Museven hii kiboko

Mambo Jambo

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
1,100
81
mu7.JPG


Hakuna Jua wala mvua lakini jamaa anaonesha tofauti yake yeye na binadamu wengine.
 
Halafu tunalalamika umaskini, huyo mlinzi wakati huo angekuwa anafanya shughuli nyingine ya ujenzi wa nchi badala ya kubeba mwavuli wakati hakuna mvua wala jua, na jamaa yuko chini ya kivuli cha mti.
 
mu7.JPG


Hakuna Jua wala mvua lakini jamaa anaonesha tofauti yake yeye na binadamu wengine.

...tahadhari muhimu bana, unaweza 'pigwa konzi' na mungu. Au ushasahau Prez wa Zambia alivyoumbuka kukaa chini ya miti..?.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=3T-1r18pqZY[/ame]​
 
Viongozi wa africa wanapenda sana kujitweza, japo nchi zao maskini. Viongozi wa dunia ya kwanza wapo simple tu, hawana hata mambo makubwa ya kujiona kama hayo ya Mu7. Mie huwa nawaona ni malimbukeni viongozi wa jinsi hii ya Mu7.
 
Hapo ndo panakuwa pagumu kwa ma presid wetu wa kiswahili kuachia ngazi...akifikia mwisho wa muda wake atarekebisha tu Katiba au kuingia kwenye jeshi la waasi ili aendelee kula "masengweji" vichakani !!!!, kwa hali hii mwavuli atapata wapi mtaani ????.......Hawa ndo viongozi wetu wanao simama majukwani na kuhamasisha "USAWA" na "UPENDO", shit, unafiki mtupu!......


Hata kama kuna mvua, hako kajamaa kalikoshika mwamvuli hakaloi, au sio kabinadamu hako au ndo mafungu ya kufanya "siteti hausi" yanakamaliza hisia za kibinadamu, hata hakasikii maumivu ambayo Mukubwa anayakwepa,duh???.Aka ka nidhamu ka "steti housi" hakana tofauti kabisha na kale ka utumwa enzi za kina sultan Sayyid Barghash bin Said Al-Busaid kule Mkunazini ina kila aina ya kukiuka haki za binadamu!......Loh!!!.
 
Oyaa! kuna kunguru bana.,......watamnyea mkulu bila kuweka mwavuli.

Kweli bwana sio kunguru tu, bali hata nyani ambao wanasaidia kuexpress hasira za wananchi kwa viongozi wao, unakumbuka nyani alivyofanya mambo ikulu ya Zambia???
 
Back
Top Bottom