Mukama amponda Dr. Slaa Asema ni mchanga katika Duru za Siasa, Chadema ni hodari kusema Uongo

Imagine......utahitaji uwanja kama EMIRATES kuwafungia watu hawa uliowakamata........halafu utahitaji polisi kama 100,000 kuwakamata...weird statistics

According to Mkama, CCM watakua wanaogopa nichi kuongozwa na Jeshi maana wanajua madudu yao. Yeye mwenyewe atakua kwenye batch ya kwanza ya watu watakaokamatwa
 
Duh!,watu 50000?hizi takwimu katoa wapi?mpaka hapo na yeye ni muongo.Pili Kama Slaa ni mropokaji ccm watakuwa sehemu ya athari hizo za kuropoka na Kama ni kweli-KWA NINI CCM MSISHITAKI MAHAKAMNI?(nnajua hamtaenda na hamjawahi kwenda sbb ayasemayo Slaa ni ya kweli lazima tuamini hivyo.Jeshi likitawala itakuwa vizuri na niaminivyo jeshi kutawala litakuwa na faida kuliko hasara zake.Kuhusu matokeo ya uchaguzi kuwa ccm

inakubalika nnapinga sivyo kabisa sbb tume ya uchaguzi ilichakachua matokeo kuanzia ngazi za juu mpaka chini.Kuhusu Slaa chama chake ni kundi au kipo kikanda-Hapo amekosea na hizo ni propaganda za ccm kuwahadaa Watanzania wazembe kufikiri kuukubali ujinga wao na kwa style hii ya kiongozi Kama huyu Mkama anaonekana ni mbaguzi hasa anapokitaja Chama cha Chadema kuwa ni chama cha kikanda pia anayo dharau kusema Chadema ni kikundi cha watu-Nnasikitika Kama huyu Mkama bado analipwa mshahara ndani ya ccm yao
 
* Huyu Mukama ni mgonjwa anasema Wananchi wajifunze ya Misri Eti Kuandamana kwao kama Chadema kumeashiria Nchi kuongozwa Kijeshi

Wednesday, 11 May 2011 11:11 newsroom

NA WAANDISHI WETU - GAZETI LA UHURU

KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amemponda Dk. Wilbroad Slaa na kusema ni mwanasiasa anayejifunza. Amemfananisha Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na mtu anayebadilisha dini na kujifanya mjuaji kuliko aliowakuta na matokeo yake anaropoka kila kukicha na kutoa matamshi ya vitisho kwa wananchi. Mukama alisema CCM inajadili mambo
yake kwa uwazi na kilichofanyika ni mabadiliko ya kukijenga upya Chama na si vinginevyo, na kwamba kwa kutoa maneno ya uzushi Dk. Slaa ni sawa na mtoto anayelilia wembe, siku moja utamkata. Pia, amesisitiza kwamba hakuna waraka wa siri.

awilson%20mukama.jpg

Aliyasema hayo jana, wakati akifafanua kauli ya iliyotolewa na Dk. Slaa kupitia gazeti moja la kila siku lenye kichwa cha habari Dk. Slaa: Nchi haitatawalika, Anasa waraka wa siri wa CCM.
Katika gazeti hilo, Dk. Slaa alikaririwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Msakila mjini Sumbawanga ambapo alisema amebaini waraka wa siri wa CCM uliokuwa na muhuri wa SIRI ambao amedai CCM imekiri kuwa haikubaliki.

Mukama alisema Dk. Slaa, haelewi nini maana ya nchi kutotawalika kwani Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia, inawekezeka kiuchumi na wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.

Dk. Slaa hana karama ya kutawala, kiongozi makini hupima hata matamshi yake, anazangumza mambo yenye mwelekeo wa kuwakosesha amani, lakiniwakati wao wakiendelea na maandamano, Serikali ya CCM inajenga miundombinu ya kusafirisha mazao, alisema.

Aliwataka wananchi wajifunze yanayotokea Misri, ambako wameandamana na sasa wanaongozwa na jeshi la nchi hiyo, kila siku watu 50,000 wanakamatwa na kuhukumiwa.

