RUV ACTVIST.
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 472
- 110
very poor great thinker, very poor analyst, umetumwa? Walaumu serikali yako, hawakusanya kodi, wezi hakuna vifaa sabau yao. Hata x-ray machine hakuna.siyo kawaida yangu nichangiapo au kuanzisha thread kutumia lugha ya laana. Mazingira yaliyopo yamenilazimu kufanya hivyo. Kazi ya udaktari ina miiko yake. Inahitaji daktari awe na sifa maridhawa. Miongoni mwake ni ukarimu, ucheshi, bashasha, huruma, uadilifu, utunzaji siri, ukweli, upendo nk...... Sifa kuu ni lazima awe na utu. Daktari ajue kuwa ansimamia uhai wa binadamu. Binadmau akiwa mgonjwa anahitaji tiba ili apone. Asipopewa tiba pana uwezekano mkubwa akafariki. Hii inaonesha unyeti na umuhimu wa kazi ya utibabu. Madaktari wanafaa kulijua hilo! je ni sahihi kwa daktari kugoma? nionavyo mimi siyo sahihi. Katika hali yoyote ile, dr hafai kugoma. Akigoma maana yake ni kwamba ameamua kuua watu. Daktari anatamka kuwa anagoma! Ili watu wafe! Nchi tunaipeleka wapi? Mishahara yetu iko chini kwa ujumla. Lkn licha ya mishahara midogo, madaktari wamekua wakilipwa zaidi ya watumishi wengine, ukiweka kando wabunge. Serikali ilikua ktk mgogoro na madaktari baada ya kugoma miezi 2 iliopita. Madaktari walitanguliza madai zaidi ya kumi. Serikali ilijaribu kutatua baadhi ya madai yao yakiwemo kubadilisha waziri, naibu wake na katibu mkuu nyoni. Wameongezewa marupurupu kadha wa kadha. Wameahidiwa kuwa mambo yaliyosalia ktk maombi yao. Hadi mwezi wa nane yatakua yameshatatuliwa. Ile mashine kuu ya vipimo ilyoharibika wameagizwa mafundi kutoka kiwanda kilichoitengeneza au watanunua nyengine. viyuko vya wanaharakati wa bongo wazungu wameasisi taasisi za kutetea haki za binadamu. Zina mema na mbaya. Tangu mgomo uliopita, wanaharakati wamekua bega kwa bega na madaktari wakiwasihi kuendeleza mgomo! Nitoe mfano mmoja. Mama kijo ni mkurugenzi wa legal and human rights centre (lhrc). Ni taasisi ya kisheria ya kutetea haki za binadamu. Haki kuu ya binadamu ni haki ya kuishi. Badala ya kusihi madaktari kutibu wagonjwa ili waishi, wanawahamasisha kugoma ili wagonjwa wafe. Huu ndiyo uanaharakati!!!!? Nauliza huu ndiyo utetezi wa haki za binadamu!? Wanatetea nyongeza ya mshahara na kuignore haki ya kuishi. Wangewasihi madaktari waendelee na matibabu ili nao wasaidiane nao kudai madai yao. Mbona serikali ilikua imeonesha mfano. Imejibu na kutatua 60% ya maombi ya madaktari! angalieni kituko hiki mama kijo hajali watanzania kwa mamia wanaokufa kutokana na kukosa huduma ya kutibiwa. Amehangaika kumtoa ulimboka mwabepande na kumuwahisha icu ili akatibiwe. Uli ni bora kuliko watanzania wengine? Mbona yeye amepewa huduma ya kutibiwa!? Kwa nini wengine wananyimwa huduma!? Nawasihi wanaharakati na madaktari pamoja na wanasiasa wasitishe kuunga mkono mgomo. Wasipofanya hivyo mungu awalaani wote. wakatabahu: Wakuziba