Mukama asema hatambui Mazungumzo ya Muafaka Arusha!

Hizi siasa za bongo zimejaa usanii mtupu!
Kweli mkuu,sababu hata sioni tume ya uchaguzi imetoa maamuzi gani kuhusu Arusha mjini,wamebaki wanasiasa wetu uchwara kudandia mambo bila kuangalia legality ya vitendo vyao.

Mukama ana sauti kuliko Pinda
Luhanjo ana power kuliko Pinda

wakati mwingine ni bora kuwa na waziri mkuu kama LOWASA kuliko PINDA
hayani ni fedheha kila kukicha, sasa mukama naye wa kumpiga biti waziri mkuu!!!!!!!

bora LOWASA hata kama alikuwa anaiba lakini ofisi ina heshima sasa vyote havipo, watu wanaiba na ofisi ya waziri mkuu haina heshima
nilipokuwa wakati wa sumaye sikutegemea kama tungekuja kupa waziri mkuu bomu kama sumaye.

Lakini sasa na regea kusema PINDA kavunja record toka haingie ofisini hapo miaka karibu saba sasa amewahikumpiga mkwara
magufuri tu kwenye issue ya bomoa bomoa lakini sasa watu wanalipa kwenye ACCOUNT BINAFSI pesa ya UDA lakini mkuu kimya
sujui yukoje

Hii ni abnormal simple jamani duh sijawahi kuona kiongozi goigoi kama huyu

huyu Pinda ni pazia tu,hivi mnakumbuka kafanya maamuzi gani vile?anaburuzwa tu,alikuja na sera ya v8 ameshanyamaza.kila.siku anaturubuni tu huku mchwa wanaendelea kula nchi,hivi nyie hamlioni hili?hana hata sauti kwa makatibu wakuu wa wizara wakati yeye ni waziri mkuu,hata kwa mameya walio chini ya TAMISEMI wakati yeye ni waziri mkuu,hamuoni huyu ni shati tu?

Napata shida sana kuwa na imani naye

Pinda anaongea kwa nafasi yake kama PM na Mukama kama CCM...kikao cha kumwagiza Pinda si lazima kimshirikishe Mukama pia maamuzi ya CCM sio lazima yazingatie nasaha za Pinda, japo ni vizuri wote kuwa aligned

Yeye anaona ni wastage of time wakati wenzao wako serious kuweka records za matukio ya ukiukwaji wa misingi na taratibu za kisheria tulizojiwekea.

Anasahau kwanba revolution is the outcome of simple ignored things. Njiti moja ya kiberiti inaweza kuleta maafa ambayo kamwe hayataweza kusahaulika katika historia.

Rich Dad, I presume you're also very rich at heart! Your words means a lot.
Mukama ni katibu mkuu wa CCM lakini that does not make him to be country' stateman.
Keep it up tajiri wa roho.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Wilson Mkama amesema hajui lolote na hatambui mazungumzo yoyote yanayoendelea kati ya Pinda na Chadema,

Akiongea na Radio Uhuru akiwa Morogoro juu ya Taarifa ya Kamati Kuu ya Chadema iliyotolewa leo Mukama amesema kwanza haoni sababu ya kuingia katika Mazungumzo kati ya Chadema na CCM kwani Meya wa Jiji la Arusha alipatikana kiharari!

Amesema ni wastage of time kwa watu wazima kupoteza muda na mgogoro usio na tija badala ya kuwaletea wananchi maendeleo! Anasema Chadema ni lazima waelewe kuwa mazungumzo wanayofanya ya Muafaka ni kati ya Pinda na Chadema kwani hakuna kikao chochote kilicho muagiza Pinda juu ya Jambo hilo!

Hilo ndio tatizo la uelewa mdogo wa baadhi ya viongozi ndani ya CCM,pengine hajui kwamba meya anafanya kazi chini ya TAMISEM ambayo bosi wao ni Pinda,hiyo ndio CCM kila mtu mkubwa kimadaraka.

Hilo ndio tatizo la uelewa mdogo wa baadhi ya viongozi ndani ya CCM,pengine hajui kwamba meya anafanya kazi chini ya TAMISEM ambayo bosi wao ni Pinda,hiyo ndio CCM kila mtu mkubwa kimadaraka.
Meya ni elected official...hana bosi,hapo ndio CDM mnapokosea.

Hata wakat wa utawala wa HITLER NA MUSSOLINI,WALE VIONGOZ WA CHAMA WALIKUWA WANANGUVU SANA SERIKALINI NA WALIKUWA WAFANYA MAAMUZ,SISHANGAI MUKAMA KUWA JUU YA PINDA

Meya ni elected official...hana bosi,hapo ndio CDM mnapokosea.

Kobello nilitarajii uwe na fikra za juu kuliko hapai. Kwa mtazamo huo huo.....

President ni elected offcial...hana boss
VP ni elected official....hana boss
MP ni elected official...hana boss
ward Councilor ni elected official...hana boss

Kwa hiyo nchi hii haina Boss??
Haya ni matokeo ya mahaba ya kichama yanapochukua nafasi ya fikra huru.

sasa hivi ni kufukuzana magamba flani afai wazirimkuu kasema mboye shujaa mukama nani bosiwake hakuna mpya

Kobello nilitarajii uwe na fikra za juu kuliko hapai. Kwa mtazamo huo huo.....

President ni elected offcial...hana boss
VP ni elected official....hana boss
MP ni elected official...hana boss
ward Councilor ni elected official...hana boss

Kwa hiyo nchi hii haina Boss??
Haya ni matokeo ya mahaba ya kichama yanapochukua nafasi ya fikra huru.
Mkuu,kwenye demokrasia ya ukweli,hakuna elected official aliye juu ya elected official.

Kwa siasa za kitemi hasa Afrika,hii kitu ndio ipo.Ni mahakama pekee itakayobainisha uhalali wa meya Lyimo,hata rais wako jeyk hawezi kumtoa umeya Lyimo au hata kwa mfano Mallah angekuwa meya ni mahakama ndiyo inayoweza kubatili uhalali wa meya.

Sasa hawa mbuzi wanakutana ili iwe nini?

Mkuu,kwenye demokrasia ya ukweli,hakuna elected official aliye juu ya elected official.
Kwa siasa za kitemi hasa Afrika,hii kitu ndio ipo.Ni mahakama pekee itakayobainisha uhalali wa meya Lyimo,hata rais wako jeyk hawezi kumtoa umeya Lyimo au hata kwa mfano Mallah angekuwa meya ni mahakama ndiyo inayoweza kubatili uhalali wa meya.
Sasa hawa mbuzi wanakutana ili iwe nini???

Tusichoke na mtaalam Nsiande wameiweka vizuri mapema sana.

Kwa sheria za nchi hii waziri mkuu ndiye kiongozi wa serikali za mitaa, waziri mkuu ana mamlaka ya kuvunja halimashauri ya mji/jiji.
Kama umekuwepo kwenye siasa za Tanzania kwa muda utakumbuka kwamba Sumaye alivunja halimashauri ya jiji la Dar na akamweka Keenja.

Anayesimamia uchaguzi wa Meya sio NEC ni mkurugenzi wa mji/jiji anayereport ofisi ya waziri mkuu. Kama Mbowe anafanya mazungumzo na Pinda ni sahihi zaidi kuliko mazungumzo na CCM coz nje ya mahakama ni waziri mkuu pekee mwenye uwezo kisheria kuingilia maswala ya halimashauri.

Hakuna demokrasia ya kweli Kobello, hata home kwako/kwenu hapawezi kuwa na demokrasia ya kweli!

Hapo ndio mnapochanganya mambo.Kisheria waziri mkuu(kupitia ofisi ya waziri wa nchi) ndiye msimamizi mkuu wa serikali za mitaa na Ofisi yake ina mamlaka ya kuanzisha na kuvunja serikali ya mtaa,kuongeza/kupunguza mipaka au eneo la serkali ya mtaa.Pia huajiri wafanyakazi mbalimbali wa halmashauri(non-elected).
Hata siku moja hii haimaanishi kuwa waziri mkuu ndiye mwenye kauli ya mwisho kuhusu uhalali wa viongozi waliochaguliwa,resident magistrate ndiye pekee anayeweza kuhalalisha au kutengua uhalali wa viongozi waliochaguliwa.
Local governmemts services act,1982 PART 3,SECTION26(1)(a)-(e).

Sasa kama wana nia ya kuvunja halmasahauri,hiyo wanaweza....ila kutengua uhalali wa viongozi waliochaguliwa na wananchi,huo utakuwa ni udikteta na upuuzi ambao ni wananchi wavivu ndio wanaufagilia.Binafsi,nadhani hawa jamaa wanachemka,na waziri mkuu angewaambia kuwa mahakasma ndiyo njia pekee.
Nashangaa mnapiga kelele kuhusu chama kuingilia serikali,wakati mwenyekiti wenu wa chama anastumia nafasi hiyo kujaribu kuingilia serikali iwafukuze mkurugenzi,OCD na iondoe kesi mahakamani dhidi yao.

Binafsi nakubaliana na maelezo ya Mukama kwani yana mantiki kwa kiasi fulani. Suala la Arusha ni suala la kisiasa zaidi na siyo suala la kiserikali. Ni suala ambalo mwanzo wake ni mgogoro wa kisiasa. Hivyo, suluhu yake ya kwanza ilitakiwe iwe ya kisiasa. Hivyo, lingehitaji maamuzi ya viongozi wa kisiasa na kushirikisha viongozi wa kisiasa kwa mambo yale yanayohusu siasa. HIvyo, kama lingekuwa linahusu siasa peke yake basi lilitakiwa liwe linahusisha mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Slaa na Katibu Mkuu Mukama na kulitafutia ufumbuzi.

Bahati mbaya, suala hili limetoka kwenye ulingo wa siasa na kuwa suala la serikali. Kwanza kutokana na taratibu za uchaguzi wa meya ambazo huongozwa na taratibu za kiserikali na pili mazingira ya maandamano na kesi zilizoko mahakamani ambazo vyote vinahusiana na suala la serikali. Kutokana na mantiki hii ya pili, tunaweza kuona kwa vile linahusiana na masuala ya serikali ya mitaa ambayo yanaangukia mikononi mwa Ofisi ya Waziri Mkuu basi hakuna mtu sahihi wa kufanya mazungumzo haya isipokuwa Waziri Mkuu.

HIvyo, Mukama hakuhitajika kabisa kuwa sehemu ya mazungumzo hayo na uhalali wa mazungumzo hayo hauitaji ridhaa, au baraka za CCM kwani suala hili si la kisiasa tena bali la kiserikali. Kutokana na hiilo kauli zote za Mukama hazihusiani na mazungumzo haya kwani Pinda hakwenda kuzungumza kama mwakilishi wa CCM bali kama kiongozi wa serikali ambaye anatafuta suluhisho la jambo ambalo linaingilia utendaji kazi wa serikali ya mitaa - in this case Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kwa hiyo hakuna namne yoyote ambayo Pinda anaweza kutaka kibali toka CCM kufanya jambo la serikali ambalo yeye aliapa kutekeleza na kusimamia.

Kwa sasa hamna haja ya CCM wala CDM kuongelea Arusha mpaka uchaguzi mdogo ufanyike na madiwani wapya kupatikana.

Back
Top Bottom