Mume wa demu wangu wa zamani

Mtu B

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
919
51
Kuna demu niliwahi kuwa naye halafu tukapotezana 5 years ago, sina hata contacts zake.

Leo nimefungua facebook nikakutana na message ya mwanaume nisiyemfahamu ananiomba urafiki wa facebook.

Kwa kuwa simfahamu, nikasita, nikaamua ngoja niangalie kwanza profile yake, nikaenda pale kwenye photos nikakuta album yenye picha kama za harusi nikaifungua. Nikakuta kweli ni picha za harusi, na zina maelezo ya tarehe na mahali ilikofungwa ndoa na ukumbi ilikofanyika harusi, picha 37 jumla. Na bibi harusi ni yule aliyekuwa demu wangu.

Imenipa maswali mengi. Huyu mume wake kanijulia wapi mimi, au huwa wananizungumzia?

Na kwa nini ananitaka urafiki? Wakuu hii imekaaje, hakuna mtego hapa?
 
Inawezekana hajui pia kama uliwahi kuwa na uhusiano na wife wake .
Haya ma face Book unaweza jikuta umeungwanishwa mpaka na mama mkwe wa G/F wako wa kwanza
 
achana nae sio kila mtu anayekuomba urafiki facebook lazima umkubalie huyo nadhani anataka kufuatilia life lako kwa karibu mpotezee (tupa kule) ombi lake bora nusu shari kuliko shari kamili
 
mmh wanakuongelega wenzako ....iyo siyo coincdence iyo njimbi ina wvu sana so anataka kujua km mnaendele aau vp!!!!
usikubali km vp chat kwanza na mkewe km una cntact zake umwulze niaje mumeo kuntaka urafik?
wwanakutaja ao au mkewe alishawai kukutaja kat kat ya majamboz,au ndo zle swaga za yan bfrend wangu dula yan alikuwa anani...yan alikuwa ana..sasa yule jamaa ndo anataka wats da hell he is......b carfl
uskubali mwaya km demu wake asi ulishamwacha ktambo sasa nin?
 
Siyo lazima ukubali ombi lake na kwa vile umeshagundua kuwa mke wake ni rafiki wako wa zamani,achana naye asije akaleta roho ya uzinzi kati yako na mke wake,maana nijuavyo hamkawii kusema tukumbushane!
 
Nakushauri kitu kimoja delete facebook account yako moja kwa moja haina maana yoyote zaidi ya kuanika hadharani tu
 
mkuu be careful usisubutu kumruhusu kuingia angazako za facebook, pia ni bora ku-limit who and what types of friends and information you put on facebook.
 
hapo kuna namna tu si bure,labda alishamuona mke wake akipitia pitia picha zako mara kwa mara,anyway nahisi si bure bwana.
kuwa makini hapo.
 
Facebook? Ngoja nicheki na Kaizer wa kule yaani RR!

hapo kuna namna tu si bure,labda alishamuona mke wake akipitia pitia picha zako mara kwa mara,anyway nahisi si bure bwana.
kuwa makini hapo.

Hebu niambieni kwa nini nijiunge facebook kama mambo yenyewe ni haya? please convince me otherwise

Kama Asprin hapo akiingia kesho yake lazima wamfate nyumbani na taa na mienge.......RR siwezi kusema kabisa:hand:
 
Face book siyo nzuri! Block kuonyesha picha zako ila kwa mtu ambaye ni rafiki yako tu! hiii kitu mbaya sana
 
Hebu niambieni kwa nini nijiunge facebook kama mambo yenyewe ni haya? please convince me otherwise

Kama Asprin hapo akiingia kesho yake lazima wamfate nyumbani na taa na mienge.......RR siwezi kusema kabisa:hand:

hata hamna faida ya kujiunga huko,sioni faida zaidi ya watu kuuza sura tu huko na mashindano hasa kwa wanawake,vdume viko huko kujaribu bahati zao,na wengi wanabahatika,siku hizi kila kitu kimerahisishwa.
 
mmh wanakuongelega wenzako ....iyo siyo coincdence iyo njimbi ina wvu sana so anataka kujua km mnaendele aau vp!!!!
usikubali km vp chat kwanza na mkewe km una cntact zake umwulze niaje mumeo kuntaka urafik?
wwanakutaja ao au mkewe alishawai kukutaja kat kat ya majamboz,au ndo zle swaga za yan bfrend wangu dula yan alikuwa anani...yan alikuwa ana..sasa yule jamaa ndo anataka wats da hell he is......b carfl
uskubali mwaya km demu wake asi ulishamwacha ktambo sasa nin?

Kuna demu niliwahi kuwa naye halafu tukapotezana 5 years ago, sina hata contacts zake.

Ndio maana wanaosoma ni wengi mwisho wa siku wanaofaulu ni wachache ina maana hata kuibia kwenye JF huwezi bi rose? duh we kiboko
 
hata hamna faida ya kujiunga huko,sioni faida zaidi ya watu kuuza sura tu huko na mashindano hasa kwa wanawake,vdume viko huko kujaribu bahati zao,na wengi wanabahatika,siku hizi kila kitu kimerahisishwa.

basi mimi naendelea kuwa wa HAPA HAPA>...
 
inawezekana mkewe amemuelezea namna ulivyokua unamchakachua akapandwa na hasira kaa naye mbali otherwise watakula kiboga
 
Ndio maana wanaosoma ni wengi mwisho wa siku wanaofaulu ni wachache ina maana hata kuibia kwenye JF huwezi bi rose? duh we kiboko
we sokomoko vp bwana?kwa nini niibie?kwan wewe unaibika?
we haujatafutwa na mwenye mali ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom