Mukama aviabisha vyombo vya Usalama: Adai CDM imeingiza mamluki toka ng'ambo

8][/COLOR]Mukama lazima awe anavuta bangi, hii siyo kauli ya mtu anayetumia akili kufikiri.Natoa ushauri kwa JKhuyu Katibu Mkuu wake akapimwe akili isije kuwa lile bichwa limejaa nta ya moshi wa bangi badala ya ubongo.
mkuu hapo kwenye red wanatofautiana nini hao??ndio walewale tu pipa na mfuniko
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili tbc, mkama analalama na kwamba CDM wameingiza mamluki waliopata mafunzo na taarifa na majina wanayo.

Je kuna haja gani kuita waandishi badala ya kupenyeza taarifa hizo police, haingii akilini maneno ya kitoto kama haya kuaminiwa.

Jibu la Dr Slaa makini kabisa, kama taarifa zina ukweli ni aibu kwa serikari legelege iliyoko madarakani ya ccm.

Hadi hapo nimejiridhisha kwamba mzee Mukama ni hopless hata kuliko mzee Makamba.

Kwa mtu msomi wa shahada mbili kama Mukama kuwa na propaganda za hovyo kiasi hiki, inaonyesha uwezo wake binafsi kiuongozi ni mdogo sana kuliko hata mtangulizi wake ambaye tulidhani kwamba huenda kwakuwa ana shule ndogo ndio maana anabwabwaja sana, kumbe sivyo.

Katika akili ya kawaida kabisa, chama hicho mnachokituhumu kuwa cha kikristo ghafla kimekuwa na link na al qaeda na kuingiza mamluki toka afghanistana na pakistani, hivi hizo nchi ni za kikristo? hovyo kabisa mzee mukama.
 
Nimeona CCM wakiwashambulia sana wana Usalama.

Pinda juzi kasema wanafanya magendo hivyo atatumia jeshi la wananchi, hapo kawatukana polisi si bora angekutana na wahusika wakaongea.

Mukama naye kawatukana jeshi la wananchi na polisi kuwa hawafanyi lolote wanachapa usingizi huku Chadema wakiingiza makomandoo toka nje.

Hapa pazuri sana, mimi huwa nawaambia watu kuwa siku ya kifo cha nyani miti huteleza na bado mtasikia mengi. Hayo yote yanatokea wakati wanausalama wapo kuwasaidia wao hao hao Igunga. hahahaha inachekesha
 
Akili za kuambiwa changanya na za kwako...Mukama kama mwenyekiti wake wa chama tu wote Mbayuwayu
 
Huyu mjita ni kutumia masaburi kufikiri au kachanganyikiwa kuona mahela yore waliyomwaga yataenda kwa wahuni wenye sera ya kula magamba na kulala magwanda. Wajita wenzake hebu muelimisheni huyu mjinga. Interahamwe na mungiki hawajawakamata na Leo wanaleta makomandoo, how come?

sijui nibadilishe jina manake hili li-mukama sijui kwao wapi na limekulia mazungira gani.nooooo huyu nahisi ni mjita photo copy
 
mIMI NINAWASIWASI NA sELIKALI HII,, MIMI NILISEMA MAPEEEMAAAA WALIPO KUWA WANASEMA ETI KUJIVUA GAMBA, MAGAMBA MAKUBWA YAMEBAKI NA SASA YANAANZA KUTEMA CHEHE,, SASA MUKAMA ALICHOKISEMA NI AIBU KWA SELIKALI, KW VYOMBO VYA USALAMA, NA KWA CHAMA CHAKE,,, NA KAMA ANAUSHAHIDI ASEME WALIPITAJE HAO 30 BILA KUONEKANA, NA WAMEFIKIA WAPI BILA KUJULIKANA, NA WAMEKUJA KUFANYA NINI,, HAO MAKOMANDOO WANATIJA GANI KWA CHADEMA
NAWASIWASI SANA NA HAYA MAGAMBA MAANA NAHISI KUNA BOMU LINAKUJA ILI WAWASINGIZIE CDM, NAOMBA WATANZANIA TUWE MAKINI SANA NA HAYA MAGAMBA MAKUBWA YALIYO BAKI
 
Huyu mzee maneno aliyosema jana unaweza kudhani hajawahi kuwa mtumishi wa ngazi ya katibu mkuu wa wizara serikalini. Anasema hao makomandoo wamepata mafunzo Libya miaka ya 1990, Palestina miaka ya 2001 na Afghanistan. Libya na Palestina wote wana balozi zao hapa nchini,sijui kama tuna mahusiano yoyote na Afghanistan,kwa hiyo ameingiza nchi yetu ktk mgogoro wa kidiplomasia.
 
Tanzania na watanzania tunapotakiwa kukaa chini na kujadili mustakabali wa Taifa letu. Sioni hoja ya msingi toka kwa Mukama. Embu tufungue macho na tuone na masikio na tusikie. je ccm sio chama cha mke na mume, baba na mtoto, shangazi na mjomba? au hayaoni haya ndani ya ccm? embu shindeni igunga kwa kuwajibu watanzania kwanini gharama ya maisha inapanda kila kukicha?
 
Mukama karopoka na badala ya kupotosha kapotoka mwenyewe kwa kuiumbua serikali ya chama chake kwa ufinyu wa fikira zake na uupuzi wa mawazo yake. Mengi yamesemwa na wachangiaji makini, maswali yanabaki kwa Mukama na chama chake. Je hao makomandoo walienda kuifunza kwa ufadhili na ruhusa ya nani? Na kama serikali ilitambua imetambua tunataka ituambie kama kupata mafunzo ya kijeshi nje ya nchi ni kinyume cha sheria. Na pia kama kweli hao makomandoo ambao yeye amekwenda mbali na kuwaita magaidi walifundisha katika nchi hizo alizozitaja tunataka waziri wa mambo ya ndani atuambie kama hayo mafunzo yalikuwa rasmi na kama sio rasmi basi atoe tamko la karipio ikiwa ni kusitisha uhusiano wa kibalozi na nchi husika kwa kufundisha raia wetu 'ugaidi' Alafu cha kuchekesha kuliko vyote anadai hao 'magaidi' wa chadema walipata mafunzo mwaka 1990, sina uhakika kama mwaka huo kulikuwa na chama kinaitwa chadema nchi hii. Hili suala sio la kubeza hata kidogo na halitakiwi kuishia tu kwenye majukwaa ya siasa. AMA KWELI MBWA MZEE HAWEZI KUFIFUNZA MBINU MPYA. Mzee Mukama wakati ni ukuta huwezi kupigana nao
 
Huyu mjita ni kutumia masaburi kufikiri au kachanganyikiwa kuona mahela yore waliyomwaga yataenda kwa wahuni wenye sera ya kula magamba na kulala magwanda. Wajita wenzake hebu muelimisheni huyu mjinga. Interahamwe na mungiki hawajawakamata na Leo wanaleta makomandoo, how come?

Huu ni ujinga. Mkama kaongea kama kiongozi na mwakilishi wa CCM na siyo kama mwakilishi wa kabila la wajita. Sioni hili suala la wajita wenzake kumuelimisha linatoka wapi. Haya ni mawazo ya kikabila ambayo hayana nafasi kwenye jamii iliyoendelea na sikutarajia yaongelewe na mtu anayejiita great thinker. Pu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,fu.
 
Du! Wakubwa hili ni zito,ninapata picha kuwa mambo nimagumu kwa ccm. Ninajiuliza maswali mengi, inawezekana haya? Kama ndio vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nini? Kama hapana uzushi huu ni hatari kubwa na sibure kuna kitu umekusudiwa. Kwa uzoefu, mara nyingi ukiona chama kilichoko madarakani (watawala) wanalaumu/tuhumu mambo ambayo kwa nafasi yao wangeweza kutumia taarifa walizo nazo kama ni zakweli kuchukua hatua staili kwa mujibu wa sheria. Huku nyuma tumewahi sikia cuf na tuhuma ya visu, chama cha waislam nk, chadema na udini nk. Yakowapi, kimya. Nazidi kujiuliza kama igunga tu sasa tunasikia haya mazito, vipi 2015? Ninapata picha moja kuwa mambo ni magumu kwa magamba. Nakumbuka uchaguzi mdogo wa tarime baada ya kifo cha Wangwe Mungu amrehemu, aliyekuwa katibu mkuu wa ccm wakati huo ndugu makamba aliwahi kutuhumu jeshi la polisi kutofanya kazi yake vizuri,hii ni baada ya kuona mambo magumu na ukweli ulijionyesha ktk matokeo kwani ccm ilishindwa na cdm. Ni vema kumtaka ndg mukama na chama chake kutoa uthibitisho wa tuhuma hizi ili hatua zichukuliwe. Akishindwa pia achukuliwe hatua kwakujenga hofu ktk jamii kwa siasa uchwara za ccm kulingana na RA alipokuwa akiachia ngazi zake ktk ccm. Hatari sana kwa viongozi wenyemwelekeo wa kulazimisha mambo wananchi wanapo unyesha kuyakataa, kwani wanaweza kutuletea maafa ktk taifa letu, tuwakemee na kuwakataa kwa nguvu zote. Kila la kheri igunga, wanaigunga tumieni haki yenu vema.Ikumbukwe kuwa haki uleta amani. Mungu ibariki Tz.
 
Nimekumbuka ishu ya Visu na mapanga ya CUF, ilivyotufanya tuamini, wakanzani na wanatania bado ni wa karne ileee!!
 
hivi haya maneno katika kiapo chao ccm siku hizi hawakifuati?nanukuu nitasema kweli daima,fitina na majungu ni mwiko,cheo ni dhamana sitotumia cheo changu.....
 
Najua anajua alichosema sio sahihi ila kipropaganda anajua yeye ni sahihi!
hebu tafakari kwa mwananchi wa kawaida ana ambiwa hbr hzo lazima atapata hofu na woga hvyo kupoteza imani kwa CDM ambayo tayari ilikuwa tumaini lao!
tukumbuke uchaguzi mdogo wa kiteto mwaka 2008 walitumia picha za vurugu za kenya na CDM ikashndwa wakati matumaini makubwa ya ushindi yalikuwepo
lazima CDM wa take action kuzima hyo propaganda haraka la sivyo ni doa kubwa ukijumlisha na DC kuvuliwa hijab halipewa majibu
 
Nanyaro hujui unachoongea. Eti anasubiri kuapishwa....Subiri aibu ya kampuni/NGO yenu 2 Oct 2011. Hivyo anza kutafuta visingizio...kuchakachua kumepitwa na wakati. Labda kisingizio kizuri safari hii ni kuwepo kwa kambi za mafunzo Singida. Mtaishia kuwa walalamishi, wanung'unikaji.
 
Kinachonishangaza ni kuwa wanasema wanao ushahidi, basi naomba wawakamte kisha wawafungulie mashitka na kuthibitisha tuhuma zao? Hili jambo siyo la kulipuuza, nionavyo tayari JK atakuwa ameshampigia Mkama kumuonya aache ujinga wa kuropoka hovyo!

Sio rahisi JK kumuonya MUKAMA aache uropokaji kwa maana hata yeye mbona ni mropokaji mzoefu ,mfano, . aliwahi kusema anawajua wezi wa bandarini na akawapa wezi muda wajirekebishi
 
hivi haya maneno katika kiapo chao ccm siku hizi hawakifuati?nanukuu nitasema kweli daima,fitina na majungu ni mwiko,cheo ni dhamana sitotumia cheo changu.....

siku hizi ni kinyume chake. Nitasema uongo daima, ukweli kwangu mwiko, nitatumia cheo kwa masilahi binafsi, cheo si dhamana.
 
Back
Top Bottom