Alisema CHADEMA ni hodari wa kusema uongo, kwa kutumia haki yao ya kujieleza kusambaza uzushi na kwamba CCM haiwezi kushindana nao kwa kuzua mambo.

Mukama alisema wamekuwa wakiwapatia vijana sh. 500 kuwavuta kwenye maandamano na kuwadanganya kwamba watawaondolea umasikini kupitia maandamano hayo.

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, alisema chanzo ni matatizo ya kisiasa yaliyozikumba nchi za Magharibi ikiwemo Libya ambao ndio wenye visima vya mafuta, nishati hiyo imepanda bei katika soko la dunia, na viwanda vyote nchini vinaendeshwa kwa kutegemea mafuta.

Hakuna siri yoyote CCM, imejipanga kuboresha utendaji wa Chama kwa kuangalia vigezo vya msingi, na kila kimoja kimepitia kwenye vikao halali vya kikatiba, alisema.

Akifafanua Mukama alisema CCM si kundi la watu ama ukoo fulani kama ilivyo CHADEMA, bali ni Chama kinachoendeshwa kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake tangu enzi za TANU na ASP.

Alisema katika mkakati wa kufanya mageuzi CCM ilipanga kuboresha mambo muhimu, ikiwemo fikra na itikadi, muundo wake, viongozi wa Chama, watendaji, usalama na maadili, wanachama na kujiimarisha kiuchumi na fedha.

Mukama alisema vigezo hivyo vyote havina usiri bali ni mikakati ambayo imewekewa mipango ya utekelezaji kwa maana ya kuunda CCM yenye mwelekeo tofauti.

Alitoa mfano wa mambo yaliyobadilishwa ni kufanya uchaguzi wa Chama na jumuia kwa mwaka mmoja ili kupunguza muda wa kushughulikia uchaguzi kutoka miaka mitatu kwenda minne.
ÒMiaka mitano ya utawala, ni mwaka mmoja tu ndo hatufanyi uchaguzi, mwakani tuna uchaguzi wa Chama , tumeona tufanye pamoja na jumuia, ili tupumzike 2013, 2014 tubaki na uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, alisema.

Alisema pia katika usalama na maadili, iliangaliwa viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa rushwa na vitendo vingine viovu, ilionekana hawawezi kusimamia vitendo vya kimapinduzi ambavyo Chama kinavitekeleza.

Ni jambo la kawaida kufanya marekebisho hususan katika kipindi ambacho CCM inakubalika kwa wananchi, bado tuna nafasi kubwa hata katika uchaguzi wa 2010 imedhihirisha tumepata majimbo 187 mara tisa zaidi ya majimbo 22 ya CHADEMA, alisema.

Alisema matokeo ya uchaguzi huo yamebainisha kwamba CCM bado inakubalika kwani hata wabunge wa viti maalumu ambao hupatikana kutokana na wingi wa kura , CCM ina wabunge 67 na vyama vingine vina wabunge 35.

Hivi karibuni CCM ilifanya mabadiliko makubwa kwa kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi waandamizi, walijizulu na kujipanga upya, ambapo nafasi ya Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na Yussuf Makamba ilichukuliwa na Mukama.

Siku chache baada ya mabadiliko hayo, baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM, walianza njama za kuwachafua viongozi waandamizi akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

mweeeee mweeeeeeee wmweeeeeeeeeeeeeeeee!!
Huyu mzee nae anazeeka vibaya;chama cha magamba wapime wenyewe wapimpa chizi rungu !! tena sokoni:mimba::A S 103::A S 103:
 
Jamani msameheni bure huyu mzee chapombe, inawezekana aliamka nao kwa kiwewe cha madaraka mapya kasahau kunywa supu. Kifupi huyu ni fisadi kama mafisadi wengine kwenye lichama la mafisadi kwa hiyo tumpuuze tu, hana jipya na hana ubavu mbele ya wenye chama kina RA&EL. Huyo mwenyekiti wao mwenyewe anawagwaya hao vidume itakuwa huyo mlevi mbwa?
 
