Elections 2010 Musoma mjini ni ya CHADEMA!

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,771
804
Sasa naweza kutamka kwa uhakika kuwa Musoma Mjini itakwenda kwa Nyerere wa CHADEMA. Kila nilikopita kati ya watu 10 ni 2 au 3 ndo CCM, waliobaki wote CHADEMA.
 
I suppose ana undugu na Rais (former) Nyerere ... Inaonekana hii ni a very open-minded family.
 
Safi, cha muhimu ni kuhimizana kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuzilinda.....
 
Sasa naweza kutamka kwa uhakika kuwa Musoma Mjini itakwenda kwa Nyerere wa CHADEMA. Kila nilikopita kati ya watu 10 ni 2 au 3 ndo CCM, waliobaki wote CHADEMA.

Asante kwa taarifa nzuri sana hiyo. Je uliwauliza pia kama wamejiandisha kupiga kura??
 
Asante kwa taarifa nzuri sana hiyo. Je uliwauliza pia kama wamejiandisha kupiga kura??
Wamejiandikisha. CCM walijaribu kununua baadhi ya shahada kama elfu 3 maeneo ya Nyakato, CHADEMA kama kawaida yao wakainasa issue kama ilivyo na kuwaanika jukwaani. Kwa hakika nimetoka Musoma leo jioni CCM wamepoteana kabisa. Nyerere ana sera zinazotekerezeka kwa watu wa chini na ana data mpaka za vikao vya ndani kabisa vya siri wanazopanga CCM. Na kama kawa ya CHADEMA data zote huwa wanazimwaga jukwaani na huwa zina kuwa za kweli kwa kuthibitishwa na watu hao hao wa CCM walioichoka.
 
Chadema ina changamoto ya kulinda kura, CCM wamejipanga vizuri waweze kushinda kwa njia yoyote!!!!!!! eg Kawe tunashuhudia mchezo mchafu wa kuchakachua majina ya wapiga kura, NEC inahusika. chadema mu wa train vijana waadilifu ili waweze kulinda kura zenu zisiibiwe hasa kwenye majimbo ambayo mna uhakika wa ushindi. like Kawe, Vunjo, musoma, Arusha mjini,etc. lindeni kama vijana wa Tarime au Moshi mjini wanavyofanya.
 
Kazi kweli kweli kwa CCM. Na hizo shahada wakizinunua, zinawasaidiaje kushinda? Ebu nijuze
 
Kazi kweli kweli kwa CCM. Na hizo shahada wakizinunua, zinawasaidiaje kushinda? Ebu nijuze
Wakinunua wewe unayeunga mkono upinzan unashindwa kupiga kura. Then ile kura uliyoshindwa kupiga wewe inapigiwa m2 wa ccm na kuingizwa kinyemela kwene kituo ulichojiandikisha
 
Jana nilikuwa maeneo ya Mkuranga pale mjini napiga dawa ya viatu, kulikuwa na vijana kama kumi wakasema jamaa waliodai ni CCM wamewafuata kununua shahada kwa Tsh 5,000 wale vijana wakasema pamoja na dhiki tulizonazo hata kwa Tsh 30,00o hawauzi shahada zao- bIG up vijana
 
Back
Top Bottom