Kuna dada tunafanya nae kazi huku nje ya Tanzania, kaolewa mumewe yupo Dar ndoa yako ina miaka mitano, toka tumekuja huku jamaa anagombana na mkewe kila kukicha tangu mwezi wa 5 tuko huku huyu dada hana raha kabisa mumewe kila akipiga simu akisikia tu sauti hata ya gari ataanza kuuliza hapo uko wapi hujafika nyumbani na amesahau kuwa huku tunatumia usafiri wa public. Mbaya zaidi amemkasirikia toka ijumaa hajaongea na yeye huyu dada hata kazi inamshinda analia tu kila mara. Amefikia kusema kuwa anataka kurudi maana hali imefika pabaya. Na mkataba tulipewa three years? Je? Aache kazi arudi Dar ama afanyeje mie nimeshindwa kumshauri maana ukiongea nae tu analia nikaona niilete hapa tumshauri. Tafadhali nisaidieni najua humu nitapata jibu
whattttt!!!!!!! yaani kweli katika halil hii ya maisha magumu watu wanatafuta kujikomboa kiuchumi eti mke aache kazi kisa mume???? we unadhani mume angekua ameenda huko nje angekumbuka hata kupiga cm sikwambii kuacha kazi kuja kumkumbatia mkewe, hivi hamjui ukiwa na mawazo ya kukosa pesa hata mapenzi hayafanyiki??? na usikute huyo mwanamume alioa mke 'ready made' kasomeshwa na wazazi halafu eti kwa ajili ya 'kukaa' na mume aache kazi! mmh ckujua kama dunia ya leo bado watu wanawaza kama enzi ya 2 ya mawe!!!!!!!!!!!!:disapointed: ooh Lord have mercy!!!!!!!!!That explains everything... Mwanaume anajisikia inferior... na hilo tatizo ni kubwa sana, sijui atasaidiwaje... ila kwa ufupi ni kwamba, dada aache kazi arudi TZ akae na mume wake...
Hivi mwanaume harusiwi kuwa na wivu au si kawaida mwanaume kuwa na wivu?