"Mungu nijalie niwe Mwanamke"

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Mwanamume mmoja alimuomba Mungu amjalie ageuke kuwa mwanamke kwa sababu alihisi mke wake anafaidi kubaki nyumbani wakati yeye anapiga mzigo masaa kumi mfululizo.

Mungu hakuwa hiyana, asubuhi alipoamka, akajikuta tayari amekuwa mwanamke. Harakaharaka akamtayarishia "mumewe" chai, ili ahawahi mzigoni, akakogesha watoto, akawapa chai na kuwatayarisha kuwapeleka shule. Wakati anarudi, akapitia sokoni kununua mahitaji ya siku. Kufika nyumbani, akaanza kusafisha nyumba na kufua nguo. Wakati anataka kutayarisha chakula, akagundua kuwa umeme umekatwa kwa sababu ya deni, ikabidi atoke mbio kwenda kulipia bili ya umeme. Alipotoka kule, wakati wa kwenda kuwachukua watoto ulishafika, ikabidi apitie shule. Kufika nyumbani, akaanza kutayarisha chakula huku watoto wanamlilia njaa.

Kwa ufupi, hadi kufika wakati wa kulala, bado hakuwa hajamaliza kazi zote, ikambidi aingie kitandani hivyo hivyo. Kitadani nako hakukuwa na kupumzika. "Mume" alitaka apewe kidogo, hakumkatalia. Lakini baada ya kumaliza tu akamwomba Mungu:

"Mungu wangu, nimefanya makosa, kwani kazi anazofanya mke wangu ni kumbwa kuliko nilivykuwa nikifikiria. Naomba unirejeshe katika hali yangu ya zamani".

"Hakuna tabu kiumbe wangu", Mungu alimjibu na kuendelea "ombi lako nimelikubali, lakini itabidi usubirie miezi tisa kwani jana ulipofanya mapenzi na mume wako, ulishika ujauzito"
 
hii ilikuwa hapa juzi, tena ya ki ngeeza, kamata 12%, na usirudie tena.!!!
Asante sana kwa angalizo lako. Mara nyingi huwa zinajirudiia kwa sababsi zote huwa tunaziona. Ninaomba mwongozo tu, nifanye nini ili kujua kuwa ile ninayotaka kutuma mimi ipo tayari?
 
Kwa kweli wanawake hata kama baadhi yao ni mama wa nyumbani mzigo wanaopiga ni mkubwa sana
 
Kazi kweli ndo tunaambiwaga tuwe makini na vitu/watu tunaowatamani....natumai alijifungua salama na akarudia uanaume wake...lol :lol:
 
Kazi kweli ndo tunaambiwaga tuwe makini na vitu/watu tunaowatamani....natumai alijifungua salama na akarudia uanaume wake...lol :lol:
Let's hope kuwa hii ilikuwa ni joke tu, vyenginevyo kama ingekuwa kweli...sipati picha ya bamkubwa na kitumbo chake.
 
Back
Top Bottom