Mungu si mfanyabiashara!!!!!!!!!!

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Habari wana Jf!Ni jumapili nyingine ambayo wote kwa namna moja au nyingine tumepumuzika nyumbani ijapokuwa sio wote waliopumzika majumbani!Leo nataka tushee yale tulioyapata kwenye nyumba ya mungu,ukizingatia leo ni Siku ya Bwana!

Kwa sababu mfumo wa mawazo ya watu siku hizi ni wa kibiashara basi nitaweka bidii yote, nguvu yote, akili yote na sala yangu yote katika lile jambo ninalolitaka na nitafanikiwa. Hii si imani bali ni biashara. Uhusiano wangu na Mungu unakua juu ya kile anachoweza kunipatia, ama lile janga ninalotaka aniepushie. Ninasali nikitaka Mungu anitimizie mapenzi yangu. Hii si imani sahihi. Imani ni kutaka mapenzi ya Mungu yatimizike kwangu bila kujali madhara na mwisho wa hayo yote.

Ukimuona mkristo anakimbia kutoka kanisa moja kwenda jingine kwa sababu anataka aombewe juu ya jambo fulani na baada ya kukaa kwa muda bila mafanikio anakimbilia kanisa ama dhehebu jingine, hii ni dhalili halisi kwamba mkristo huyu hana imani ila yeye ni mfanyabiashara. Anamchukulia Mungu kama mwezi katika biashara (business associate) na hii si imani kama anavyoonya Yesu. Kudumu katika maombi ni jambo moja, lakini kudumu katika imani wakati unamilima na mikuyu katika maisha ni jambo jingine.

Imani ya kweli ni kuamini kuwa Mungu atakufufua wakati ambao unabeba msalaba, na miiba kichwani kuelekea Kalivari ambapo unauhakika utatundikwa na kufa. Imani inayosisitizwa na Yesu si lazima iuondoe msalaba. Ni vyema kuomba Mungu auondoe msalaba lakini siyo kwa mapenzi yetu bali kwa mapenzi yake, ( Rej. Mat. 26:39).
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom