MUME: Mke wangu kaniibia Nyeti

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu vya habari zimedai kwamba Ali kwa sasa hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kuwa nyeti yake imetoweka kimiujiza na shutuma zote anambebesha mkewe kwamba ndiye aliyefanya ‘mchezo' huo.

Habari zinadai kuwa kutokana na hilo, kumezuka mgogoro mkubwa kati ya wanandoa hao kwani mume amekuwa akimdai mkewe arejeshe nyeti yake, jambo ambalo halijawezekana.

Imedaiwa kuwa Hadija, mara baada ya kufunga ndoa na Ali mwaka 1996 alikuwa na wivu wa kupindukia, hivyo kuamua kutafuta dawa na kumfanyia mumewe ili ndoa yao izidi kuimarika lakini mara baada ya kutenda alichoambiwa afanye kama dawa, nyeti ilitoweka na kubaki na ‘kipande' kidogo cha kusaidia kutoa haja ndogo.

"Kutokana na madai ya Ali, mkewe aliamua kufungasha virago na kutoweka nyumbani na kwenda kusikojulikana wakati mumewe yupo kazini," kilisema chanzo.

Gazeti hili baada ya kusikia habari hizo za kushangaza, lilimtafuta Ali ambaye baada ya kuulizwa kuhusu mkasa huo alititirisha maneno kama ifuatavyo:

"Ni kweli hayo uliyoambiwa. Kwa sasa ninachomdai mke wangu aliyetoweka ni nyeti yangu, naomba anirudishie kwani ufumbuzi wa mgogoro wetu hauwezi kupatikana kamwe kama hatazirudisha.

"Hapa unaponiona ndugu mwandishi mimi siyo mwanaume tena. Sina ‘kitu', hapa kimebaki ' kipande' kama kalamu ambayo haifanyi kazi yoyote. Mke wangu nilipomuoa alinikuta nina watoto sita niliozaa na mke niliyemuacha mwaka 1994, sasa hivi siwezi kufanya tendo la ndoa.

"Mgogoro wa kutoweka na nyeti yangu ulianzia mke wangu alipoanza kunilalamikia kuwa natembea nje ya ndoa na akaniahidi kuwa ni lazima atanidhibiti. Madai yake niliyapinga lakini nguo zangu za ndani zikaanza kupotea. Nilipomuuliza alisema angeninunulia nyingine, nilikuwa na mashaka naye, nikamuomba anirudishie lakini hakufanya hivyo.

"Mara tu chupi zangu zilipoanza kupotea, nikawa sisikii hamu ya tendo la ndoa. Mwezi uliopita, nyeti yangu ikawa imetoweka, nilipomuuliza akawa mbogo. Ilipofika Julai 28, mwaka huu, saa sita mchana, nilitoka kazini na kurudi nyumbani lakini sikumkuta mke wangu na nguo zangu za ndani na soksi hazikuwepo pia.

"Licha ya nguo, picha zangu nazo alizichukua na nilipomuuliza mtoto wangu Karim akasema mama yao amesema kabeba vitu vyake vyote ndani ya nyumba na hakumuambia anakokwenda.
 
Duh,bongo ni zaidi ya tuijuavyo,mi ndio maana bado niponipo kwanza.
 
Hizo ni bluetooth za kiafrika yaani sayansi mwitu. Pole kaka ila nakushauri kwa kuwa una watoto baki hivyo hivyo kwa kuwa utajiepusha na uasherati na maradhi.
 
Hizo ni bluetooth za kiafrika yaani sayansi mwitu. Pole kaka ila nakushauri kwa kuwa una watoto baki hivyo hivyo kwa kuwa utajiepusha na uasherati na maradhi.

alie kunyima kunde amekupunguzia .******......mshululu 2 mkeo bola mcho unayo basi wee waachie wenye meno walebaki na hako KAMBILMBI furahia maisha kama kawa pole na wana SAYANS wa Kibongo
 
Ila nimekuja kutafakari nakusikitikia sana na mtafute shogake mkeo umhonge akupeleke kwa mganga aliyefanya hayo. Duu pole sana.
 
Msaada upo hapa jf kama bado anazitaka. Zitarudi na manguvu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom