Mume wa waziri Kabaka afariki

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Nimepokea taarifa muda huu huu kuwa mume wa Naibu Waziri gaudencia Kabaka, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, nafuatilia kujua hali halisi. Lakini habari zaidi zinaeleza amefariki akiwa nyumba ya wageni aliyofikia jana akiwa njiani kwenda kwenye shughuli zake za kazi mikoani. Taarifa zaidi zafuata baadaye
 
It is confirmed, John Kabaka mume wa naibu waziri wa elimu Gaudensia Mgosi kabaka amfariki akiwa wilayani Tarime. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake,AMEN!
 
It is confirmed, John Kabaka mume wa naibu waziri wa elimu Gaudensia Mgosi kabaka amefariki akiwa wilayani Tarime. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake,AMEN!
 
huyu mzee alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani? au ni kifo cha ghafla tu. Angekuwa amekatwa jina na NEC tungesema ni presha za uchaguzi lakini nadhani mama alifanikiwa kupata kiti maalumu huko Mara
 
Mungu awepeni nguvu na uvumilivu familia ya John Kabaka katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo
 
mUNGU AWAPE HERI NA NEEMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU. nEEMA ZAKE ZIWATAWALE MPATE USAHIDIZI WA KUTOSHA
 
ni mzee mpole ,mtaratibu...mwenye kutoa nafasi kwa mwenzi wake kufanya kazi za kulitumikia taifa.......! poleni wafiwa...!
 


– August 17, 2010

Na Ahmed Makongo, Bunda.

MUME wa Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Gaudensia Kabaka, aitwaye Jonh Marwa Kabaka (63), amefariki dunia akiwa ndani ya nyumba moja ya kulala wageni iliyoko mjini Bunda.

Jeshi la polisi wilayani Bunda limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililotokea usiku wa kuamkia leo mjini Bunda, katika gesti moja iitwayo Nyasa, ambapo kifo cha Kabaka kiligundulika leo asubuhi, baada ya wafanyakazi wake kumfuata ili awapatie fedha za kununua kifaa kimoja cha gari lake lililokuwa limeharibikia mjini Bunda.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya DDH-Bunda, Dk. Mathias Baruya, alisema kuwa mwili wa marehemu unahifadhiwa katika hospitali hiyo.

Mdogo wa Naibu waziri Kabaka aitwaye Kasmu Rinyumunka, alisema kuwa Kabaka aliyekuwa na wafanyakazi wake, walikuwa wakitokea nyumbani kwao wilayani Tarime, wakielekea mjini Mwanza na kwamba walilala mjini Bunda, baada ya gari lao kuwa limeharibika.

Alisema kuwa jana asubuhi wafanyakazi wake walipobisha hodi katika chumba cha Kabaka, hawakupata majibu yoyote na kuamua kumuita mhudumu wa nyumba hiyo, aliyetoa taarifa polisi, ambao walivunja mlango na kukuta akiwa amefariki.

‘Wenzake walipoamka asubuhi walikwenda kumfuata hili awapatie fedha za kununua spea, lakini baada ya kufika waligonga mlango bila majibu yoyote na kuamua kumuita muhudumu wa gesti hiyo na ndipo polisi wakaja na kumkuta amefariki, kwa kweli hatujui chanzo ni nini' alisema Rinyumunka.

Polisi walisema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio walishuhudia mwili wa marehemu ukiwa kitandani na akiwa amevaa nguo zake kama kawaida na kwamba chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.

Waziri wa kilimo, chakula na ushirika Stephen Masato Wassira, na katibu wa CCM wilayani Bunda, Charles Mwangwale, walifika katika eneo la tukio, ambapo waziri Wassira alisema kuwa amesikitishwa sana na kifo hicho, ambapo amesema kuwa wanafanya taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu, kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Matukio ya watu kufia katika nyumba za kulala wageni mjini Bunda yamekuwa yakitokea mara kwa mara, ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja alikutwa amefia katika nyumba moja ya kulala wageni iitwayo Mtabi.

Katika tukio jingine mwanamume mmoja, Kyamarisi Ngochoge, mkazi wa kijiji cha Mugeta, wilayani Bunda, anashikiliwa na jeshi la polisi, baada ya kumuua mke wake aitwaye Christina Kyamarisi, kwa kumkatataka mapanga mwili mzima kutokana na wivu wa mapenzi.

Polisi walisema kuwa tukjio hilo lilitokea juzi majira ya saa 1:30 asubuhi, katika kijiji cha Mugeta wilayani hapa.
Source: RFA
 
Back
Top Bottom