Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

Amekosea nn sasa kusema ukweli ? hakuna kitu hapo kwenye thread yako aiseee

Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''

Huelewi nini au ndye paymaster wako? Ndiyo maana uelewa wenu ni sawa na urefu wa pua
 
  • Thanks
Reactions: FJM
ni aibu sana kwa mzee kama yule kuchafua hali ya hewa kiasi kile.....
 
Mi nadhani Kauli yake ndio imemuumbua kuwa kumbe CDM haina ukabili muda mrefu... look here Mkani ndio alikuwa Katibu mkuu wa kwanza wa CHADEMA, ambaye ni MSUKUMA, akawa mwenyekiti MSUKUMA sasa hapo inakuwaje kuitwa ni chama cha kikabila?


Na ongeza Mwislamu akawa katibu mkuu na mwenyekiti
 
Kanifurahisha Mh. Mbowe kwa kuweka historia ya Chama vizuri tena kwa lugha nyepesi lakini yenye uzito na msisitizo wa hali ya juu. Aibu kwako Mukama. Maana ulianza kwa mbwembwe kweli (utafikiri hauko msibani!) kuonyesha Chadema imejaa ukanda. Kuna mtu mmoja pale kasema kuna vitu vingi visipoandikwa kwenye vitabu unakuta historia inatoweka. Nadhani hata hili Nape amekuwa akilipigia vuvuzela kweli ila leo amenywea....
 
Huyu jamaa alitakiwa awe nyumbani kwake analisha ng'ombe! sijui kwa nini walimteua kuwa katibu mkuu! jamaa hafai hata ukatibu kata!! Vapour zote za CCM kumbe yeye ndiyo huwa anamtuma katibu wa itikadi na uenezi.

Sasa pale ccm wewe umeona ni nani anafaa? walidhani kumtoa mzee Makamba ndio dawa kumbe hakuna wa kumsaidia mwingine wote mabogus tu!! Eti chama kikongwe kuliko vyote Tanzania, Shame on them all!!
 
Huyu jamaa alitakiwa awe nyumbani kwake analisha ng'ombe! sijui kwa nini walimteua kuwa katibu mkuu! jamaa hafai hata ukatibu kata!! Vapour zote za CCM kumbe yeye ndiyo huwa anamtuma katibu wa itikadi na uenezi.

...hafai hata kuchunga Ng'ombe,huyo ni Mvua Samaki - anavua chochote hata nguo anaweza vua tu. Wachunga Ng'ombe wanajua suruba za maisha - cheki Edward Sokoine (Edward Lowasa - Hajachunga Ng'ombe),Julius Nyerere, Chacha Wangwe,etc,
 
Kweli nime amini zile ndevu zake zimetanda hadi kwenye ubongo wake ndio maana akayasema yale.
Acha nisiongeze maana nitapata ban,sijawai kuona kichaa kama huyu, saa nyingine hata vichaa hutulia lakini huyu sielewi.

Hivi kwanini hakuomba nafasi pale cdm square?Kweli siasa za udini na ukabila zimeletwa na nyinyiemu! Sasa naanza kuamini tuhuma za uamsho kwa nyinyiemu.
 
Hivi Katibu mkuu wa CCM anachaguliwa au anapachikwa tu? Maana Mkama Dah! huyu siyo kabisa, afadhali ya Makamba!
 
Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.

Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.

Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.

ccm wamepagawa, wamekosa mvuto kwa wananchi na sasa popote wakiona kusanyiko la watu wanadhani ni kongamano la kisiasa, sasa kwenye hadhara ya msiba wanaleta porojo na utumbo wao wa kisiasa kama si kufilisika kwa maadili na busara tuite nini? wallahi ningekuwepo hapo msibani ningempiga huyo 'hamnazo' mukama kidole cha nnya kwa 'bahati mbaya' lakini!
 
ukweli utabaki ukweli.kaskazini ni ukanda wenye wapambanaji.je,sokoine angekuwa Cdm mgemwita mkanda?
 
Mkama ni sampuli tu ya viongozi waliosheheni ndani ya CCM. Wanaweweseka na kuhangaika mithili ya panya waliolishwa sumu katika unga na kutenda vitendo vya ajabu kabisa mbele ya kadamnasi! Ni sumu ya ufisadi waliyovimbiwa, matumbo kuwavimba wakichafua hewa kila wanapopita. Hautapita muda mrefu kabla hawajaangamia wote. 2015 ndiyo kiama yao.
 
Back
Top Bottom