Mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile

Kweli binadamu tuna tabia tofauti, suala hili hata kwa wale wanaopenda kujaribu jaribu mambo huwa hawawezi kufanya kwa wake zao labda kama jaribio hufanya kwa ma proffesionals na inasemekana hata price huwa iko juu kwani madhara yake yanafahamika.

Tabia hii huleta matatizo sana wakati wa kujifungua kama mtu atabahatika kupata mtoto na aibu hii huwa haijifichi kwani manesi huwa wanafahamu kwamba mwanamke anayetendwa hivi uwezo wake wa kusukuma mtoto huwa ni mdogo hadi jitihada za kitaalamu zifanyike, sasa kweli mtu na akili yake timamu anafanya hivi kwa mkewe, aibu gani hii jamani.

Pole dada huna ndoa hapo huu ni mkusanyiko wa wahuni mlioamua kuishi pamoja, usikae kimya hii ni balaa na udhalilishaji uliopita kikomo. Watu wanao heshimiana na kupendana kama ndoa inavyopaswa kuwa hawatendeani hivi!!
 
hahahaa Masa alinielewesha anachomaanisha sio tiGo hahaaaa utabaki nje wewe shauri yako mpwa!!!!!

Hehehehe hata mm najua umerudi kundini kama Kondoo upo chini ya mchungaji Masa
 
Huyu mume ana pepo wa ukatili binadamu kama binadamu huwezifanya unyama wa aina hii!! Suala hapa si kutaka kupewa mlango wa uwani la hasha suala ni ukatili anaoutumia kwa kulazimishia kupata hicho kitu. Kusema ukweli imeniuma sana eti unaanguka na kupoteza nguvu ye anakugeuza na kukuingilia?? Jamani angemaliza hiyo starehe yake na kukukuta umeshazimika moja kwa moja angesemaje?. Hapana huyo ana yake kwani mlimdai mahari ya kiasi gani? Je wakati wa uchumba na urafiki hakuwa na vitabia vilivyokuwa vinaashiria ukatili? ah kumbe muhusika hayupo?

We kaizer hebu njoo ukaniulizie maswali yangu kisha uje uniletee majibu hapa ndo niendelee ama sivyo nafunga bakuli langu. Umeniuzi!
 
hivi hii sredi inazungumzia nin?...

tumeezungumza saana kuhusu huyu mama anayeliwa kinyume na maumbile na mumewe..

plz karibu ufanye recapitulation afu tuendeleeeeeee
 
Binadamu anastaajabisha sana, pamoja na utashi wote anafanya vitu vya ajabu.Wanyama pamoja na kukosa akili na utashi hawawezi kuingiliana kwa mtindo huo.Tuwaeleweje binadamu wa aina hiyo.Naona hata nguruwe watauona ufalme wa mungu.
 
teh teehh..vumilia dada wahenga walisema mvumilivu hula mbivu.si ulisema kwa shida na raha huyo ni wako sasa vumilia wala hakuna madhara yoyote utakayopata.hata mimi wifi yako alikuwa anaogopa mwanzoni lakini siku hizi kishazoea mwenyewe anataka iyo kitu
 
........Moyo wangu umeniuma kwa kweli, hii dunia sijui inaelekea wapi!! Hivi kwa nini mwanaume unakuwa katili kiasi hichi jamani? Mkeo ulimpenda, mkafunga ndoa halafu leo unamfanya mwenzio kitenesi kwa kumpiga kisa tigo.

Huyu dada inabidi aondoke hapo, huyo si mume bali ni mnyama.Asingoje apewe talaka hapo, inabidi hata kama talaka ajipe mwenyewe na kuondoka.Huyu mwanaume si binadamu wa kuishi naye, maana huo ni mchezo wake wa kutaka nyuma.

......Kipindi walipokuwa wachumba sijui hakujua tabia ya huyu mwanamume, hadi akakubali kuingia katika ndoa? Miezi sita ya ndoa moto umeanza kuwaka eehhhhh!!

Utakuta hata kazi huyu dada hana, maana mtaji ndio hivyo tena kachukuliwa na huyo mumewe katili.
Imeniuma kwa kweli, I wish ningejua yupo wapi huyu dada kwa hapa Dar nifatilie hii issue.
 
najua hizi pole hazimfikii huyu dada kwani hayupo hapa JF. maoni yangu ni haya... sikweli kuwa ndoa ni ndoano. anachodai huyo baba ni kinyume kabisa na mkataba wa ndoa na maadili ya watanzania. ushauri wangu kwa huyo dada ni kuwa alifikishe hili suala mbele ya watu ambao anadhani wanaweza chukuliwa kama washauri wazuri, huko akatoe msimamo wake juu ya hilo, hapo kama jamaa ataona bado ni haki yake kufanya ulawiti basi mama anahaki ya kuomba talaka.
kama huyu dada ni mkristo ampeleke huyo baba kwa wazee wa kanisa au wachungaji. ninauhakika wakristo wote wananjia zinazofanana ktk kushughurikia matatizo ya ndoa, nasema hivyi kwakuwa mimi ni mkristo. huko hilo jambo litajadiliwa sirini- ninamaana halitatangazwa kwa jamii , kwahiyo dada asiogope kumtia aibu mumewe. huko dada hatashawishiwa kukubali kuingiliwa kinyume, bali huyo bwana ataelimishwa madhara ya anachotaka kufanya kimwili na kiroho, hivyo mume mbaya anaweza kuwa mume mzuri- ni mpaka atakaposisitiza kuwa hataacha hiyo tamaa ya hiyo dhambi, basi mama ufikilie kumuacha.
 
Yohana 14 : 1-18 .....aliyeniona mimi amemuona baba yangu aliyenipeleka....Filipo akamwambia utoneshe Baba yatutosha,.....Filipo nimekuwa pamoja nanyi hata usinijue?.....(wapo watu wanao kataa Yesu si Mungu ili watende mambo kama hayo kwa wake zao....imeandikwa mambo yote yatapita lakini neno litasimama....
E Mungu baba kwa jina la Yesu aliye hai, wewe ndiye mwenye uwezo wa kumnusuru dada huyu katika hali ile mbaya naagiza malaika zako wa Mbinguni kumwokoa na ufirauni wa mume kwa jina la Yesu, .....ukasema kaeni ndani yangu nami ndani yenu ili muwe salama, ninaamini hatotendewa tena matendo hayo machafu tangu sasa kwa jina la Yesu Ameeni

Nafikiri hapa kuna practical problem linalohitaji practical solution??? A material problem ambayo imeshavuka mpaka kutoka its spiritual base, ijapokuwa bado vimefungamana, hivyo solution yake nayo lazima iwe material solution iliyovuka mpaka wa it's spiritual base ijapokuwa viendelee kufungamana hivyo hivyo. Kama hivi.

1. Ajicheki yeye mwenyewe kwanza alikosea wapi kabla hajaingia katika ndoa hii. Hamtahini Mwenyezi Mungu mja kutokana na mambo ya haramu. Kama alikosea, yaani pengine aliingia katika ndoa hii kinyume na ridhaa ya wazazi wake waadilifu, then amejitakia, ajute kwa Mola wake, na amuahidi Mola wake na yeye mwenyewe katu kutowa-overide wazazi wake wanapompa ushauri halali katika mambo ya halali ambayo mamlaka wamepewa na Mungu. Moja ya halali za wazee ni kuhusu ndoa za mabinti zao, na mamlaka ya wazazi juu ya ndoa za mabinti zao ni kuwalinda kutokana na mambo kama haya. A-reflect alikutana vipi na huyu jamaa na a-take action kama hapo juu. Kuyafanya hayo ndani ya moyo wake ndio driving force ya yajayo.

2. Ajue kwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha kuabudiwa mwengine yeyote asiyekuwa yeye, awe baba, awe mama, awe mume, ijapokuwa amewapa mamlaka fulani fulani mmoja juu ya mwengine, distinctions za madaraja na mamlaka haya yamo hata katika mila za kila jamii, madhehebu nk. na karibu mila na jamii nyingi za Tanzania ni nzuri, ama mimi namkaribisha a-search ni vipi uislamu unaweka daraja za kila mtu katika jamii, wazazi, watoto, waume, wake, nk, nk. Mapenzi, hofu, utii, na emotional feelings zote sinamstahikia Mwenyezi Mungu peke yake. Na hakuna utii kwa kiumbe yeyote katika kumuasi Muumba. Baba, mama, mume wanstahili tu utii pale wanapomtii Allah (SW), pale tu wanapoondosha utii mbele ya Mwenyezi Mungu, basi ni HARAMU kuwatii.Aidha wanampomlazmisha mja kufanya maovu ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kufanya maovu, basi vita ni halali juu yao, yaani vita ikiwemo kutoana roho, ni halali, mmoja atakufa shahidi na mwengine atakufa kafiri, simple as that. Na hata Chembe tu ya mapenzi kwa kafiri ni dhambi na ni ku-condone au ku-perpetrate the crime, iwe mimi, uwe wewe, awe yeye, awe mume, awe baba, awe mama, awe yeyote yule. Kafikri anaweza kuwa mkristo, anaweza kuwa muislamu, anaweza kuwa pagan, nk, nk.

