Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
Pole sana dada, Jitahidi sana kumwomba Mungu atakuongoza kuamua jambo la hekima kwako na kwa familia yako.
haya mambo huwa yananiumiza sana kichwa, wamama wengi sana wanapolalamika kuhusu kugundua waume wao kuwa na watoto wa nje huwa tunawashauri wavumilie na kuwapenda hao watoto wa nje, kisa watoto hawana makosa. Ni kweli watoto hawana makosa, lakini tujaribu kujiweka kwenye nafasi za hao wamama, ni kweli tungeweza kuwalea kwa upendo hao watoto wa nje kisa hawana makosa?
Kwa mtoto ambaye umemkuta kabla hujaolewa naweza kufikiria, lakini huyu ambaye kazaliwa tukiwa tumeoana, tena mdogo kuliko watoto wangu! hili huwa nakataa kuliwaza. hii inaonyesha dhahili kuwa huyu baba hajipendi hata mwenyewe, pamoja na kumpa mimba mtu huko nje anaweza akapata na magonjwa mengine pia. kama kweli umemtamani mtu huko nje kwa nini ujiachie kiasi kwa kusababisha mimba?