Mukama anapokosoa mabadiriko yanayotokea Misri anakuwa amesahau kuwa hadi sasa Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Misri keshafungwa miaka kumi na zaidi jela pamoja na kuamuriwa kurudisha fedha za umma alizofisadi?

Mukama atueleze kama serikali ya genge lake la chama cha magamba wanaweza kuchukua hatua bold kama hii kulinda mali ya umma
 
CCM wamepanda upya ili kubadilisha mbegu "chafu" ya msimu uliopita...walichosahau ni kwamba msimu wao wa kupanda umeshapita na mvua za kupandia nzazo hazipo tena!
 
mukama kawadanganya ccm, kafanya utafiti wa aina yake, ameshauri kuvua gamba ili apate ukatibu mkuu, matokeo yake gamba limegoma kuvuka kaibuka na mpya hatukuwahi kusema tutavua magamba, mtamkumbuka makamba muda si mrefu. cost vs benefit za kuvua gamba. cost outweighs benefits therefore stop. viva mukama viva. hureeeeeeeeeeeeeee
 
WA ZAMANI ALIKUWA NA NUNDU WA SASA ANA UPARA, CDM NI CHAMA CHA UKOO FULANI, SAWA, KUNA MBOWE NDUGU YAKE NI NANI MWINGINE CDM? WENJE KUNA WENJE MWINGINE CDM, MAREHEM SHELEMBI KUNA SHELEMBI MWINGINE CDM,ZITTO KUNA ZITTO MWINGINE CDM?

CCM KUNA YUSUF MAKAMBA PIA KUNA JANUARY MAKAMBA
2. JAKAYA KIKWETE KUNA RIDHWAN KIKWETE
3.ALLY HASSAN MWINYI KUNA HUSSEIN MWINYI
4.MOSES NNAUYE KUNA NAPE NNAUYE
5.JOHN NCHIMBI KUNA EMMANUEL NCHIMBI
6.ROSTAM AZIZ KUNA HUSSEIN BASHE
7. SAMUEL SITTA NA MAGRET SITTA

WANATAKA AKIMALIZA KIKWETE AMPE HUSSEIN MWINYI NA BAADA YA HUSSEIN MWINYI NI RIDHWAN KIKWETE, AMA KWELI CCM NI GAMBA
wOTE HAO NI WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAGAMBA MTU NA MTOTO WAKE , KAMA WANATAKA TUWAWEKEE AU TUWATAJE NA MAHAWARA ZAO WALIOWAPA NAFASI KWENYE MAGAMBA

Mambo mengine ni kujifanya kipofu kwa makusudi.

Mbowe->Mtei->Ndensabulo->Komu->Slaa->Rose kamili>christna Lissu->
fuatilia hiyo link.
 
Hii ni ngoma ambayo inaelekea patamu! Nadhani tuendako tutarajie heading za magazeti kusomeka km ifuatavyo!

-"Baada ya hali ngumu ya maisha hatimaye wananchi wavamia mgodi na kuchoma moto wawekezaji"

-"Askari waungana na wananchi kudai haki zao na kikosi maalum cha jeshi kilichotumwa kukabiliana na hali hiyo nacho chaungana na wananchi baada ya kuona madai yao ni ya msingi"

-Wananchi wajichukulia sheria mikononi kwa kwa kuwakatakata kwa mapanga majangili waliovamia hifadhi ya Taifa

-Maandamano yaendelea sehemu mbali mbali za nchi na madai ya wananchi ni kwamba mali ambayo wamejitwalia wageni bila utaratibu irejeshwe na mikataba ya kinyonyaji ivunjwe
 
Jamani msameheni bure huyu mzee chapombe, inawezekana aliamka nao kwa kiwewe cha madaraka mapya kasahau kunywa supu. Kifupi huyu ni fisadi kama mafisadi wengine kwenye lichama la mafisadi kwa hiyo tumpuuze tu, hana jipya na hana ubavu mbele ya wenye chama kina RA&EL. Huyo mwenyekiti wao mwenyewe anawagwaya hao vidume itakuwa huyo mlevi mbwa?

Ah, kumbe naye anapata sana, basi bwana:grouphug:
 
Ukabila na ukanda naamini CHADEMA wanaongoza. Ukichukua kabisa hali halisi ya kimahesabu yani ukubwa wa chama kugawia ukanda na udungu.Mhhh
 
* Huyu Mukama ni mgonjwa anasema Wananchi wajifunze ya Misri Eti Kuandamana kwao kama Chadema kumeashiria Nchi kuongozwa Kijeshi

Wednesday, 11 May 2011 11:11 newsroom

NA WAANDISHI WETU - GAZETI LA UHURU

KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amemponda Dk. Wilbroad Slaa na kusema ni mwanasiasa anayejifunza. Amemfananisha Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na mtu anayebadilisha dini na kujifanya mjuaji kuliko aliowakuta na matokeo yake anaropoka kila kukicha na kutoa matamshi ya vitisho kwa wananchi. Mukama alisema CCM inajadili mambo
yake kwa uwazi na kilichofanyika ni mabadiliko ya kukijenga upya Chama na si vinginevyo, na kwamba kwa kutoa maneno ya uzushi Dk. Slaa ni sawa na mtoto anayelilia wembe, siku moja utamkata. Pia, amesisitiza kwamba hakuna waraka wa siri.

awilson%20mukama.jpg

Aliyasema hayo jana, wakati akifafanua kauli ya iliyotolewa na Dk. Slaa kupitia gazeti moja la kila siku lenye kichwa cha habari Dk. Slaa: Nchi haitatawalika, Anasa waraka wa siri wa CCM.
Katika gazeti hilo, Dk. Slaa alikaririwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Msakila mjini Sumbawanga ambapo alisema amebaini waraka wa siri wa CCM uliokuwa na muhuri wa SIRI ambao amedai CCM imekiri kuwa haikubaliki.

Mukama alisema Dk. Slaa, haelewi nini maana ya nchi kutotawalika kwani Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia, inawekezeka kiuchumi na wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.

Dk. Slaa hana karama ya kutawala, kiongozi makini hupima hata matamshi yake, anazangumza mambo yenye mwelekeo wa kuwakosesha amani, lakiniwakati wao wakiendelea na maandamano, Serikali ya CCM inajenga miundombinu ya kusafirisha mazao, alisema.

Aliwataka wananchi wajifunze yanayotokea Misri, ambako wameandamana na sasa wanaongozwa na jeshi la nchi hiyo, kila siku watu 50,000 wanakamatwa na kuhukumiwa.

Alisema CHADEMA ni hodari wa kusema uongo, kwa kutumia haki yao ya kujieleza kusambaza uzushi na kwamba CCM haiwezi kushindana nao kwa kuzua mambo.

Mukama alisema wamekuwa wakiwapatia vijana sh. 500 kuwavuta kwenye maandamano na kuwadanganya kwamba watawaondolea umasikini kupitia maandamano hayo.

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, alisema chanzo ni matatizo ya kisiasa yaliyozikumba nchi za Magharibi ikiwemo Libya ambao ndio wenye visima vya mafuta, nishati hiyo imepanda bei katika soko la dunia, na viwanda vyote nchini vinaendeshwa kwa kutegemea mafuta.

Hakuna siri yoyote CCM, imejipanga kuboresha utendaji wa Chama kwa kuangalia vigezo vya msingi, na kila kimoja kimepitia kwenye vikao halali vya kikatiba, alisema.

Akifafanua Mukama alisema CCM si kundi la watu ama ukoo fulani kama ilivyo CHADEMA, bali ni Chama kinachoendeshwa kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake tangu enzi za TANU na ASP.

Alisema katika mkakati wa kufanya mageuzi CCM ilipanga kuboresha mambo muhimu, ikiwemo fikra na itikadi, muundo wake, viongozi wa Chama, watendaji, usalama na maadili, wanachama na kujiimarisha kiuchumi na fedha.

Mukama alisema vigezo hivyo vyote havina usiri bali ni mikakati ambayo imewekewa mipango ya utekelezaji kwa maana ya kuunda CCM yenye mwelekeo tofauti.

