salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 418
- 136
Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.
Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.
Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.
Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.