gambachovu
JF-Expert Member
- Dec 29, 2011
- 1,854
- 292
........Wana MMU mambo zenu!! Haya leo kuna hili, wewe mdada umeolewa na mwanaume ambaye anakujali. I mean anakupa huduma zote kama chakula, malazi na mavazi. Yaani chochote unachotaka kama ana uwezo nacho anakupa.
.......Ila sasa huyu mwanaume ana matatizo yake, nayo kama hivi:
Hana maneno laini, kama mjuavyo wanawake tunapenda kusifiwa. Hata mkewe ajitahidi kufanya kitu kizuri kama kupika, kuvaa vizuri hajui hata kumsifia mkewe. Watu wa nje watamsifia mkewe lakini si mumewe.
- Mvivu kukutana kimwili na mkewe, sio kwamba ana matatizo hapana. Yaani tendo la ndoa halipi kipaumbele sana.
- Hapendi kutoka out, anaweza kumpeleka mkewe sehemu yoyote anayotaka kwenda, akifika huko yeye anabaki kwenye gari na kumuacha mkewe aende na watoto.
- Wakialikwa sehemu, kama kwa marafiki kupata dinner au mkusanyiko wowote wa watu haendi, lazima atoe udhuru.
Mkewe ameshamwambia muda mrefu kwamba hapendi hiyo tabia yake, na je watoto watajifunza nini kwa baba wa jinsi hii?
Huyu mdada ameniambia mengi kuhusu mumewe, ila mimi nimeshindwa kumwambia achukue uamuzi gani.......nimebaki tu nimezubaa kwa hizi tabia za mumewe.
Kuna mengi yakuandika kuhusu huyo mume wa mtu......sasa jamani mume wa hivi kweli anavumilika? Kama wewe mdada umeolewa na mume wa jinsi hii utafanyaje?
kuna haja ya kujua kabila lake..
Kama ni kabila hilo ninalodhani,avumilie tu... Hawarekebishiki...