Alitoa mfano wa mambo yaliyobadilishwa ni kufanya uchaguzi wa Chama na jumuia kwa mwaka mmoja ili kupunguza muda wa kushughulikia uchaguzi kutoka miaka mitatu kwenda minne.
ÒMiaka mitano ya utawala, ni mwaka mmoja tu ndo hatufanyi uchaguzi, mwakani tuna uchaguzi wa Chama , tumeona tufanye pamoja na jumuia, ili tupumzike 2013, 2014 tubaki na uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, alisema.

Alisema pia katika usalama na maadili, iliangaliwa viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa rushwa na vitendo vingine viovu, ilionekana hawawezi kusimamia vitendo vya kimapinduzi ambavyo Chama kinavitekeleza.

Ni jambo la kawaida kufanya marekebisho hususan katika kipindi ambacho CCM inakubalika kwa wananchi, bado tuna nafasi kubwa hata katika uchaguzi wa 2010 imedhihirisha tumepata majimbo 187 mara tisa zaidi ya majimbo 22 ya CHADEMA, alisema.

Alisema matokeo ya uchaguzi huo yamebainisha kwamba CCM bado inakubalika kwani hata wabunge wa viti maalumu ambao hupatikana kutokana na wingi wa kura , CCM ina wabunge 67 na vyama vingine vina wabunge 35.

Hivi karibuni CCM ilifanya mabadiliko makubwa kwa kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi waandamizi, walijizulu na kujipanga upya, ambapo nafasi ya Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na Yussuf Makamba ilichukuliwa na Mukama.

Siku chache baada ya mabadiliko hayo, baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM, walianza njama za kuwachafua viongozi waandamizi akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Mukama sijui Mkama kwanza pole siku chache tu umeshachoka hivi,please visit a clinic for some advice,mambo magumu.
 
ORODHA ya majina ya wateule wanaosubiri kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambayo uteuzi wake ulikwama katika njia ya demokrasia za ndani ya chama hicho, imevuja ndani ya chama hicho.

Majina 105 ya wateule hao waliopatikana kwa njia ya ushauri wa mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya njia ya kura kushindikana, yamo ya wake, watoto na ndugu wa vigogo na viongozi wa chama hicho.

Njia ya kura ilishindikana kutokana na kuibuka kwa makundi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, wakati wa uchaguzi wa wabunge hao kupitia wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

Katika uchaguzi huo, ilibainika kuwa baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo walikuwa mamluki na baadhi ya wagombea kutoa kauli za kuulaumu uongozi kwa kutaka kuwapa ulaji wagombea wa viti maalumu wanaowataka.

Lawama hizo zimejidhihirisha kwani katika orodha hiyo, mbali na watoto na ndugu wa vigogo wa chama hicho, pia wabunge wote wa viti maalumu wa Chadema waliomaliza muda wao, wakiwamo wanaogombea katika majimbo ya uchaguzi, wamerudishwa katika orodha hiyo na kupewa nafasi za juu.

Wabunge waliomaliza muda wao walioko katika orodha hiyo ni Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo; na ni wa kwanza, jambo linalomhakikishia ubunge ikiwa uteuzi utafanyika kwa kufuata wa kwanza mpaka wa mwisho.

Wengine ni Mhonga Ruhwanya (namba 3), Halima Mdee (5), Grace Kiwelu (9) ambaye ni mkwewe Ndesamburo, Anna Komu (13) na Susan Lyimo (10).

Pia yumo Rose Kamil Sukum (19) ambaye ni mke wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Aidha, kwa mfumo huo wa Chadema, wagombea ubunge ambao wamo miongoni mwa majina hayo, watajihakikishia ‘ulaji' bungeni endapo watashindwa katika majimbo hayo.

Wagombea hao wa majimbo walioko katika orodha hiyo ni Mdee wa Kawe, Leticia Nyerere (16), Kwimba; Regia Mtema (11), Kilombero na Sukum, Hanang. Wengine ni Christina Lissu Mughiwa (20) na Paulina Slaa Narcis (84).

Orodha hiyo pia imewataja Easther Matiko(2), Anna Mallac (4), Paulina Gekul (6), Conjesta Rwamlaza (7), Susan Kiwanga (8), Christowaja Mtinda (12), Mwanamrisho Abama (14), Joyce Mukya (15), Naomi Kaihula (17), Chiku Abwao (18), Raya Hamisi (21), Philipa Mturano (22) na Mariam Msabaha (23).

Wengine ni Rachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30), Rosana Chapita (31), Mona Bitakwate (32), Evarim Mpangama (33), Asha Kayumba (34), Hija Wazee (35), Mary Martin (36), Sophia Mwakagenda (37), Bupe Kyambika (38), Magreth Mangowi (39), Esther Daffi (40), Jane Pesha (41), Aikande Kwayu (42) na Helga Mchomvu (43).

Pia orodha hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Rebecca Magwisha (44), Neema Msuya (45), Anastazia Manyanda (46), Selina Nguma (47), Bertha Matanwa (48), Christina Ngola (49), Lydia Mwaipaja (50), Zaituni Lubinza (51), Adelastela Kilindi (52), Hawa Mwaifunga (53), Loyce Iboma (54) na Rita Kanoro (55).

Aidha wamo Monica Saile (56), Saida Othman (57), Edith Malale (58), Zainab Bakari (59), Rehema Makoba (60), Hadija Lyellu (61), Mary Komba (62), Rosale Lyimo (63), Omega Makundi (64), Marieth Chenyege (65), Veronica Ngale (66), Monica Mutasigwa (67), Judith Elyawoni (68), Rose Makara (69), Cecilian Ndossi (70) na Catherine Sakaya (71).

NB : Mambo mengine tuwe tunaambiana tu ukweli, wafuatilie na akina Regia Mtema tupate ukweli wao. Tanzania hakuna demokrasia ila kuna udugu, ukanda na rushwa ya ngono. Wala hakuna haki yoyote wala ukombozi, Mkombozi wa taifa hili bado hajaja
 
Mukama is another Joke.
Kwa wale ambao labda mna CV yake, huyu jamaa aliwahi kushika wadhifa wa kupigiwa kura na wananchi? Hata hiyo nafasi aliyonayo sasa hivi naye kapewa baada ya kutunga uongo kwenye ripoti yao kuwa JF inamilikiwa na CHADEMA. Mambo mengine kweli si lazima uingie darasani au kupata semina elekezi ili kuwa na UFAHAMU.

Kama CCM wanajadili mambo kwa uwazi, iweje Nape aseme iliamuliwa fisadiz wajiondoe within 90 days halafu Mukama anakuja anadai kuwa kulikuwa hakuna maamuzi kama hayo. Baada ya hapo Mwenyekiti wao Taifa ambaye ni Rais JK anadai anachokisema Nape ndicho chama kimeamua. Sasa uwazi hapa uko wapi?

Yaani hapa utaona kuwa tatizo ni chama. Mukama na Nnauye walikuwa na heshima zao kwenye jamii ingawa huwezi kulinganisha na ya Dr. wa UKWELI (Slaa), lakini sasa hivi they are jokes. Angalia hapa chini UMukama akiwemo)......

13.JPG

Ukiwa mwanachama wa CDM ni raha tu katika maisha yako kwani ni upande wa HAKI wenye kujali maisha yako wewe Mtz kuliko CCM ni PRESHA na matumaini ya uongo unaojali matumbo ya wachache!!
 
CDM mjiande kujibu hoja sasa na sio kulia lia .... Dozi(Hoja) ndio hizo zimeanza kutoka sasa!

Mmh kama hizi ndiyo dozi na upupu si itakuwa ni balaa tupu. Kwa watanzania especially wana-CCM kuwaambia kuwa hizo ni dozi kweli unawadhalilisha. Na kibaya zaidi ni pale hao wana-CCM wanakubali kudhalilishwa.

Strategy ya JK ilikuwa kuleta Sekretarieti itakayofanya zaidi ya ile iliyokuwa chini ya Makamba. Wana-pupulize kisha tunaambiwa kuwa ni dozi. Sasa wakianza kufanya upupu kwa level yao itakuwaje kwa watanzania wengine?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom