Jamani wana jf tembea uone, uangalie jinsi Tanzania ilivyo, nilibahatika kwenda kondoa miezi iliyopita hali ya uko hususan miundombinu ya barabara inatisha, mimi nilipanda basi la kondoa via kiteto, yani ile tunaiacha barabara ya kwenda makao makuu ya nchi na chama, barabara yote kuanzia hapo ni vumbi tupu na makorongo mbaya zaidi usafiri wa uko ni shida,watu wanabanana afadhali hata ya posta asubuhi, kwa kifupi wilaya nzima haina lami?
Lami uchwara inaonekana kwenye daraja lilojengwa enzi za mkoloni, naona kwa wakazi wa hapo ambao hawajawahi kutoka nje ya wilaya yao lami wanaionea hapo, huwezi kudhani kama hapo ndo makao makuu ya wilaya nyumba za polisi utadhani mabanda ya ng'ombe, benki wana moja tu NMB.
Kondoa jinsi ilivyo utadhani si mji wa kihistoria, manake una michoro ya mapangoni na mali kare kibao. Kwa kifupi kondoa ovyo.