Mukoba: Mgomo wa walimu ni halali na umeanza leo hii!

Hivi wale Madaktari wa Iran wako wapi? halafu ifike wakati sasa jeshi liseme sasa tunataka kuongoza na nchi na siyo kuwaita tu Serikali ikiwa imebanwa vilivyo.
 
walimu kwa haya maisha hadi lini?mshahara wenyewe ukitoka hata katikati ya mwezi huwa haufiki kinachofuata ni kukopa tu,walimu tunanuka madeni,leo tufanye kweli.
 
kwa sababu mwanafunzi hafi mwalimu akigoma,
serikali ya CCM itaenda mahakmani,
kisha wote tutaambiwa ni,
marufuku kutaja suala hilo.
 
Sasa hivi Mukoba yuko ITV anazungumzia kuhusu mgomo wa walimu na anasema ni halali. Mwl. atakayeenda kazini in msaliti kama wasaliti wengine waliowahi kutokea katka mapambano ya ukombozi

Huyu Mukoba ni msaliti namba moja wa walimu, na lazima yupo kwenye payroll ya ikulu mambo ya kugeresha watu wazima eti kuna mgomo wakati hakuna pande yoyote itakayoathirika ni unafiki.

Kwa taarifa shule nyingi za serikali zimeshafanya mitihani zikisubiri kufungwa ijumaa ya wiki hii kwahiyo walimu wengi wapo kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo kazi ambayo wanafanyia nyumbani, pia wanafunzi wanakwenda kucheza na kufaya kazi za usafi tu kwa hiyo kugoma huku ni sawa na kuwaambia walimu wakae nyumbani waendelee na zoezi la kusahihisha mitihani.

Kwanini Mukoba asiitishe mgomo siku ya kufanya mtihani wa darasa la saba au siku za mitihani ya form four ile ya taifa?
 
Nimelazimika kutembelea shule mbalimbali za msingi hasa za vijijini zilizoko mkoani mbeya baada ya kusikia kerere za wanafunzi zikitokea madarasani.nilipofika kwenye madarasa hayo ni mekuta kuna wanafunzi tu.na baadhi ya shule kuna walimu wakuu wanafundisha kwenye darasa moja moja huku walimu wengine wakiwa wanarandaranda mitaani na wengine wamebakia nyumbani mwao.hali nilioiona ni kwamba mgomo huu unaweza kuwa na athari kubwa kwa serekali hasa baada ya kuitikiwa na walimu wa shule za vijijini ambao kwa kawaida huwa si wepesi wa kuitikia migomo kabla ya kusomo upepo unavyo kwenda kwa kutegemea wenzao wanao fundisha shule za mijini.
 
Mgomo wetu ni zaidi ya halali serikali imeonesha dharau ya hali ya juu dhidi ya walimu japo kutekeleza madai yetu japo moja
Hivyo walimu hatuna budi kushikamna na kuwaonesha who are TEACHERS
WENZETU KENYA WANALIPWA MARA TATU ZAIDI YETU NA WAMEGOMA WANATAKA WAONGEZEWE 300% NA KUNA MAKUBALIANO WAMEFIKIA .IWEJE SISI WALIMU WA KITANZANIA TUSIWEZE KUSIKILIZWA?
HAPA KAMA NOMA NA IWE l
LIWALO NA LIWE
 
hata mahakama waje na kanusho hatuendi job aisee! tumechoka sana tena awaambie kabisaa kwamba na wanafunzi watatujaion soon ndipo watakapoona kwamba cwt yawweza kuwa chama cha uinzani chenye nguvu kuliko chama chocote kile.

wanafunzi wakiwajoin nasi wazazi hatuna budi kuleta balaa.
Tuone nani atamtoa kucha mwenzie
 
wasiwasi wangu ni kuwa walimu watagomaje wakati mishahara bado?wataweza kweli kukomaa wakati hali tete?Ushauri wangu, wangesubiri waingiziwe chao then wapate hiyo nguvu ya kugoma....
 
Kama kweli uongoz wa bunge unawajali watanzania maskini ambao watoto wao wanasoma shule za serikali ni lazima kuwe na hoja ya dharura kukijadili hili swala kwn wanafunz wengi wanarud nyumban kutokana na mgomo kwa mkoa wa kilimanjaro mgomo upo kwa baadh ya shule hasa za mjini bunge iokoe hili kwan walimu wana madai ya msingi waache itikad ya vyama lijadiliwe
 
Mimi nilitegemea kupata update....

Kwani wamegoma kweli au wameogopa mkwara wa kitoto uliochimbwa na Ikulu....

Kwa watu ambao hawakupikwa kwenye tanuru la freedom square,...nina hakika huo mkwara utakuwa umetosha kuwafanya waendelee kulamba unga wa chaki.......

Sitaki kuwa Tomaso ila nadhani hawana guts za kuwakaribia Ma-Dr!!
Mkuu hiyo mikwara siku hizi tushaizoea kwa taarifa yako ni WAKUU WA SHULE TU ndio wapo shuleni
WE ARE TEACHING THE LESSON GUYS LIKE YOU
FOR THIS GENERATION OF TRANSPARENCY NO FEAR CAN BE EXPERIENCED BY INTELLECTUALS WE ARE READY FOR EVERY THING.
LIWALO NA LIWE
 
Tutachukua walimu toka jeshini ili waweze ku cover,na irani wametuahidi walimu elfu tatu,pesa imetengwa bil.21,afu kama vipi LIWALO NA LIWE!
 
Wadu naombeni kuelewa kuhusu mgumu wa walimu tanzania ni haki yao kugoma au sio? Kwa mtazamo wangu naona ni haki yao na pia waendelee kugoma tena ikibidi tuwaunge mkono wapate masilahi yao kwa manufaa ya elimu bora kwa vizazi vijavyo.
 
Tanzania,

Ikiwa siku za Bunge la Bajeti zinazidi kuyoyoma na mambo yasiyotarajiwa yanasikika Bungeni na jipya la Mgomo wa Waalimu kuanza leo.... ukiwa kama Mtanzania usiache kusikiliza Bunge ili uwe na Mtazamo na ujiulize Tanzania tunaposema neno "MZALENDO" tuna maana gani.

Sikiliza Arusha Mambo Internet Radio; LIKE na kutuma maoni yako kwa info@arushamambo.com mara baada ya redio kufunguka; bonyeza hapa:

http://tunein.com/tuner/?StationId=158711&
 
tatizo walimu wakidanganywa kidogo tu wanakubali wanarudi kazini halaf wanaanza tena kulalamika.....au wakiahidiwa kazi za kuhesabu watu kwenye sensa
 
mbona mnagoma wakati mitihani imeshafanywa? Na soon shule zitafungwa? Usanii gani huu? mgomo gani huu hauna timing?
 
Back
Top Bottom