Mussa Hassan "Mgosi" umechemsha kwa masharti haya!!

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Mshambuliaji wa Simba Mgosi ambaye ameambiwa wazi kiwango chake kimeshuka na hahitajiki kwenye kikosi cha kocha wa Simba Mganda Moses Basena, ametoa masharti mazito kwa timu inayomuwania ya Villa Squad.

Kwa mujibu wa gazeti la Dimba leo amotoa masharti yafuatayo;

1. Anataka katika mkataba wake awe anafanya mazoezi jioni tu,

2. Acheze mechi za Dar pekee na si zitakazo kuwa zinachezwa mikoani

Kwa mtaji huu na kama hawa ndio wachezaji wa kutumainiwa na kutegemewa timu ya taifa hatutafika popote miaka nenda rudi, yaani mchezaji umeshuka kiwango unatoa masharti kama haya...
 
kocha analalamika kuwa wachezaji wa kibongo wanacheza mechi chache sana ndo maana wanaperfom kidogo yeye anataka afanye mazoezi jioni na acheze mechi za dar huyo kweli hamnazo inaelekea uvivu na ustaaa ndo umefanya kiwango chake kishuke ila hao ndo wachezaji wa kibongo hata aje ferguson na msaidizi awe mourinho kwa style wabongo tutabaki kuwa kichwa cha mwendawazimu
 
Kuna siku nilienda taifa ilikuwa inacheza Yanga na timu ya nje basi yeye akiwa amepakiwa katika gari la Kaseja akashuka na kwenda kuomba pesa kwa Kassim Dewji ambaye alimpatia noti kadhaa bila kuhesabu jamaa alifurahi kinoma, niliumia sana kuwa wachezaji wetu bado wako tegemzi kiasi hicho kumbe hata mazoezi hawafanyi sasa mafanikio ya kucheza soka ulaya yatakuja kweli?
 
kashakuwa maarufu huyo sasa hivi utasikia na yeye anaigiza filamu! mara katoa single yake, nk
 
Back
Top Bottom