"Mume amefariki leo, Mke anaolewa kesho"...!!!

Kuna mke wa jamaangu mmoja ambaye aliamwambia mumewe baada ya kutoelewana ndani..."Nimechoka, naenda kwa Mamaangu!"
Familia hiyo ilikuwa na Watoto 7.
Basi mumewe akamjibu..."Ni sawa tu, nenda kwa mama yako, Ila sasa hivi na mimi nimeamua kurudi kwa Mama yangu mzazi, lakini ili mambo yaende sawasawa, na hawa watoto wetu saba wote waende kwa mama yao!
Mke yule kusikia hivyo akamwambia mumewe ..."Yaani Una maana watoto waje kwangu sio!"...Basi nimebadilisha mawazo siendi popote!
Familia zetu hizi ziko flagile sana, hakuna upendo.

Alikosea alitakiwa kusema anaenda kwa baba yake! ili watoto wabaki na mume!! kazi kweli kweli
 
namkumbuka james dandu alikufa hapa kwa ajali mkewe baada ya wiki mbili akambeba muuza sura mmoja kumpeleka ulaya walikokua wanaishi na mumewe dandu,hiyo inatokea lakini nadhani baada ya mkeo kukuchoka sana
 
Mkuu masuala ya ndo usipoenda nayo vyema na yakiwa yamekaa kushoto visa kama hivi hukosi
Watu wanaombeana wafe ili apate uhuru
Je kwenye kumuombea huko yeye Mungu akawa amepanga vingine kuwa mwanamke atangulie
Suluhisho sio kuombeana kifo ila ni kutafuta muafaka wa haya mambo na masuala ya ndoa mengi kukubali kujishusha na kutafuta kiini cha tatizo ndiko kwema
Bila hivyo muafaka hautokaa upatikane
 
Tatizo ni kuwa watu huharakisha sana suala la ndoa......unakutana na mtu hata hujamjua vizuri unatatfuta wazazi wake uoe......unapokuja kumjua vizuri too late......ndio haya ya kuombeana vifo
hilo unalosema kweli lipo lakini kuna wengine tumekaa nao miaka kumi then ndio tukafunga ndoa lakini bado mbeleni mnabadilika sana na hivi sheria ni pasu kwa pasu ndio maana mnaringa siku ikitokea tumetengana sioi tena nageuka snake tu.......
 
Kwa wasio ktk ndoa ni ngumu sana kuelewa na kuamini hilo.Mimi sijashtuka wala kushangaa maana ndoa na mahusiano mengi ya siku hz mkiwa wachache sana kwenye cycle basi mko 8 chini ya hapo hakuna.Ndoa nyingi zinaishi kwa mazoea tu na kusogeza siku mbele, bt nyingi ZILISHAVUNJIKA muda mrefu sana.
 
kinachompata huyu dada hadi kutamani mme wake afe ni kitendo cha mume wake kumfanya ajisikie hana thamani yoyote katika hii dunia ni heri afe kwa hiyo yeye nae anajisikia vibaya anamuombea kifo ili aone kama kwenye hii dunia yupo atakayeona thaman yake au la?na iwapo atakutana na mwanaume kama mume wake basi ataishia kujiua.
 
Kwa maelezo ya huyu shostito ni kwamba yeye ndiye anatunza familia, nadhani wana mtoto/watoto, anayo kazi nzuri inayomuingizia kipato cha kutosha(ofcourse alitaja mahali anapofanya kazi, ni kampuni kubwa hapa nchini).
Kinachomtatiza ni kwamba mume haonekani kumjali kabisa, haonyeshi mapenzi yoyote kwake, anahisi kama ana mwanamke mwingine.

Sasa kwa nini asijiondokee hata leo ili aachane na manyanyaso?? Btw, kufanya kazi kwenye mshahara mnono sio guarantee kuwa hakuna wawezeshaji wa nje wanaompa kiburi hata kutamka maneno kama hayo!!
 
Mkuu huyu mwanamke alikuwa hazungumzii kurithiwa, alikuwa anamaanisha kwamba ataolewa na mwanaume mwingine anayempenda.

Utakumbuka alikuwa anamwambia mwenzake kwamba, tafadhali msije kuniuliza huyu mchumba nilimpata lini na wapi!!

Kwahiyo tayari mume mpya keshapatikana, kinachosubiriwa ni kifo cha mume wa sasa.

Dady bana!! mie nilijua kuwa upo kwenye sihasa tu.Kumbe hata kwenye viti virefu unaenda?Anyway Usihofu mummy hayupo kama hao uliowasikia kwenye viti virefu.I am praying for you dady.
 
Back
Top Bottom