Mukama ameikejeli Katiba!

pole sana wewe sijui nani brain vile, walokutuma wamekukaanga, think twice and come again, CDM itazidi kuwashika sana tu, kama wanaoifadhili ni watu wa nje kama unavyodai basi wanawatakia mema watanzania!
 
GeniusDrain (sorry-GeniusBrain), nijibu hapa kwanza kabla sijaendelea; WOTE waliokosana na J.K.Nyerere (sio waliomkosea maana he is not an angel that always was right) wana laana? zingatia keywords;WOTE, WALIOKOSANA
 
Umesahau Kuwa Akina Mzee Mbowe na akina Mtei ndo walikuwa wakimlipia Nyerere nauli za Kwenda Uingereza Kudai Uhuru????
Mtu Kutofautiana Na Nyerere si Kukosa Adabu.....Kama ni Kukosa Adabu alikosa Mkapa na Kikwete ambao walivunja Misingi ya Azimio la Arusha alilolisimamia Nyerere na wao wakaanza kufanya Biashara wakiwa Ikulu na Kutetea Mafisadi

Mwalimu alikuwa very very visionary leader, kwa upeo wa Mtei asingeweza kumfikia mwalimu hata robo. Mzee Mtei alitaka kumzunguka mwalimu kwa kumpa ushauri ambao kuikweli nia yake ilikuwa ni kujinufaisha yeye mwenyewe
 
pole sana wewe sijui nani brain vile, walokutuma wamekukaanga, think twice and come again, CDM itazidi kuwashika sana tu, kama wanaoifadhili ni watu wa nje kama unavyodai basi wanawatakia mema watanzania!

Tunashukuru kwa ku confirm juu ya hilo kuwa nyie si chama cha siasa, bali ni vibaraka wa watu wa nje ! tunazidi wa tz kuwafahamu sura yenu halisi siku hadi siku
 
CDM itazidi kusonga mbele mtajitahdi kugundua mbinu za kukidhoofisha lakini mtaishia kupewa majibu na ma great thinkers.
 
Jibu hoja acha bla bla ! sio ya kweli hayo

Watakuona huna akili,coz agenda nzima ya uanzishwaji vyama vingi nchini ilikua ya IMF,unakitajaje chama kimoja kwamba kilianzishwa na IMF,au hujui kama pia Re-structuring ya miaka ya themanini pia ilikua requirement ya IMF,na ikatekelezwa na CCM!
 
CDM itazidi kusonga mbele mtajitahdi kugundua mbinu za kukidhoofisha lakini mtaishia kupewa majibu na ma great thinkers.

Si unaona watoa jibu jepesi kwa hoja nzito. Tunashukuru kwa kukubaliana na thread yenyewe
 
Watakuona huna akili,coz agenda nzima ya uanzishwaji vyama vingi nchini ilikua ya IMF,unakitajaje chama kimoja kwamba kilianzishwa na IMF,au hujui kama pia Re-structuring ya miaka ya themanini pia ilikua requirement ya IMF,na ikatekelezwa na CCM!

Na huu ufadhili wa maandamano kumbe pesa mwapata IMF , tunashukuru kwa kutujuza hivyo
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama


My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk

jf hatujadili hoja za kusikia.

leta hoja na supporting data.
 
Who is Nyerere by the way mpaka watu wote lazima wakubaliane na mawazo yake?mbona wengi walishampinga hadharani na alikuwa anawapa ubalozi ili wawe nje ya nchi na wasishughulike na siasa za ndani?naye ni mtu ambaye alikuwa na haki ya kuwa challenged,

Twende kwenye hoja Mzee Mtei walitofautiana na Nyerere kuhusu kushusha thamani ya shilling na yeye km waziri wa fedha/gavan akagoma mbona mwaka jana China wametakiwa kushusha thamani ya fedha yao nao wakagoma na wao ni wa soshalisti?

Mara baada ya kutofautiana Mtei alifanya nini?aliiandika barua ya kujiuzulu na sio kung'ang'ania madaraka na kutekeleza sera usizo ziamini, leo viongozi wangapi wa CCM wanatekeleza yale wasio ya amini?Mfumo wa vyama vingi vilipoanzshwa zaidi ya miaka 15 toka Mtei kujiuzulu akaanzisha CDM ili apate fursa ya kutekeleza yale aliyo ya amini.

1995 Mrema alipokuwa juu Nyerere alisema msitishike nae huyo bali kuweni Makini na kina Mtei ndio tishio kwa CCM na hiyo ni 1995 ambapo wachahce waliifahamu na kuijua CDM, wengi walimwamini Mrema na NCCR lakini kwa Nyerere CDM ilibaki tishio kwake
 
Mkuu huu ukibaraka wa IMF unaendeleaje ? kumbe kuna bwana nje anawalisha, na kuwavisha !


CDM,CUF,NCCR wakiwa ni vibaraka wa yeyote yule, tunachotaka ni siasa na demokrasia ya ukweli..

hakuna kitu kinachonikera kama mbinu na mikakati ya kuua vyama pinzani. Huu ni mpango mbaya kabisa, kwani siku CDM na vyama vingine vitakapokufa ndo itakuwa tumepata demokrasia ya kweli??

Demokrasia inahitaji kukuzwa ili kuwe na uwajibikaji wa kutosha kwa chama kilichopo madarakani. Ningefurahi kama vyama vya upinzani vingeendelea kupewa misaada ya kila hali ili vifanye shughuli, kuliko mipango ya sasa ya kuviteketeza ili CCM ibaki madarakani..Demokrasia haiendelei kwa kuvifanya vyama vingine vikose uhai..(haina maana)
 
Back
Top Bottom