Mukama(CCM) akunwa na Gazeti la Mwananchi

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wednesday, 04 April 2012 21:50
0digg
Boniface Meena
KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama amelisifia Gazeti la Mwananchi akisema linaandika habari bora na kuchuja ukweli na uongo.

Mukama alitoa sifa hizo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine alizungumzia tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kuhusu Mradi wa Machinjio wa Jiji la Dar es Salaam na uchaguzi wa ubunge Arumeru Mashariki uliofanyika Jumapili iliyopita.

Alisema Gazeti la Mwananchi linafanya uandishi bora unaofuata weledi kwa kutenganisha uongo na ukweli…
“Linafanya utafiti na kuandika habari bora kabisa.”

Akizungumzia mradi huo wa machinjio, Mukama alizilalamikia baadhi ya Kamati za Bunge kwa kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mambo yanayojadiliwa ndani ya kamati akieleza kuwa ni kinyume cha kanuni na taratibu za Bunge.

“Mimi nilitoka jiji tukiwa tumekamilisha kila kitu kuhusu mradi wa machinjio na kampuni ya kuendesha mradi huo ilikuwa imeshapatikana na ulikuwa ni mradi bora na ambao ungekuwa na mafanikio,” alisema Mukama na kuongeza;

“Lakini tatizo ni kwamba wakurugenzi wa Dar es Salaam waliamua kufunga mradi huo wakati mimi nikiwa tayari nimeshaondoka jiji. Sijui kwa nini wamefanya hivyo huku wakijua Dar es Salaam inahitaji machinjio ya kisasa na nashangaa kwa nini hawakuendeleza mradi ule.”

Kuhusu Kamati za Bunge kutoa taarifa kwa waandishi wa habari zikiwamo hizo za kwake kuhusika katika mradi wa machinjio, Mukama alisema: “Hii Kamati ya LAAC (Serikali za Mitaa), ya Augustine Mrema inafanya kazi ‘in camera’ (ndani) na ikimaliza kazi zake inazikabidhi Bunge, sasa inashangaza inawazungumzia watu kabla ya kufanya uchunguzi.”

“Hizi kamati zimegeuka kuwa ‘quasi judicial’ (mahakama za pembeni) bila kufanya uchunguzi wa kina na bila kujiuliza nini wanachozungumza. Hizi kamati zimekuwa zikituhukumu bila kutoa nafasi ya kutusikiliza tunaohukumiwa. Mimi niko safi si kila mtu ndani ya chama hiki ni Richmond,” alisema Mukama.

Wadau
hebu someni ktk Nyekundu hapo,mukama kumbe anaelewa kuwa ndani ya chama kuna wana Richmond?
 
Mwandishi wa Mwananchi nakushauri. Usihadaike na 'simple popularity' kutoka kwa Mukama. Waswahili husema kuwa maneno matamu yalimtoa nyoka pangoni. Mukama alihisi kuwa mwandishi atamkaba koo kwa kumuuliza maswali ya kumuumbua ndipo akaamua kucheza naye kisaikolojia tu. Simple as that! Kwani Mukama ni professional kiasi cha kujua chombo kipi cha habari ni kizuri na kipi hapana. Mbona hatujamsikia akivizungumzia vyomba kama Aljaazera, MwanaHalisi, Raia Mwema, Citizen.......Acheni kuhadaika na sifa chapwa kihivyo!!!!
 
Back
Top Bottom