Mume wangu amenitenga baada ya kupinga manyanyaso ya ndugu zake

Hivi unadhani wote tunao comment humu tuna ndoa za msikitini. Siku hizi hakuna cha until death...mambo yakifika shingoni unasepa tu...Huku unafanya reference kwenye kosa la uzinzi linavyoruhusu divorce.

Hivi unataka kunambia hujaona Wakristu walo divorce??? Ndoa ilikuwa kifungo mwaka 1947 si leo.

Me naomba niulize,hivi kama huyu dada angekuwa amefunga ndoa ya kikristo angefanyaje?inamaan asingeweza kuachika mpaka mmoja afe?na asingeweza kuolewa tena?na kama angepata man mwingine angeishi nae tu lakini bila kutambulika kama ni mke?naomba nielimishwe wadau..
 
Hivi unadhani wote tunao comment humu tuna ndoa za msikitini. Siku hizi hakuna cha until death...mambo yakifika shingoni unasepa tu...Huku unafanya reference kwenye kosa la uzinzi linavyoruhusu divorce.

Hivi unataka kunambia hujaona Wakristu walo divorce??? Ndoa ilikuwa kifungo mwaka 1947 si leo.

Sidhani kama umekuja kwa nia ya kunielimisha,naona unaushabiki ambao siuelewi,hebu shusha pumzi halafu unielimishe..
 
hapo pia ndo ambapo wanawake tunakosea sana manake kama kuwa goli kipa jamani tubadilike hata ile kodi ya meza save mia mia ili ujichezee kamcezo uate mtaji wako manake haya maisha si rahisi kiivyo kama wanavyofikiri. katika utumwa ambao tunapaswa kuuepuka ni ule wa kuwa tegemezi kiuchumi kwa wanaume yaani hio ndo hutumika kama kitanzi aisee. mimi huwa ni mkali sana kwa wanawake wa aina hii wallah kuliko uteseke eti kisa huna mtaj nitafute nikupe kwa riba ukomboke lol!
hapana mimi sio golikipa,ninafanya biashara na zinaniingizia kipato cha wastani ndo mana nimeweza kulea ujauzito mwanzo mwisho,Na hadi sasa namlea mwanangu.
 
Nashukuru sana kwa kunifariji na kunipa ushauri,Naahidi kuufanyia kazi na anzia leo narudi chumbani kwangu na nitakua ngangari kinoma akitaka asepe yeye,NIMECHOKA na nitarudi kuwapa matokeo.MBARIKIWE SANA
 
Ndugu ushabiki uko wapi? Ina maana mi muongo kusema wakristu wana divorce? Sikuelewi?

Sentesi yako ya kwanza imekaa kishabiki ndio maan nikakwambia hivyo,haya tuendelee sasa,kwahiyo wanadivorce na inakubalika kikanisa au inakuwaje? Na wanapo achana wanaandikiana talaka tu au kuna utaratibu unafuatwa?
 
jitathmini dada..nahisi kuna kitu kimejificha ndani yenu.......halafu hapa hii story inatakiwa kuwa balanced,inatakiwa tupate na maelezo ya upande wa pili....
Mimi siamini kama kuna mwanaume anaweza kuwa katili kiasi hicho with no reason....
Lazima kuna kitu hapo....TUAMBIE VIZURI DADA ANGU
wako wengi tu mitaani ila wanakutana na wanawake wanaojua kuvaa miwani ya mbao!huwezi kunitoa chumbani,kama unataka toka wewe!huwezi kunilazimisha niende kijijini nikalee mama yako wakati wewe una dada zako,kama hutaki mama yako akae kwangu,basi dada zako waache waume zao wakalee mama yao.hatoki mtu!mume wangu tukae chini tujiulize tulikosea nini?tuombane msamaha,tuanze maisha upya!waume wa siku hizi bila kusimama kiroho ni vurugu tuuu!simama kiroho dada!
 
yaani sweetlady ukija kwangu nakupa ushauri uwe ngangari siyo nenda beba virago ondoka hapana. inabidi tueke mkakati wa kuwatimua wao wala sio sisi kutimka khaa! mbona kuna watu wanakomaa hadi baba anabeba virago na akienda vikimshinda anarudi na begi lakae kam mkimbizi? hatujaamua tu.

hahahaaa!begi aje nalo atoe wapi?anarudi yeye na miguu yake miwili na nusu!mdogo kama piritoni!mwema yeye utadhani mtakatifu flani!samahani atakuomba urefu kutoka hapa hadi ulaya!kachunwa kachunika hadi kabakizwa mifupa tu!halafu wakati huo anakukuta uko bomba na hujatetereka kimaisha!kuanzia wakati huo heshima na adabu!
 
Pole sana, ila tu MAJARIBU NI MTAJI , Ninaamini wewe utakua Mwalimu mzuri kwa wengine Baada ya kushinda hiyo vita.

Hata kama huyo Bwana hakutaki tena Mungu anaweza Yote

Egemea Kwa Mungu Upate Faraja ya kweli

Mtumainie Mungu Tu Ktk Maisha yako , naye atakuwezesha

MUNGU TU NDIO JIBU LA YOTE HAPA DUNIANI, Chuchumaa Miguuni Pake, Utafarijika
 
sijasoma uzi mzima (i'm under meds), kwa nini asimuache huyo mume au kwenda mahakamani kuomba ndoa ivunjwe?
 
Wengi wanatengana kwanza utaratibu unafuata baadae. It is more easier mkiwa mbali for say 2 years kupata talaka. Hata kama ndoa ni ya kanisani mahakama inavunja tu...ila with time, na kanisa linalainika nalo linavunja tu...nina experience ya watu wa karibu. Kanisa likiona hakuna huwezekano wa suluhu wanavunja ili victim aendelee kushiriki.

Sentesi yako ya kwanza imekaa kishabiki ndio maan nikakwambia hivyo,haya tuendelee sasa,kwahiyo wanadivorce na inakubalika kikanisa au inakuwaje? Na wanapo achana wanaandikiana talaka tu au kuna utaratibu unafuatwa?
 
yaani jitu mmekutana wote mna meno 32 akunyanyase na wewe umetulia tu eti kiapo? kiapo kitu gani?

halafu huyo mwanaume maandiko yanasema mtu mume ataiaha nyumba ya baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja, anapotaka mtoto wa mwanaume mwenzie akakae kijijini ana maana gani?
aambatane na mama mkwe wake?
mama mkwe ana mabinti, kwa nini wasiache ndoa zao wakaenda kumhudumia mama yao? au huyo binti ndo mwenye uchungu sana na mama mkwe kuliko watoto wake?

na huyo kijana nia na madhumuni ya kuoa ni nini? kupata housegirl wa mama yake au ameoa wa kufanan nae? waambatane pamoja?

mke huko kijijini nani atamtimizia haja zake za kimwili? mama mkwe?
na kijana huku mjini nani atapunguza mihemko yake?

tatizo huyo mleta mada hajitambui na hajithamini, muoga wa kuface maisha yake na legelege ndo maana ananyanyasika....
anapaswa kugangamala, saa nyingine wanaume wanahitaji mtu bandidu, akileta ukauzu na mke anakua kauzu mambo yanakaa sawa, lakini ukijinyenyekesha na kujitia unyonge sana matokeo yake ndo haya

Hivi unadhani wote tunao comment humu tuna ndoa za msikitini. Siku hizi hakuna cha until death...mambo yakifika shingoni unasepa tu...Huku unafanya reference kwenye kosa la uzinzi linavyoruhusu divorce.

Hivi unataka kunambia hujaona Wakristu walo divorce??? Ndoa ilikuwa kifungo mwaka 1947 si leo.
 
Ndo mwanzo wa kuleteana HIV...huyo mume wake mihemko atamalizia wapi wife akiwa kijijini???? leave aside mke nae ndio hana hisia???

yaani jitu mmekutana wote mna meno 32 akunyanyase na wewe umetulia tu eti kiapo? kiapo kitu gani?

halafu huyo mwanaume maandiko yanasema mtu mume ataiaha nyumba ya baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja, anapotaka mtoto wa mwanaume mwenzie akakae kijijini ana maana gani?
aambatane na mama mkwe wake?
mama mkwe ana mabinti, kwa nini wasiache ndoa zao wakaenda kumhudumia mama yao? au huyo binti ndo mwenye uchungu sana na mama mkwe kuliko watoto wake?

na huyo kijana nia na madhumuni ya kuoa ni nini? kupata housegirl wa mama yake au ameoa wa kufanan nae? waambatane pamoja?

mke huko kijijini nani atamtimizia haja zake za kimwili? mama mkwe?
na kijana huku mjini nani atapunguza mihemko yake?

tatizo huyo mleta mada hajitambui na hajithamini, muoga wa kuface maisha yake na legelege ndo maana ananyanyasika....
anapaswa kugangamala, saa nyingine wanaume wanahitaji mtu bandidu, akileta ukauzu na mke anakua kauzu mambo yanakaa sawa, lakini ukijinyenyekesha na kujitia unyonge sana matokeo yake ndo haya
 
Wapi wanaharakati wa haki za wanawake au wanasubiria migomo tu kwa watumishi wa umma ndiyo wauze nyago kwenye TV?
 
Wasema nini kaka the Magnificent? Huamini mwanaume anaweza kuwa katili? Hujasikia kile kisa cha mwanaume mmoja huko mkoani mara aliyemburuza mkewe kwenye lami kwa kutumia gari lake?Upo ukatili wa kutisha unaofanywa na baadhi ya wanaume kama huyu mume wa Lonely Heart.

kwa mkoa wa Mara mbona hiyo kawaida sana?? hapo kipi cha kushangaza? huku kwetu tushazoea hayo mambo ni ya kawaida tu.....nataka hii stori iwe balanced,basi....hatuwezi kuyafanyia kazi maelezo ya mtu mmoja....
 
Pole sana ndugu.. Tatizo lako ni kubwa sn unahitaji uvumilivu ulee watoto wako
 
hapana mimi sio golikipa,ninafanya biashara na zinaniingizia kipato cha wastani ndo mana nimeweza kulea ujauzito mwanzo mwisho,Na hadi sasa namlea mwanangu.

sasa mnakwambia hivi kuwa ngangari ndani kwako usibandue mguu kwani yeye alitoka wapi na wew umetoka wapi? akitaka asepe yeye ila si wewe mfungie vioo mwanzo mwisho na pendeza mwanzo mwisho mwanao aish vizuri mbona atarudi uzuri hawana ujanja hasa unapomshindwa kwa jambo kama hili.
 
Wengi wanatengana kwanza utaratibu unafuata baadae. It is more easier mkiwa mbali for say 2 years kupata talaka. Hata kama ndoa ni ya kanisani mahakama inavunja tu...ila with time, na kanisa linalainika nalo linavunja tu...nina experience ya watu wa karibu. Kanisa likiona hakuna huwezekano wa suluhu wanavunja ili victim aendelee kushiriki.

yaani aisee tunatofautiana sana miye ndani angu sitoki toka wewe na virago vyako. n ahuo ndio msimamo wangu so fanya yote nmiye sijali na chumbani kwangu siondoki. manake haya mawazo ya sisi kina mama kuondoka ndio ynayowapa wanaume iburi cha kuona ataondoka niliwah kumwambia hubby hapa ndani hakuna mwenye chake manake mie na wewe sote wajaji tu wenye haki ni watoto so wakitaka wao watufukuze manake hapa ndio kwao ila mimi na wewe hapa tumekuja tu. hakuweza kunijibu na hapo nimefunga vioo hadi mwisho.
 
Back
Top Bottom