Muokoeni mama yangu

Hapo haitajiki sheria grey area kubwa sana cha msingi ni maarifa, na ni rahisi kabisa kwa sababu baba ni mlevi. Ngoja nifikirie linchpin ili dominoes zianze kufall.
 
@ Bondpost, sina cha kukulipa ndugu yangu, from your post i have learnt alot, kikubwa kuondokana na hofu ya hatma ya jasho la mama. Labda niongeze kwamba kesho mungu akijalia nasafiri kwenda nyumbani kwani mama kanipigia kuniambia mdingi kaliwasha toka last week. I believe am going home like a first born thanks to you. Ombi langu ni kukuomba upokee updates zangu on the situation na mungu akuongeze nguvu na maarifa katika kunishauri. May god bless you
 
On second thought, given that the school is under his name and some of the properties too, can he sell them and if so how can we stop that from happening? And with the constant emotional torture akilewa na kumsumbua mother kwa mikwala, how can that be tamed?
 
Baba namjua sana, ni mjanja sana katika kesi kesi, naimani nikimuomba tukae tuongee kifamilia ataleta hoja kwamba wote tupo against him, kibaya zaidi atapata point ya kumsingizia maza kwamba kapanga njama na wanae. SWALI: Approach gani effective itakayomfanya aheshimu wito at the same isimnyime mama usingizi?
 
At this point naomba niwashukuru wote mliopata mda kushare ma experience and pain regardless of who and what he or she said, making a point to read my post was encouraging enough may you all be blessed na mungu awaepushia yalionifika mwenzenu
 
Poleni sana,
Hata hivyo mshukuru Mungu kuwa mama yenu alipona kuambulia
marazi.
 
Nenda na huo ushauri niliokupatia kamuelezee mama, msikilize kwanza yeye anachokitaka haswa ni nini ndipo tutaweza kushauriana zaidi.
Suala la baba kujimilikisha mali sio tatizo, mahakama inaangalia ushahidi ndugu, wala haiangalii mambo atakayoyazua tu, kumbuka mahakama ndio sehemu pekee mtakayopata suluhisho la kudumu.
Ila soma vizuri yote niliyokushauri. Nashindwa ku-quote vifungu maana vitakuchanganya tu since wewe sio mtaalamu wa sheria but otherwise hayo yote ni msimamo wa sheria.
Kumbuka mahakama inamaamuzi yake na sio kila unachotaka utapata but at least mtakuwa na msimamo wa kueleweka na kumuweka baba yenu katika utaratibu madhubuti kwenye mambo kadhaa mnayoyalalamikia.
Cha muhimu ni mama afanye maamuzi, otherwise there is nothing you can do mtabaki kulalama na kuaibisha familia yenu.
Thats all. Ukitaka ushauri zaidi, tafuta mwanasheria mzuri wa mambo ya ndoa awasaidie, am ready to be of any assistance at fee mkuu hapa nimesaidia kukupa mwangaza wa mambo yalivyo, its more than enough my friend if you happen to read between lines.
Pia waweza kumshauri mama aende nanyi TAMWA, LHRC na kwingine wanatoa msaada wa kisheria bure au kwa gharama ndogo sana ila ndio mfahamu kuwa wao wako busy kwa kesi nyingi.
 
ikifikia hapa ndo pale familia inamwomba Mungu amchukue huyo baba mapeeema!
 
ikifikia hapa ndo pale familia inamwomba Mungu amchukue huyo baba mapeeema!

Ha ha ha haaa! Mnaanza kuingia ubia na ziraili aondoke na huyo kiumbe wake! Duh! Hiyo ni stage mbaya sana.
Ila kuna watu wanaombewa wafe maana ni majanga katika familia. Ila suluhisho ni kumtanguliza mungu tu na kufahamu njia sahihi ya kudai haki yako.
 
Kisa kirefu sana mpaka nimeshindwa kukisoma, "summarize". Unajuwa kila kisa kinapokuwa kirefu uongo unakuwa mwingi. Unatuandikia novo nzima, kisa na mkasa?

Weka mistari mitatu minne yenye nguvu to the point.
 
Kisa kirefu sana mpaka nimeshindwa kukisoma, "summarize". Unajuwa kila kisa kinapokuwa kirefu uongo unakuwa mwingi. Unatuandikia novo nzima, kisa na mkasa?

Weka mistari mitatu minne yenye nguvu to the point.

Dah! Nahisi wewe unataka kujidai ni mathematician! Ila kama umeshindwa kusoma vimistari vichache hivyo sijui wewe upo katika kundi gani!
Labda uwe unaenda kwenye jamii photo panakufaa! Huku ni maelezo kwa wingi mkuu!
Ila na wewe yakikukuta utasimulia tu, ngoja tusubiri.
 
Dah! Nahisi wewe unataka kujidai ni mathematician! Ila kama umeshindwa kusoma vimistari vichache hivyo sijui wewe upo katika kundi gani!
Labda uwe unaenda kwenye jamii photo panakufaa! Huku ni maelezo kwa wingi mkuu!
Ila na wewe yakikukuta utasimulia tu, ngoja tusubiri.

Si andika novo uuze.

Hapa unaweka summary tu. Mimi nipo katika kundi wasilopenda uongo wa hadithi ndefu ndefu, huko kwenye picha ndio napapenda sana, unaweka mistari kidogo inayoelezea wazi kabisa. Nadhani hujui kuwa picha moja inaelezea maneno elfu moja. Kama unabishaa muulize Kipanya, yake moja inaelezea maneno laki moja.
 
Baada ya kupata nafasi na kuipitia tena stori yako, naona hapo tatizo ni tamaa yako. Mwache baba afaidi. Wacha na hao wanawe wengine wafaidi. Mama hajaja na mali yake hapa duniani na anaondoka yeye tu, hivyo-hivyo kwako wewe, kwa baba yako, kwangu mimi na mwingine yeyote yule.

Kama umewahi kuona raha kupokea, basi jaribu kutoa, si kutoa nauli, si kutoa kilo ya sukari, kutoa kitu ambacho unakipenda kama vile nusu ya mali yako, ukampe mwenye kuihitaji, raha yake haina mfano.

Wacha ubahili na roho mbaya, umetoka kwa udongo utarudi kwa udondo, Hizi mali zipo na zitaendelea kuwepo milele na milele. Wewe Jee?
 
Back
Top Bottom