Mume wa Khadija Koppa ambaye ni diwani kata ya Magomeni - Bagamoyo amefariki dunia

Huyu mama omari kumbe anauguza mume halafu anapuyanga2. Jana alikuepo rukwa kwenye tamasha. R.I.P.

hivi inamaana ukiuguza usifaye kazi??mgonjwa atakula nini??
yuko rukwa kikaz je asingekwenda kisa anauguza ilihali anaowatu wanaoweza kumkalizia na yeye akaenda tafuta pesa za kumnunulia mgonjwa dawa?? tuache ujinga wa kuwaza padogo unless umekuwa na mgnjwa wa kitandani kwa muda mrefu ndipo utakapoelewa kwann Hadija Kopa alifanya hicho unachokiita kupuyanga.
 
RIP.Ukiacha watani wa makabila ambao huenda msibani na utani ukawa sehemu ya kuwafariji waliofiwa utani kwa taarifa hizi si jambo la afya njema!
 
RIP Diwani aka Jaffar,
Pole Malkia aka Gwiji wa Mipasho aka Taarabu Khadija Kopa na wote tulioguswa na Msiba huu.


Mume wa Malkia wa Mipasho Khadija Kopa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mogomeni Bagamoyo kupitia CCM Jaffar Ali Yusuf amefaiki dunia mapema asubuhi ya leo katika Hospitali ya Lugalo.

Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema ndugu yao huyo alikuwa anaumwa kwa muda mrufu na alianza kuumwa siku chache baada ya kushinda kiti cha udiwa ni katika kata hiyo. Hata hivyo ndugu hao hawakuwa tayari kusema aina ya ugonjwa uliokuwa unamkabili ndugu yao huyo.


Ikumbuke kuwa Bwana Jaffar Ali Yusuf alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Magomeni miezi michache iliyopita baada ya diwani wa alikuwa anaogoza kata hiyo kupitia CCM Abdalah Mshindo kufariki dunia mwaka jana.


Habari kamili zitakuja kadri tutakapo zipokea

..........................................................UPDATE .................................................................

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

7.JPG



Enzi za uhai wa Mrehmu hapa akiwa na Mkewe Bi Khadija Omar Kopa

Jaffary+Kopa+Kili.JPG
Khadija+kopa+na+Kharifan.JPG
 
jamani mbona hicho kiti kimepata mkosi mara mbili au kuna mkono wa mtu mambo ya uchawi

Hicho kiti kilikuwa cha chadema maccm yakapora kura ole wao kila atakaye kalia bila ridha ya wananchi mauti kumkuta.
 
Rest in Peace Jaffar. Ila ndugu wanaposema mgonjwa kaugua kwa muda mrefu kama mleta mada alivyosema kwani wanashindwa nini kuutaja huo ugonjwa wa muda mrefu. Tunapotoa general and undefined statements zinasababisha maswali mengi sana kwa wasomaji wa habari. Pole sana mama Hadija kwa kufiwa na mume wako uliyempenda sana. Mlipendana hadharani bila kujali binadamu maana hatuna dogo. Hivi msanii Lulu alipotuhumiwa (sijui kama ni kweli maana sikuona hata picha moja wakiwa na Komba) kuwa anatembea au ni mpenzi wa mheshimiwa huyu ni kwa nini hamsemi? Mwanamke akimzidi mwanaume basi utasikia mara mama yake mara bibi yake mara vile. Hivi wale wanaoa wanawake zaidi ya mmoja nipeni umri range wa mke mdogo!!!! Wengine ni sawa na watoto wao na hawasemwi!!! Kabla hatujakosoa basi tuangalie pande zote za shilingi.
 
R.I.P diwani, pole malkia yote mipango ya Mungu na yatupasa tushukuru kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom