Mukama ameikejeli Katiba!

CDM,CUF,NCCR wakiwa ni vibaraka wa yeyote yule, tunachotaka ni siasa na demokrasia ya ukweli..

hakuna kitu kinachonikera kama mbinu na mikakati ya kuua vyama pinzani. Huu ni mpango mbaya kabisa, kwani siku CDM na vyama vingine vitakapokufa ndo itakuwa tumepata demokrasia ya kweli??

Demokrasia inahitaji kukuzwa ili kuwe na uwajibikaji wa kutosha kwa chama kilichopo madarakani. Ningefurahi kama vyama vya upinzani vingeendelea kupewa misaada ya kila hali ili vifanye shughuli, kuliko mipango ya sasa ya kuviteketeza ili CCM ibaki madarakani..Demokrasia haiendelei kwa kuvifanya vyama vingine vikose uhai..(haina maana)

Hakuna asiyetaka vyama vya upinzani viendelee, ila sasa angali kama hivi vinavyo anzishwa na mataifa ya nje ndivyo vyama watanzania wanavitaka ? wanajimaliza wao wenyewe mkuu
 
101576126_5ed4a5f57c.jpg
 
Who is Nyerere by the way mpaka watu wote lazima wakubaliane na mawazo yake?mbona wengi walishampinga hadharani na alikuwa anawapa ubalozi ili wawe nje ya nchi na wasishughulike na siasa za ndani?naye ni mtu ambaye alikuwa na haki ya kuwa challenged,

Twende kwenye hoja Mzee Mtei walitofautiana na Nyerere kuhusu kushusha thamani ya shilling na yeye km waziri wa fedha/gavan akagoma mbona mwaka jana China wametakiwa kushusha thamani ya fedha yao nao wakagoma na wao ni wa soshalisti?

Mara baada ya kutofautiana Mtei alifanya nini?aliiandika barua ya kujiuzulu na sio kung'ang'ania madaraka na kutekeleza sera usizo ziamini, leo viongozi wangapi wa CCM wanatekeleza yale wasio ya amini?Mfumo wa vyama vingi vilipoanzshwa zaidi ya miaka 15 toka Mtei kujiuzulu akaanzisha CDM ili apate fursa ya kutekeleza yale aliyo ya amini.

1995 Mrema alipokuwa juu Nyerere alisema msitishike nae huyo bali kuweni Makini na kina Mtei ndio tishio kwa CCM na hiyo ni 1995 ambapo wachahce waliifahamu na kuijua CDM, wengi walimwamini Mrema na NCCR lakini kwa Nyerere CDM ilibaki tishio kwake

Barua ya kujiuzulu hakuandika kwa hiari yake alilazimishwa kujiuzulu baada ya kuonekana ni msaliti wa nchi. Gabbage in Gabbage out, unategemea chama kilichoanzishwa na msaliti wa nchi, na chenyewe kitakuwa kisaliti tu
 
Katibu Mkuu mpya wa CCM amesema CDM itakufa mara 100 kwa kuwa ni chama kimeanzishwa kwa matakwa ya IMF na aliye anzisha CDM ni mtu aliyetofautiana na Nyerere, naomba kuweka kumbukumbu sawa kwa Mukama na wengine wote;

Kwanza, Who is Nyerere by the way mpaka watu wote lazima wakubaliane na mawazo yake?mbona wengi walishampinga hadharani na alikuwa anawapa ubalozi ili wawe nje ya nchi na wasishughulike na siasa za ndani?naye ni mtu ambaye alikuwa na haki ya kuwa challenged, mbona kule kuitikia zidumu fikra sahihi za M/Kiti wa CCM waliacha kuitikia na kuanza kuguna ndani ya ccm kwenyewe?

Twende kwenye hoja Mzee Mtei kutofautiana na Nyerere na hii ilikuwa kuhusu kushusha thamani ya shilling na yeye km waziri wa fedha/gavana akagoma, mbona mwaka jana China wametakiwa kushusha thamani ya fedha yao nao wakagoma na wao ni wa soshalisti?

Mara baada ya kutofautiana Mtei alifanya nini?aliiandika barua ya kujiuzulu na sio kung'ang'ania madaraka na kutekeleza sera asizo ziamini, leo viongozi wangapi wa CCM wanatekeleza yale wasio ya amini?Mfumo wa vyama vingi vilipoanzshwa zaidi ya miaka 15 toka Mtei kujiuzulu akaanzisha CDM ili apate fursa ya kutekeleza yale aliyo ya amini.

1995 Mrema na NNCR alipokuwa juu Nyerere alisema msitishike nae huyo bali kuweni Makini na kina Mtei ndio tishio kwa CCM na hiyo ni 1995 ambapo wachache wetu/wenu waliifahamu na kuijua CDM, wengi walimwamini Mrema na NCCR lakini kwa Nyerere CDM ilibaki tishio kwake

Kuhusu hoja ya chama kuanzishwa kwa shinikizo la IMF, swali hapa nani dhaifu, walio anzisha chama au waliokubali kuingiliwa utawala wa ndani na siasa zao?mbona China na CUBA hawajatekeleza hayo mashinikizo?kwangu CCM ndio dhaifu kwa kukubali kupelekeshwa na mataifa ya nje, vyama vingi viliporuhusiwa watu wakatumia haki yao ya kikatiba na kuvianzisha na kueleza itikidai na sera zao ambazo kimsingi ni hamasa kubwa kwa CCM imewasaidia kuwajibika zaidi na hata walioanzisha ni wenye nguvu serikalini mfano Prof Kighoma Malima, Oscar Kambona na wengine wengi

Sio sahihi hata kidogo kusema CDM itakufa kwa kuwa tu kimeanzishwa kwa shinikizo la IMF, historia inaonyesha mataifa mengi tu hivi vyama vilivyoanzishwa kwa shinikizo la IMF vimeshashinda chaguzi nyingi na bado imara, mfano mzuri ni Ghana, Zambia, Malawi, Uganda, Ivory Coast
 
OSAMA I APPRECIATE YOUR KIND FOR KILLING MUKAMA STORIES TO THE NEWS:israel::israel:
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk
Nadhani una taahira ya ubongo, hahahaaaaaaaaaaa
Hivi unajua Mtei alikorofishana na Mwalimu kuhusu lipi? Yeye alidhani uchumi wa soko ndio muafaka kwa dunia ya wakati huo, Mwalimu akasema hapana. CCM inafuata sera gani? Sasa kama CCM ndio mliodanganywa na World Bank kuuza hata NBC yetu kwa bei chee na nchi mkaibinafsisha kwa bei chee kati ya CCM na Chadema ni akina nani vibaraka wa WB? Plz fikiria usiwe kama zuzu unameza kila kitu. Ukiangalia Mtei aliangalia mbali sana na ndio maana Mwalimu hajawahi kumchukia
 
'………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha'.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk

Jamii Forums inasomwa na watu wengi sana ndani na nje ya Tanzania. Na wasomaji hawa wapo watanzania na wasio watanzania ili mradi wanaelewa kiswahili. Hili jukwaa linatupa nafasi nzuri ya kutoa maoni na michango ambayo kimsingi ni ya kujenga taifa hata kama ni kukosoa basi ni constructive criticism. Na ndio sababu watu wanasema ni jukwaa la 'great thinkers'.

Vyama vya siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Na vyote vinasajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria husika. CCM, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, NLD, DP, Demokrasia Makini vyote hivi vimesajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliwekwa.(wasiliana na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupata nakala). niishie hapo.

IMF - nadhani unaongelea International Monetary Fund ni taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na maswala ya kifedha na uchumi kwa nchi wanachama. Narudia - nchi wanachama. IMF wanachama wake ni NCHI na sio chama au kikundi kimoja kimoja. NCHI.

@GeniusBrain, naomba usome hii "IMF is an organization of 187 countries, working to foster global monetary cooperation, secure financial stability, facilitate international trade, promote high employment and sustainable economic growth, and reduce poverty around the world".

Tanzania ni mwanachama wa IMF na ndio maana tumekuwa tumapata mikopo huko. CHADEMA hata CCM au chama kingine chochote hakiwezi kuwa mwanachama wa IMF hata kama wangetaka iwe hivyo.

Nirudi kwenye point yangu ya msingi, Ndugu yangu GeniusBrain hoja yako si tu ni aibu kwako binafsi bali pia inatuibisha watanzania wote (milioni 42 na ushee), kwamba, hatujui maudhui na kazi za taasisi za kimataifa kama IMF. Na mbaya zaidi hatujui hata vyama vya siasa ndani ya mipaka ya nchi yetu vinanzishwaje.

Sijui ulikuwa unalenga nini hasa kwa kuanzisha hii hoja ila nadhani tuhimizane humu jamvini ili hii kasumba ya porojo, character assissination, mudslinging na cheap political scoring tactic zikome. Ni aibu mno kwetu sisi watanzania.

Mwisho ningekusihi sana ndugu yangu GeniusBrain na wengine wenye maoni kama yako watambue kuwa watanzania wana akili timamu na wana uwezo wa kutenganisha mema na mazuri. Maneno kama...chama fulani kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi' ni madharau kwa watanzania wenzako (insult to our intelligency).Tabia ya kikoloni hii.

Tutumie hili jukwaa kwa kuongelea mambo ya msingi na yenye tija tuache kuaniaka umbumbu wetu hadharani.
 
Kumbuka ni Mwl aliyetamka kuwa" CHADEMA VEMA" Uongo wako unatisha.Tumia muda wako vema kuliko kuongopea umma wa wa Tanzania.
 
Jana nimemsikiliza nilichogundua ile ripoti ya utafiti aliyoitayarisha alikuwa anajifagilia njia ili kupata ulaji maadamu alichokuwa anakitafuta amekipata sasa hataki kuwakwaza wengine hasa mafisadi ili asiwe na makundi, kweli ccm hakuna mwenye nafuu, na huyu Nape bora arudi masasi kwani kufanya kazi na huyo mzee itakuwa ngumu sana kwani wanapishana kimtazamo kuhusu ilo gamba lao.
 
Kipi bora wenye magamba ambao wameisha jivua magamba au kuwa chama cha vibaraka wa nje ? kuishi kwingi ni kuona mengi

Nilishakushauri kubadili jina uwe RETARDEDbrain.
Hiyo nyimbo unayoimba ya kujivua gamba wenzio walioitunga wamesha ifuta, we bado umebebana nayo.
Nnauye na Mukama wanatunga nyingine kwa sasa.
 
Jamii Forums inasomwa na watu wengi sana ndani na nje ya Tanzania. Na wasomaji hawa wapo watanzania na wasio watanzania ili mradi wanaelewa kiswahili. Hili jukwaa linatupa nafasi nzuri ya kutoa maoni na michango ambayo kimsingi ni ya kujenga taifa hata kama ni kukosoa basi ni constructive criticism. Na ndio sababu watu wanasema ni jukwaa la 'great thinkers'.

Vyama vya siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Na vyote vinasajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria husika. CCM, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, NLD, DP, Demokrasia Makini vyote hivi vimesajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliwekwa.(wasiliana na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupata nakala). niishie hapo.

IMF - nadhani unaongelea International Monetary Fund ni taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na maswala ya kifedha na uchumi kwa nchi wanachama. Narudia - nchi wanachama. IMF wanachama wake ni NCHI na sio chama au kikundi kimoja kimoja. NCHI.

@GeniusBrain, naomba usome hii "IMF is an organization of 187 countries, working to foster global monetary cooperation, secure financial stability, facilitate international trade, promote high employment and sustainable economic growth, and reduce poverty around the world".

Tanzania ni mwanachama wa IMF na ndio maana tumekuwa tumapata mikopo huko. CHADEMA hata CCM au chama kingine chochote hakiwezi kuwa mwanachama wa IMF hata kama wangetaka iwe hivyo.

Nirudi kwenye point yangu ya msingi, Ndugu yangu GeniusBrain hoja yako si tu ni aibu kwako binafsi bali pia inatuibisha watanzania wote (milioni 42 na ushee), kwamba, hatujui maudhui na kazi za taasisi za kimataifa kama IMF. Na mbaya zaidi hatujui hata vyama vya siasa ndani ya mipaka ya nchi yetu vinanzishwaje.

Sijui ulikuwa unalenga nini hasa kwa kuanzisha hii hoja ila nadhani tuhimizane humu jamvini ili hii kasumba ya porojo, character assissination, mudslinging na cheap political scoring tactic zikome. Ni aibu mno kwetu sisi watanzania.

Mwisho ningekusihi sana ndugu yangu GeniusBrain na wengine wenye maoni kama yako watambue kuwa watanzania wana akili timamu na wana uwezo wa kutenganisha mema na mazuri. Maneno kama...chama fulani kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi' ni madharau kwa watanzania wenzako (insult to our intelligency).Tabia ya kikoloni hii.

Tutumie hili jukwaa kwa kuongelea mambo ya msingi na yenye tija tuache kuaniaka umbumbu wetu hadharani.

Elewa maana ya kuanzishwa ilivyo andikwa kwenye thread yenyewe. Na hili liko wazi IMF ndio walioanzisha vyama vingi kwa shinikizo zao
 
Kumbuka ni Mwl aliyetamka kuwa" CHADEMA VEMA" Uongo wako unatisha.Tumia muda wako vema kuliko kuongopea umma wa wa Tanzania.

Na mwalimu huyo huyo aliisema ' Rais na kiongozi bora atatoka CCM'. Na kauli nyingine mwalimu alisema ' bila CCM imara nchi itayumba'. Mbona hakusema maneno hayo kui refer CDM ? Tafakari na zingatia
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk
Nyerere alitofautiana hata na walio ndani ya chama chake................... Na ndiyo maana wengine aliwawekea vikwazo kuwania urai kwa vile alijuwa watatakiwa kulipa fadhira
 
Jamii Forums inasomwa na watu wengi sana ndani na nje ya Tanzania. Na wasomaji hawa wapo watanzania na wasio watanzania ili mradi wanaelewa kiswahili. Hili jukwaa linatupa nafasi nzuri ya kutoa maoni na michango ambayo kimsingi ni ya kujenga taifa hata kama ni kukosoa basi ni constructive criticism. Na ndio sababu watu wanasema ni jukwaa la 'great thinkers'.

Vyama vya siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Na vyote vinasajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria husika. CCM, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, NLD, DP, Demokrasia Makini vyote hivi vimesajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliwekwa.(wasiliana na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupata nakala). niishie hapo.

IMF - nadhani unaongelea International Monetary Fund ni taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na maswala ya kifedha na uchumi kwa nchi wanachama. Narudia - nchi wanachama. IMF wanachama wake ni NCHI na sio chama au kikundi kimoja kimoja. NCHI.

@GeniusBrain, naomba usome hii "IMF is an organization of 187 countries, working to foster global monetary cooperation, secure financial stability, facilitate international trade, promote high employment and sustainable economic growth, and reduce poverty around the world".

Tanzania ni mwanachama wa IMF na ndio maana tumekuwa tumapata mikopo huko. CHADEMA hata CCM au chama kingine chochote hakiwezi kuwa mwanachama wa IMF hata kama wangetaka iwe hivyo.

Nirudi kwenye point yangu ya msingi, Ndugu yangu GeniusBrain hoja yako si tu ni aibu kwako binafsi bali pia inatuibisha watanzania wote (milioni 42 na ushee), kwamba, hatujui maudhui na kazi za taasisi za kimataifa kama IMF. Na mbaya zaidi hatujui hata vyama vya siasa ndani ya mipaka ya nchi yetu vinanzishwaje.

Sijui ulikuwa unalenga nini hasa kwa kuanzisha hii hoja ila nadhani tuhimizane humu jamvini ili hii kasumba ya porojo, character assissination, mudslinging na cheap political scoring tactic zikome. Ni aibu mno kwetu sisi watanzania.

Mwisho ningekusihi sana ndugu yangu GeniusBrain na wengine wenye maoni kama yako watambue kuwa watanzania wana akili timamu na wana uwezo wa kutenganisha mema na mazuri. Maneno kama...chama fulani kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi' ni madharau kwa watanzania wenzako (insult to our intelligency).Tabia ya kikoloni hii.

Tutumie hili jukwaa kwa kuongelea mambo ya msingi na yenye tija tuache kuaniaka umbumbu wetu hadharani.

You are a great thinker, big up. Kuna watanzania wana uwezo wa kifikiri tuache porojo jamani. Kuna watu wanadhani akizungumza Mukama basi ndio ukweli. Tujaribu kusoma na kuwa critic tuzimeze kila kitu jamani. Hili Taifa haliwezi kukombolewa na watu wajinga
 
Kwa hiyo unasemaje?Chadema kifutwe?,sbb Nia yako ndio hiyo.Acha umbea Leta sera zitakazotusaidia Kama vijana wenzio,unakuwa na mawazo mafupi Kama Avunuasi!!!!!!?
 
Lakini mimi naona ni kutokuwa tactical enough katika timing. Angesitisha mkutano huo au angeufanya Jumapili siku ambayo newsroom nyingi huwa ni kavu kuhusu news hivyo chochote huingizwa gazetini kwa ajili ya Jumatatu.

Hata hivyo it served them right! Hii kitu gamba (na kwa nini Jk alili-coin hilo neno) limewachanganya sana CCM -- kuna watu na akili zao wamegeuka wapumbavu kutokana na kukwepa kuzumgumzia suala hilo kwa uwazi kabisa.= -- wanakaa wanazunguka zunguka tu.
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :

  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk

Ok. Kama ndo hivyo safi kabisa. Tutakuwa tunaomba omba pesa kuliko kuomba omba net za mbu.
 
Back
Top Bottom