Museveni afanya kufuru-ateua mawaziri 76...........

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Hii unaweza kudhani ni kituko lakini ni kweli.Rais wa Uganda ameliomba bunge la nchi hiyo na hatimaye kuridhia ateue mawaziri 76.Alipokuwa anahojiwa na Idhaa ya BBC leo kama haoni kitendo hicho ni ufisadi wa wazi bila kumung'unya maneno Museveni aling'aka na kusema kwake yeye idadi ya mawaziri sio tatizo.Bila aibu alisema marekani wizara moja tu ya mambo ya nje ina mawaziri wa nchi 10.Akahoji ni nini cha ajabu Uganda??
Nilishtuka na kusema Mungu aepushilie mbali tusije Tanzania kujiingiza kichwa kichwa kwenye shirikisho la kisiasa na watawala wa aina hii.Ni bora tubaki na mama yetu Tanzania vinginevyo tutajatawaliwa na madikteta wa kutupwa...........
 
Pengine ana hoja. Anasema tatizo siyo wingi au uchache wa mawaziri bali kukosekana kwa maendeleo. Maendeleo yanaletwa na mambo mengi likiwemo la utashi wa kisiasa na uwajibikaji. Rais wa Tanzania anaishia kuwalalamikia mawaziri wake aliowateua kwamba ni mzigo. Mzigo huo anapaswa kuutua nani?
 
Museveni will definately make the Regional Intergration Project in East Africa very difficult to achieve; the harmonization of regional policies will be an impossible task given his dictatorial tendancies!!
 
kuwa na mawaziri wengi executives kunaonyesha kuwa ama anayewateua ni mvivu kiakili na kimwili hivyo hawezi kutumia bongo yake kuiendesha nchi AU hata hayo madubwana mengi yanayopewa uwaziri upstairs ni sifuri na hivyo ni bora yawe mengi ili kutoka katika wingi wao upate mchele kidogo.

Hata hivyo kwa uchumi wa nchi zetu hasa TZ na UG tunapaswa kuwa na mawaziri wasiozidi 15 na bunge lisilozidi wabunge 120-150 tu. Badala ya kugeuza mabunge kuwa talk show centres.
 
fmpiganaji: 'Nilishtuka na kusema Mungu aepushilie mbali tusije Tanzania kujiingiza kichwa kichwa kwenye shirikisho la kisiasa na watawala wa aina hii.Ni bora tubaki na mama yetu Tanzania vinginevyo tutajatawaliwa na madikteta wa kutupwa........... '

Nashangaa hawa wasiopenda Federation kila kitu kwao ni ushahidi wa ubaya wa Federation. Yaani wewe mkuu bado hujui kwamba hata hivi sasa Tanzania twatawaliwa na madikteta wa kutupwa? Kila mtawala, tangu Alhajj, wameua wananchi bila ya sababu: Mwembe Chai, Zanzibar,Arusha.... na bado waona 'twatawaliwa' na democrats?
 
Ni kama ndoto lakini ni kweli Rais Museveni wa Uganda ameliomba bunge na hatimaye limeridhia yeye kuteua mawaziri 76.Nilimsikia leo asubuhi akihojiwa na Idhaa ya BBC ambapo aliulizwa kama haoni ni ufisadi kuwa na baraza kubwa namna hiyo.Kwanza alimshangaa mwandishi aliyemuuliza swali na akamwambia mbona hashangai Marekani wizara moja ya mambo ya nje ina mawaziri wa nchi (kumi) 10? Akasema kama hilo linawezekana marekani kwanini lisiwezekane Uganda?
Nilisikitika sana baada ya majibu hayo na nikaililia Afrika.Mwishoni nikamuomba Mungu aepushilie mbali shirikisho la kisiasa Afrika Mashariki kama viongozi wenyewe ndio kama huyu.Ataibomoa Afrika Mashariki.Ni aheri tubaki na mama yetu Tanzania.......
 
Museveni is a big disappointment. Alivyoingia madarakani alisema tatizo moja Kubwa la Afrika ni viongozi wasiotaka kuachia madaraka. Sasa yeye mwenyewe kawa mmoja WA hao viongozi.

Huyu mpuuzi anajilinganisha na Marekani wakati anategemea misaada ya Marekani.
 
ndio hapo sasa,uongozi afrika bora ungerudi wa kifalme tu tujue moja
hii "demokrasia" ya kiafrika ni uhuni mtupu na ubabe M7 ni noma yule mzee
 
Ni kama ndoto lakini ni kweli Rais Museveni wa Uganda ameliomba bunge na hatimaye limeridhia yeye kuteua mawaziri 76.Nilimsikia leo asubuhi akihojiwa na Idhaa ya BBC ambapo aliulizwa kama haoni ni ufisadi kuwa na baraza kubwa namna hiyo.Kwanza alimshangaa mwandishi aliyemuuliza swali na akamwambia mbona hashangai Marekani wizara moja ya mambo ya nje ina mawaziri wa nchi (kumi) 10? Akasema kama hilo linawezekana marekani kwanini lisiwezekane Uganda?
Nilisikitika sana baada ya majibu hayo na nikaililia Afrika.Mwishoni nikamuomba Mungu aepushilie mbali shirikisho la kisiasa Afrika Mashariki kama viongozi wenyewe ndio kama huyu.Ataibomoa Afrika Mashariki.Ni aheri tubaki na mama yetu Tanzania.......


This is a joke
mawaziri 76 kwa nchi kama uganda kwa uchumi upi na hapo kila wizara inahitaji kuwa na wafanyakazi wake na mishahara na usafiri na posho na kila aina ya matumizi
Wanaifanyia nini uganda mawaziri wote hao
 
Analipa fadhira kwa ndugu,jamaa,na marafiki ndio tatizo la kuingia madarakani kwa mlango wa nyuma
 
Siku zote viongozi huwa wanatoaga mifano pale wanapotaka mambo yao yaneemeke
Ila ikija wakati wakupewa mifano ya kuachia madaraka kama wenzetu huwa wanadai umetumwa na Africa
hilo haliwezekani.
 
Uganda haifiki hata nusu ya Tanzania iwe na mawaziri 76 au ndio hayo mafuta yaliyopatikana ndio yanamtia wazimu mmh makubwa
 
Back
Top Bottom