokwenda nalo dodoma ndugu othman ni kubwa sana kwa mabega yake lakini amelibeba kama mzega zega kwa maslahi ya zanzibar ndio nikasema na ninarudia mhe.othman masoud sio yule mbunge wa dimani aliyekata viuno na siasa za kufuata mkumbo zina tawala chama hiki siku zote lakini haina maana ndio siasa pekee na sahihi kwa sote.
 
Back
Top Bottom