3. Kwa mume kumtamkia tu mke au mke kumtamkia tu mume, sembuse kumlazimisha. Au kwa mke na mume KUKUBALIANA, TAYARI NI TALAKA. Kisharia hakuhitaji tena talaka ya maandishi wala matamshi. Ni TALAKA, hakuna ndoa tena. Kwa hakika KABISA hata kuendelea kuishi baada ya siku na wakati wa tendo hilo aidha KIMAKUBALIANO au KULAZIMISHWA ni maisha ya ZINAA, kama hayajui hayo, well sasa anajua, na hahukumiwi mtu kwa asilo lijua, aidha baakujua, elimu ni mtego, ajiondoshe na zinaa, ni uchafu, uchafu, MOTONI, MOTONI, MOTONI.

4. Kwa mmoja kumlazimisha mwengine hiyo ni RAPE na KUDHALILISHA UBINADAMU. Katika RAPE kuna (a) MHALIFU (Rapist) na (b) Victim (The raped). Mhalifu anastahili adhabu na victim anastahili protection. Kwa taarifa tu Tanzania sheria zao ni linient kidogo, sijui ni kifungo cha miaka 35-maisha, sina uhakika. Lakini, na akaribie tena mhusika katika uislamu, japo asome tu na kufahamu na kulinganisha na kutafuta nguvu ya kujitetea. Adhabu ya rapist, aliyeoa au aliyewahi kuoa, ni MAWE MPAKA KUFA NA ... Hata hivyo hili hufanywa na dola na ushahidi hutakiwa, hivyo anaweza kulishughulikia baadae akitaka, na hata kama hakulishughulikia hilo, bado dignity yake itakuwa preserved, cha muhimu yeye ni kutoka katika madhila hayo kwanza. Anaweza kumuachia Mwenyezi Mungu hili huko kesho akhera, kwa maana kulishughulikia hapa duniani wakati mwengine unaweza kujiadhiri mwenyewe au kuadhiriwa bila kukusudia. Muhimu kwa yeye ni kutoka hapo. Na kama ana chembe ya masikitiko ya mapenzi kwa kuachana na mtu huyu, basi ni yeye mwenyewe vile vile mwenye matatizo, pengine makubwa zaidi, na hayo ya huyo mume ni mengine. Ana-overide mapenzi juu ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi ya binadamu, HARAMU na adhabu yake motoni.

5. La kufanya ni yeye kuwakutanisha baba yake mzazi na baba mkwe wake (baba mzazi wa huyo mume) na kuwaambia kinaga ubaga. Madaraja yanakwenda hivi kama hao mababa hao hawapo, yaani wameshafariki: Mababu, mababa wadogo, kina kaka, halafu wajomba, nk, nk. Awaweke ana awaambie. Awaambie sio kwa kutaka usuluhishi, la hasha, ni kuwataarifu tu SABABU iliyovunja ndoa yao, maana HAIPO TENA. Na vile vile anawaambia ili wao (HASA BABA MKWE au upande wao) wachukuwe responsibility ya kuwaprotect wasichana wengine watakaokuwa approached na mtoto wao kwa ajili ya ndoa hapo baadae. Hapa anatakiwa uwe very firm and assertive. Hints za ku-stay cool ni kama hivi:
i) Binafsi aweke hofu saaaana kwa Mwenyezi Mungu, naye atawafanya watu wamuhofu yeye na yeye aondokane na hofu ya binadamu
ii) Asifiche kitu chohote, lakini awekee wazi na ukweli ya yaliyotokea na aweke wazi kwamba hana furaha kuyasema hayo bali inambidi kuyasema.
iii) Aweke wazi kwamba hakuwaita wao pale kwa usuluhishi bali amewaita ili kuthibitisha kuvunjika kwa ndoa yake na mtoto au mkwe wao.
iv) Awaaambie kabisa wazazi hao kwamba watakuwa wana-commit haramu na uhalifu kama (a) Hawatofuatilia haraka na mara moja suala hilo na kumuita mtoto wao(mkwe wao) kuthibisha kukataa suala hilo na kuchukuwa hatua zinazostahili (b) Wakikulazimisha kurudi japo kwa usiku mmoja tu kwa huyo bwana, hasahasa awaekee wazi kwamba hayuko hata mmoja wao mwenye haki ya kufanya hivyo kutokana na uzito wa allegations zilizopo mbele yao, ijapokuwa mpaka hapa ni bado allegation tu. Vile vile awaonye wazi na kwa taratibu kwa sauti ya chini, bila ya panick wala zogo kwamba ikiwa kwa njia moja au nyengine (kwa mfano mazingaombwe) ata-back down na kukubali kurudi kwa huyo bwana maana yake ni kwamba: kesho yake wafunge safari ya kuja mjini mazikoni kuzika maana unakwenda huko tu kwenda KUMUUA huyo bwana na kwamba haki ya kufanya hivyo ni haki yako kisharia.

La mwisho katika mkutano iwe kakubali iwe kakataa, yeye asirudi maana ndoa haipo.
- Iwe kakubali : ndoa haipo kwa maana tendo lile limevunja ndoa, na wewe umethibitika mkweli na yeye mkorofi
- Iwe kakataa : ndoa haipo kwa maana kama yeye ni mkweli na muadilifu basi katu hatokubali kukurudisha nyumbani kutokana na allegations nzito za haramu ulizomfanyia, maana mke kumsingizia mume uovu wa liwati mbele ya watu hao hapo juu ni dhambi ambayo mume kama ni muadilifu, basi hutakiwa aivunje ndoa, na kama anailazimisha basi ni muongo huyo.
- Wafunge mkutano kama huyo mume hakukubali "UOVU wake" na yeye mwanamke haukuthibitishwa "USAFI wake" kwa "KIAPO". Baada ya hapo ni haramu kurudiana na yote yaliyojiri yasizungumzwe tena katika level yenu ya kibinadamu bali wamuachie Mwenyezi Mungu amuumbue aliye muongo. Yeye ashughulikie tu na kujenga maisha yake yaliyo mbele yake na asilizungumze tena hilo jambo na yeyote, hata kama ataolewa tena na mume mwengine, amuamini Mwenyezi Mungu kwamba haki yake haitopotea na dignity yake haitashuka as long as anabakia kuwa yeye ndiye mkweli.. Na hata kama huyo mume wa baadae, sio katika mkataba wa ndoa, bali katika maisha na mazungumzo ya kawaida tu nyumbani ni haramu kwake kumuuliza au kumkusemesha maneno na story za past ambazo zitapelekea kupunguza mapenzi baina yao. Amueleze hivyo kwa taratibu, kama ni mume mwema akafahamu na katu asidadisi basi asitoe ofa ya kumwambia kwa imani, na akiwa anamuuliza uliza hata miaka kumi mara moja asimwambie, kwisha habari.
 
kwenye hii sredi nimegundua watu wanajua kuandika...!lol

posti zengine kama magazeti ya mzalendo...!
 
Kwa nini asiende polisi kushtaki??

Aende Polisi wapi na wapi bana wakati masuala ya "kula bata" siku hizi kwa kiasi kikubwa yanahalalishwa na jamii. Hii nyimbo na video yake wakubwa kwa watoto wanaweza kuiskia kwenye Redio na kuitazama kwenye Luninga 24/7


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=tmW34SJENpg&feature=player_embedded[/ame]
 
mficha maradhi kifo humuumbua. kwake imeshatokea, wala sijui kama anasoma huku. cha msingi kwa wadada wa leo. msiende kwa waume mkiwa mikono mitupu! yanaweza kuwakuta mengi mabaya na mkakosa pa kukimbilia. hakikisheni mnakuwa na vyanzo vyenu vya kipato na hali itakapobadilika kwenye ndoa una pa kujishikiza
 
kwenye hii sredi nimegundua watu wanajua kuandika...!lol

posti zengine kama magazeti ya mzalendo...!

......Usishangae Geoff, wengine wana fani ya uandishi wa habari hapa. Anyway hii kitu imegusa wengi bana, tatizo hatuwezi kumpata huyo mdada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom