Mume wa demu wangu wa zamani

Kuna demu niliwahi kuwa naye halafu tukapotezana 5 years ago, sina hata contacts zake. Leo nimefungua facebook nikakutana na message ya mwanaume nisiyemfahamu ananiomba urafiki wa facebook. Kwa kuwa simfahamu, nikasita, nikaamua ngoja niangalie kwanza profile yake, nikaenda pale kwenye photos nikakuta album yenye picha kama za harusi nikaifungua. Nikakuta kweli ni picha za harusi, na zina maelezo ya tarehe na mahali ilikofungwa ndoa na ukumbi ilikofanyika harusi, picha 37 jumla. Na bibi harusi ni yule aliyekuwa demu wangu.

Imenipa maswali mengi. Huyu mume wake kanijulia wapi mimi, au huwa wananizungumzia? Na kwa nini ananitaka urafiki? Wakuu hii imekaaje, hakuna mtego hapa?

Imegundulika hivi karibuni Facebook kwa kutafuta umaarufu na kujiongezea watu hujaribu kuwaunganisha watu,unaweza kuona friend request kumbe mtu hajatuma,ukijibu inajionyesha kwa yule kuwa wewe ndio unaeomba urafiki.
 
Ataka REVENGE, Huyo bwana ili muwe DRAWWWW!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nimepitia tena hii thread ya 2010 imeniburudisha sana. Kwa taarifa tu ni kuwa hii issue niliimaliza vizuri
 
Back
Top Bottom