Mungu wa Mtikila ni wa Ibrahim, Isaka na Yakobo?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
WADAU niko katikati ya nchi najaribu kufuatilia mjadala wa watunga sheria katika mjengo wao.

Wote mashuhuda namna juzi walivyomshikisha adabu Dk. Magufuli ambaye anatamba kuwa ni mtoto wa mfanyakazi na pia ni mtoto wa mkulima.

Watunga sheria wa kutoka mjengoni wakasema hapana, hapana kwa kutunga sheria ya unyang’anyi ya kutaka kuwaacha maskini wafugaji kama wale wa Kilosa walivyofanyiwa.

Wanataka awepo bosi wa kuamuru mfugaji auze mifugo yake imekuwa mingi, wakahoji mbona mwenye utajiri wa fedha haambiwi apunguze fedha zake? Mbona mkulima haambiwi apunguze mashamba yake? Iweje mfugaji tu ndiye aambiwe apunguze mifugo yake.

Hilo likawa neno, watunga sheria wakamshauri Magufuli auondoe muswada huo na akajipange upya, Naibu wa Spika akasema hapana umeshakuja mjengoni; lazima uendelee kujadiliwa.

Matokeo yake wabunge wakamgomea Magufuli. Hao ndio wazee wa kutunga sheria, wanapoamua wanaonesha kwamba wao si mihuri ya kupitisha sheria mbovu.

Wanaamua kusimama na kusema hapana kwa hili. Yawezekana ni kwa kuwa uchaguzi unakaribia? Tuachane na hayo wadau wangu, turudi kwa mchunga kondoo wa Mungu, Christopher Mtikila ambaye juzi kabambwa tena na polisi kwa makosa yale yale ya kukashifu.

Mtumishi wa Mungu mwenye kuongoza kanisa kila siku anaingia matatani kwa kukashfu, kumbukeni aliwahi kufungwa kwa kumkashfu Mr Ben na ana kesi nyingine mahakamani ya kumkashfu Mr Jk.

Iweje mchungaji huyu awe na tabia za namna hii. Sisi waumini wake tutajifunza nini kwake? Kama kiongozi wetu kila mara anaingia matatani na polisi kwa makosa yale ya kukashfu, au kanisa lake hilo ndilo fundisho lake kuu?

Maana kama sio itikadi ya kanisa lake iweje yeye kila siku atende kosa kama hilo kila mara. Sisi waumini wa Kanisa la Wokovu tunasikitika kwa hili na naamini kwamba Mungu anayemtumikia hataki mafundisho haya ya kukashfu iweje kila siku atende kosa hilo.

Je, ana Mungu mwingine anayemwabudu au ni huyu huyu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo? Kama ni Mungu yule mwenye wivu anayewabatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne, basi Mtikila atakuwa amekosea kuchagua wa kumtumikia.

Kwani kama yeye na nyumba yake wangechagua kumtumikia Mungu huyo mwenye wivu kamwe asingekuwa na tabia hizo. Dini yake inahubiri uvumilivu, upendo na kusameheana.

Ndio maana nahoji jamani watumishi wa Mungu huyu Mchungaji Mtikila anamtumikia Mungu gani? Sidhani kama anamwabudu Mungu wa Yakobo. Labda wadau nisaidieni kuhusu kiongozi huyo nyie mnamwonaje? Ni kweli anamwabudu Mungu wa Mbinguni?
Niandikieni sagatik@yahoo.com
 
thread yako ina kosa relation, kwani umeanza na mambo ya magufuli then ukaja na mtikila ambapo hata kwa mtikila uyo hujaonyesha uhusiano wa suala la kukashifu na kanisa lake! umezungumza suala la mungu mwenye wivu cjui umemaanisha nini! labda unieleweshe kidogo ili niweze kuchangia
 
Uzi huu kwa kweli haueleweki. Mkuu, nyoosha uzi ili tuweze kuufuatilia na kuurefusha. Huu wako una kona tele, hausomeki.
 
Back
Top Bottom