Mume anaweza kumfanya mkewe kuwa zuzu!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Ni wazi unawajua wanawake ambao wanaishi katika ndoa ngumu za manyanyaso hadi unafikia kuuliza, ‘hivi huyo mwanaume amempa kitu gani kikubwa hivyo?' Wanawake hawa nao wanakuwa wamefikia mahali ambapo wanaamini kuwa wanatakiwa kuishi hivyo, kwenye uhusiano wa ain hiyo.

Ni kitu gani kinatokea hadi mwanamke kuamini kwamba yeye ameandikiwa kuishi kwenye ndoa ya shida na karaha na mwingine kuamini kwamba hivyo ndivyo ndoa zinavyotakiwa kuwa? Malezi na mazingira ni moja ya sababu kuu, lakini usugu ni sababu nyingine.

Ninaposema usugu nina maana kwamba mwanaume anatokea kumdhalilisha mwanamke na mwanamke huyo kuvumilia hadi anajikuta amefikia kuamini kwamba hiyo ndio ndoa, hivyo ndivyo anavyostahili kuishi.

Mwanmke anapovumilia mateso ya ndoa kwa muda mrefu sana bila kujua ni kwa nini au kwa matarajio kwamba mmewe atabadilika, hufikia mahali ambapo kujiamini kwa mwanamke huyo huisha na hujishusha kithamani na kuwa chini kabisa.

Hebu jaribu kuwachunguza wanawake wote ambao wameteswa na kudhalilishwa kwa muda mrefu na waume zao, unaweza kuona dalili fulani za uzuzu. Uzuzu huu unatokana na mwanamke huyo kujishusha thamani kwa kuamini kwamba yeye ni dhalili na si lolote.

Kumbuka kuwa hapa sizungmzii hali ambayo tunaiita utegemezi, hali ambayo humfanya mwanaume au mwanamke kuona kwamba hawezi kuishi bila kuwa na mwanamke au mwanaume aliye naye.

Hapa nazungumzia ile hali ambapo hakuna utegemezi, bali mwanamke amekuwa akijiambia kwamba mumewe atabadilika tu, bila jambo hilo kutokea.

Kwa kuwa amevumilia kwa miaka kadhaa, hufikia mahali udhalilishaji huo wa mwanaume ukamfanya mwanamke huyo kujishusha mwenyewe kithamani kwa kutojiamini na kudhani kwa yeye ni mtu duni.

Hutokea vipi mwanamke akawa zuzukufuatia kunyanyaswa au kudhalilishwa sana na mumewe? Kinachotokea ni kwamba zile kauli na vitendo ambavyo anafanyiwa na mumewe mara kwa mara kama sio kila siku, hatimaye hujijenga ndani mwake na kumpa haiba mpya.

Haiba hii inakuwa ni ile ya kutojiamini, kuogopa na kudhani yeye ni mtu duni, kwa sababu kauli na vitendo vya mumewe dhidi yake vimejikita sana akilini mwake kiasi kwamba ameviamini.

Ni vizuri kwa wanawake kuangalia tabia za wanaume ambazo kama wataamua kuzivumilia kwa muda mrefu sana watajikuta wamekuwa mazuzu,wamekuwa ni watu wasiojiamini, woga na wanaodhani wao ni duni.

Tabia hizi zina athari kubwa za kisaikolojia kwa wanawake kutokana na ukweli kwamba ni zenye uwezo mkubwa wa kutweza na kushusha hadhi ya anayeambaiwa au anayetendewa.

Kuna wanaume ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi, wivu ambao hauna sababu za msingi. Kutokana na wivu huo wanakuwa ni watu ambao wanajaribu sana kuwadhibiti wake zao kiasi kwamba wake hao wanakuwa kama watoto wadogo kwao, wanakuwa kama mali ambayo inahitaji kulindwa ili isiibwe au kupotea.

Hapa unaweza kukuta hata mwanaume hufikia hatua ya kumkagua mkewe (watu wazima wanaelewa nazungumzia ukaguzi upi) kila anaporudi nyumbani baada ya kutoka nje kidogo hata kwa dakika kumi tu.

Kama unajikuta unaishi na mwanaume mwenye tabia za unyanyasaji kama huo nilioutaja hapo juu, inabidi uanze kukagua upya uhusiano wenu. Ni muhimu kuukagua upya kwa sababu kama hilo litashindikana kuna uwezekano wa kuja kujikuta umezoea maisha ya namna hiyo ambapo matokeo yake ni wewe kuwa zuzu.

 
Eeh,maelezo marefu!bt 2mekuelewa mkubwa.but fest kno maana ya uzuzu na uvumiliv
 
kwa hiyo wawaache hao waume au? kwa kweli unyanyasaji ni mbaya sana na mwanamke anatakiwa kuonyesha msomamo wake mapema kupinga unyanyasaji, sio uvumilie muda mrefu ndio uanze kumwambia ukweli mumeo atakwambia kuna watu wamekushika masikio
 
Back
Top Bottom