Mume wangu kantongoza

Dah! Ribosome mbona umekuwa mkali hivyo? Basi ntakulipa kwa kunieleleza, kiswahili kinanisumbua, anyways asante kwa mchango, ntatafuta the right word hapo.

Sikuwa mkali ila umenichanganya mpaka sikuelewa unamaanishi nini. Samahani sana kama nimekukwaza.
 
Naombeni jamani tusaidiane hili. Mume wangu alikuwa masomoni nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili, amerudi hivi karibuni. Aliporudi kanunua line ya Airtel ambayo ndio ninayoifahamu. Mie sikujua kumbe mwenzangu kanunua line ya tigo, ambayo hakunambia. Sasa siku moja usiku nashangaa msg inaingia:-

YEYE: Darling mambo vipi? Naona tangu jamaa yako arudi umenitosa
MIE: Mbona mie sikufahamu?
YEYE: Hee! kumbe tuko wengi tunaoiba? Njoo basi tukutane hapa Rose garden

Na mengine meeengiiiii.

Mie nkaushtukia mchezo hapo, ila nkasema wacha nione hii movie mwisho wake utakuwaje. Tukapanga hadi kukutana, bahati nzuri sikuwa na papara. ALHADULILAH! mara nafika eneo la tukio ni yeye huyooo!

Nilighafilika kwa kweli, ingawa hisia zangu zishantuma kuwa kama sio yeye basi ameweka watu wanitrace. Hivi ingekukuta wewe mwana JF mwenzangu, ungeliamuaje hili?

Sasa wewe ulikwenda kufanya nini kama sio kuzini, maana hata aliyekuandikia meseji ulikuwa humjui, kufika tu hammadi!! mmeo kasimama anaku-observe, ame-confirm, eti?!
 
Ndoa za vijana ni kazi kweli kweli!!

Kwani huyo mwanamume alikuwa anampima mke wake mwenyewe ili iweje?

Hivi watu hawaamini kwamba kwenye ndoa watu tunaishi kwa kanuni ya imani?

Haya majaribio ya kuprove kwamba some is guilty ni hatari sana...

Heri yetu tunaoamini kuwa kila mtu ni msafi hadi tuuone uchafu wake!!

Babu DC!!
 
bombu una hatari wewe! Ulienda kweli? lolz

Nilienda mpenz @ neiwa, I wanted to know what is behind the scene, lol. Mara boomb! Nkamkuta jibaba kaweka pozi
 
Last edited by a moderator:
Bahati nzuri huyo mume wa bombu siyo mimi, Kama ni mimi Power angekuja eneo la tukio angefikia kipondo kikali sana ambacho asingekisahau maisha yake yote.

Mamaa, wewe mnyanyasaji wa kijinsia. Sasa huoni yeye alinikosea heshima kunitongoza?
 
Sikuwa mkali ila umenichanganya mpaka sikuelewa unamaanishi nini. Samahani sana kama nimekukwaza.

Usijali my dear, ni mambo ya kawaida tuu kwenye jamii yetu hii. Back to the topic mwenzio sina amani sasa, nifanyeje? Ushauri wako
 
Labda ukute mkataba wa kwanza umeshaisha,then that guy atakuwa na right kukutongoza tena otherwise mmh!

Yaani we acha tu! Ndoa yenyewe hata 3 years haijamaliza ndo yashaanza hayo
 
Sasa wewe ulikwenda kufanya nini kama sio kuzini, maana hata aliyekuandikia meseji ulikuwa humjui, kufika tu hammadi!! mmeo kasimama anaku-observe, ame-confirm, eti?!

Eeh! Usinijudge hivyo jamani, sikutaka tu kuweka mambo yote hapa. Ila najua hata wewe ungetamani kumjua ni nani huyo ambaye anakufahamu hadi kuelewa kuwa mume karudi safarini
 
Is this a true story Bombu?...if it is then am kind puzzled usiku wachat na mtu usiyemfahamu na anakuambia mkutane sehemu ya starehe nawe pasi hiyana waenda, binafsi nashindwa kuelewa lengo lako lilikua ni lipi haswa.
 
Ndoa za vijana ni kazi kweli kweli!!

Kwani huyo mwanamume alikuwa anampima mke wake mwenyewe ili iweje?

Hivi watu hawaamini kwamba kwenye ndoa watu tunaishi kwa kanuni ya imani?

Haya majaribio ya kuprove kwamba some is guilty ni hatari sana...

Heri yetu tunaoamini kuwa kila mtu ni msafi hadi tuuone uchafu wake!!

Babu DC!!

Heri yenu babu, mie mwenzenu yamenishangaza haya. Anyways wengine wananambia eti ndo upendo huo
 
Is this a true story Bombu?...if it is then am kind puzzled usiku wachat na mtu usiyemfahamu na anakuambia mkutane sehemu ya starehe nawe pasi hiyana waenda, binafsi nashindwa kuelewa lengo lako lilikua ni lipi haswa.

Story ni ya kweli mkuu, ila hapo umeniquote vibaya, wala sijaweka neno usiku. Mie usiku huwa nazima siku kwani sipendi usumbufu nkilala, na,hapo rose garden nlienda muda wa lunch kwa sababu ni jirani na ofisini kwangu
 
alikuwa amekosea namba kuna demu wake mwngne alkuwa anamtafuta..

Hahaa, na hili nalo laweza kuwamo. Ila mie namuamini, na muda wote akiwa huko nlimwombea arudi salama tuijenge family yetu. Kumbe mwenzangu ndi ivo tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom