Mukama ameikejeli Katiba!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Vyama vya upinzani vilianzishwa nchini Tanzania kwa mujibu wa sheria mwaka 1992.

Katibu mkuu wa CCM bw. Wilson Mukama anapotamka kwamba vyama vya upinzani vilianzishwa kwa shinikizo ana maana gani?

Akumbuke kwamba wanachama walioko kwenye vyama vya upinzani ni watanzania kama walioko ndani ya CCM.

Inawezekana pia CCM ikawa chama cha upinzani, na itakapotokea ikawa hivyo CCM nayo itakuwepo kwa shinikizo kutoka nje ya nchi?
 
Laiti Mukama angejuea kuwa Osama angekufa jana yake ange-cancel hafla aliyowaandalia wahariri pale Krmpiski jana Jumatatu na kutoa pumba zake. Leo hii magazeti yoote, ni habari za Osama tu katika lead story zao, isipokuwa HABARI LEO tu ndiyo imetoa kipaumbele pumba za Mukama pale Kempiski kwa kuzifanya lead story.
Na hivyo hivyo kwa habari za Ris-One katika kuukana ubilionea wake.
Hii safi sana Wahariri wa magazeti – Big Up! Tuko pamoja!
 
Ni kweli, vyama vingi vilianzishwa kwa shinikizo, na kutokana na shinikizo hilo CCM waliamua kukubali shingo-upande na kuanzisha upinzani feki wa akina Mrema na Cheyo ambao leo hii tunashuhudia mmoja mmoja wanarudi walikotoka (CCM).

Ukimsikiliza Mrema au Cheyo leo hii unashindwa kuelewa kama kweli ni wapinzani au ni wanaCCM wanaojifanya wapinzani. Lipumba naye vilevile, isipokuwa nguvu ya CUF zanzibar inamlazimisha aonekane kama mpinzani wa kweli, lakini ukweli ni kuwa Lipumba, Cheyo na Mrema si wapinzani. Ni mapandikizi ya CCM ambayo sasa yanazikwa na kufukiwa na Chadema.
 
Lakini Tvs jana jioni zimempa muda mwingi bila sababu. Huyu baba wala sio mwanasiasa. Angekaa tu ofisini amwache Nape aendelee kubwabwaja. Mbona Richard Tambwe HIza haonekani tena? Au haikuwa ajira ile!
 
Laiti Mukama angejuea kuwa Osama angekufa jana yake ange-cancel hafla aliyowaandalia wahariri pale Krmpiski jana Jumatatu na kutoa pumba zake. Leo hii magazeti yoote, ni habari za Osama tu katika lead story zao, isipokuwa HABARI LEO tu ndiyo imetoa kipaumbele pumba za Mukama pale Kempiski kwa kuzifanya lead story.
Na hivyo hivyo kwa habari za Ris-One katika kuukana ubilionea wake.
Hii safi sana Wahariri wa magazeti – Big Up! Tuko pamoja!

Nasema kwa kinywa changu Bora Magamba/Makamba na sio Mukama!!!Mukama is not a political material he sounds as civil servant.atafutiwe kazi nyingine,ukinibishia we kilaza!!!!???
 
teeh teeh nadhani hizo ni salamu tosha kwa CCM na inathibitisha wanashidwa kusoma alama za nyakati
 
Kwa nini serikali ya ccm ilikubali shinikizo la imf? Kama kingekuwa chama makini na chenye msimamo si kingepinga shinikizo la imf na kuendelea kusimamia msimamo wake wa kuwa na chama kimoja. Mkama hana tofauti sana na makamba maa naye anakatabia ka kuropoka bila kufikiri. Kama serikali ingekuwa na uwezo wa kutatua matatizo yake yenyewe ingekataa shinikizo. Zaidi ya hapo kuna mambo mengi hapa nchini yameanzishwa kile mukama anachoita shinikizo. Eg. Cost sharing, privatization n.k.
 
Nimemuona kwa tv jana, nadhani CCM watambue kuwa huyu Mukama basi ni tatizo lingine pengine kubwa kuliko Makamba. Maana uropokaji wake au kutoa hoja ya siasa hiyo jana imenipa kutambua kuwa ni mtu wa kukurupuka kama Makamba. Sasa hajui kwa kutoa hicho kihoja kuwa upinzani umeanzishwa na shinikizo la watu wa nje ni kukuiaibisha chama chake sababu ndo kilipitisha hizo hoja.

Mi nadhan anahitaji kuwa makini kwenye kutoa toa matamko ya kusema vyama vingine yasiyo na misingi yoyote ya mantiki, kama CCM inataka kujikita kwenye kurudisha adhi yake basi sasa ni muda muafaka washughulikie hao mafisadi kwa vitendo then watoe takwimu za mara kwa mara kuhusu utekelezaji wao wa ilani. Hayo maneno maneno ya TAARAB waliyorisishwa NA Makamba na mwenyekiti wao yatazidi kuwaponza tu na kuonekana wasanii zaidi.

Message sent!!
 
Vyama vya upinzani vilianzishwa nchini Tanzania kwa mujibu wa sheria mwaka 1992.

Katibu mkuu wa CCM bw. Wilson Mukama anapotamka kwamba vyama vya upinzani vilianzishwa kwa shinikizo ana maana gani?

Akumbuke kwamba wanachama walioko kwenye vyama vya upinzani ni watanzania kama walioko ndani ya CCM.

Inawezekana pia CCM ikawa chama cha upinzani, na itakapotokea ikawa hivyo CCM nayo itakuwepo kwa shinikizo kutoka nje ya nchi?

Ndugu zangu kama kweli kasema hivyo, basi amefichua udhaifu wa CCM kwamba chama ambacho mtu mwenye fedha au taasisi ndiye anasikilizwa; 'mkono mtupu haulambwi', kwamba chama badala ya kuwa cha wakulima na wafanyakazi kinawasikiliza wenye fedha kama IMF. Kumbe hata kinapojigamba kupigana na ufisadi ni geresha tu maana wenye fedha ndiyo wanaoamua nini kifanyike katika chama na hata ndani ya Serikali. Hongera mukama kwa kuongea ukweli na uhalisia wa kinachoongoza maamuzi ya CCM, hicho ni chama kinachojigamba kuzaliwa kutokana na vyama vilivyopigania uhuru na mapinduzi matukufu lengo likwa kurudisha nchi mikononi mwa wananchi ambapo waliowengi ni masikini, wakaanzisha na mashina ili kuonekana kuwa karibu na wananchi kumbe ilikuwa danganya toto wenye fedha ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. Waakajisumbua kuitishwa kura ya maoni kujua matakwa ya 'wananchi' kumbe walikuwa wanasubiri maamuzi ya IMF na rasilimali za taifa zikatumika huku wakijua mwamuzi ni IMF loo!! Hiki ndicho chama kinachotaka kuondoa umasikini kwa wananchi wa Tanzania kwa kutumia mashinikizo ya walionancho, hivi kuna tajiri anayetaka masikini atajirike, hakuna hata siku moja mbapo masharti ya IMF yakafanikiwa kuondoa umasikini kwa walio wengi bali ni kukusanya utajiri mdogo walionao wengi na kuwapa wachache. Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba matakwa yao, mahitaji yao, maoni yao kamwe hayatasikilizwa kwa kuwa wanaosikilizwa ni wale wenye nacho.
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk
 
Hahahahahahah ukistaajabu ya Mussa!.....Na CCM ni chama cha nani vile!?
 
'………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha'.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :

  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk

Umesahau Kuwa Akina Mzee Mbowe na akina Mtei ndo walikuwa wakimlipia Nyerere nauli za Kwenda Uingereza Kudai Uhuru????
Mtu Kutofautiana Na Nyerere si Kukosa Adabu.....Kama ni Kukosa Adabu alikosa Mkapa na Kikwete ambao walivunja Misingi ya Azimio la Arusha alilolisimamia Nyerere na wao wakaanza kufanya Biashara wakiwa Ikulu na Kutetea Mafisadi
 
Back
Top Bottom