Ni kweli kabisa ajali hiyo imetokea, na limepinduka mara 3.
Eneo la Mkolani-Buhongwa ni baya sana kwa hapa Mwanza, magari hukimbia sana na kuna kona 3, hakuna matuta na kuna mteremko mkali. Eneo lilipopindukia gari ni Darajani (kati ya Mkolani na Buhongwa). Ila kwa taarifa za uhakika, hakuna mauti katika ajali hii, ila walikuwemo wanafunzi wengi wa SAUT. Ni basi la princess Muro-YUTONG.
madereva hawana huruma na abiria. Ingepitishwa kanuni kuwa kila gari la abiria liwe na nambari za simu za polisi wa
usalama barabarani ili inapotokea basi linaenda mwendo kasi kiasi cha kuhatarisha usalama wao waiarifu polisi.
Sasa kama anaweza kwa nini hakuepusha ajali in the first place, ili asije tena kuhangaika kuwaponya? Huyo Mungu mnavyomuelezea utadhani power Mabula!halafu MUNGU huwa anaweza kuokoa awezavyo pamoja na ajali kuonekana mbaya kuliko. 25 wamejeruhiwa, lakini 6 kati yao hali zao si nzuri.
naona tbc hawapo makini-taarifa ya jana asubuhi wao wanaisoma leo kama breaking news,ni jambo la ajabu sana...hii ajali ilitabiriwa au iliotokea leo alfajiri ni nyingine.
hizi picha siyo kweli kwani hayo mabati hayawezi kuhimili mzigo wa tani 10. fikiria basi kama yale ya mohjamed trans, shabiby yaliyopata ajali kama hiyo yalikuwaje? labda kama liliacha njia lakini halikupinduka nitamwelewa mleta maada
Sasa kama anaweza kwa nini hakuepusha ajali in the first place, ili asije tena kuhangaika kuwaponya? Huyo Mungu mnavyomuelezea utadhani power Mabula!
Anyhow, mwendokasi mara nyingi ni mchango wa abiria. Last year nimepanda Shabiby likawa linaenda mwendo wa wastani sana, halafu Shabiby lina tabia ya kusimama simama njiani kupandisha wanafunzi basi abiria wakaanza kulalamika kwamba hawafiki. Nikawashanga sana nikawaanzishia full timbwili, nikawaambia, kwani tiketi imeandikwa mnafika saa ngapi? Hakuna mwenye jibu, ila nilikuwa outnumbered nikaonekana mimi ndio kichaa na nina muda wa kupoteza barabarani. Yani hakuna mwenye concept ya road safety. Nadhani hata safety records zake ni nzuri hili basi, bahati mbaya linaishia Dodoma tu from Dar nadhani.
Zamani eeh? Kwa hiyo unanambia ndugu yangu nikisema power Mabula inawezekana kuna a whole generation humu hawajui what I'm talking about? Duu, kumbe kweli nimezeeka aisee! Alikuwa analetwa shuleni kwetu kufanya miujiza, mara kachomwa bisu la tumbo hafi, mara kala moto haungui, mara kazuia landlover kwa jino la mbele! Nilivyokuwa mkubwa na kuelewa ule usaii nikagundua kwamba usanii wa Mungu ndio worse zaidi kwa sababu angalau power Mabula unamuona na kumgusa!umenikumbusha mbali sana.
.... we unadhani nani kaepusha