Mukama amdanganya Kikwete kuhusu umiliki wa JF, wamiliki wa JF hawa hapa

Status
Not open for further replies.
kheee sasa JF imeingia mpka kwenye ripotu ya kushindwa kwa JK kwenye uchaguzi???? uwiiii kazi ipo mwaka huu...
 
Swali ni moja mbona nguvu kubwa sana inatumika kukana kumilikiwa na CDM? Kwani CDM ni tusi? Shame Kubenea leo anatuambia ukweli kuhusu JF unapatikana kwenye makaratasi ya BRELA huku akiendelea kumbana Rostam kuwa ni mmiliki wa Dowans wakati makaratasi hayo ya BRELA hayana jina la Rostam, sijui hii ni triple standard au ni kupenda kutumia ujinga wa wana JF.

Lakini hujkumu ya ICC imemvua nguo RA kabisa kwamba ni mhusika mkubwa na ndiye atakayenufaika iwapo ile tozo dhidi ya Tanesco italipwa -- majina yaliyowekwa Brela ni ya front men wake. Isitoshe JF hainuki ufisadi kama Riuchmond-Dowans.
 
ccm wana majibu rahisi sana. wanasema jf ni ya vijana wa chadema. ukweli ni kwamba vijana wengi wasomi wanapenda mabadiliko hivyo wapo chadema. mawazo mengi hapa ndani ni ya kimapinduzi na hivyo ccm kwa urahisi wa kufikiri wanadhani jf ni ya chadema. suluhisho lao wameamua kuwaajiri vijana wanashinda humu kuvuruga mawazo mazuri ili ionekane ccm wana watu pia. kweli ccm wameishiwa.
 
Dunia ya vijana wa sasa na Teknohama inawatoa jasho wazee gunguri wa utafunaji!
 
Si wamekuandikia kuwa Malecela ambaye ni CCM waziwazi na Steven Diallo ambaye ni ndugu yake Kigogo wa CCM wapo hapa ndani na wana-Share kwenye JF. Na Chadema walishindwa nini kuwatafuta watu wa kawaida na kuwapa share ya kuwa wenye JF hadi wakatafuta watu ambao wako karibu na CCM Vigogo?

Kama hilo ni kweli, basi CCM badala ya kupeleka MAMLUKI CDM, wao ndiyo sasa wameingiliwa mlango wa pembeni ya nyumba.

Pia mtu kama Hamis Kigwangala ambaye ni Mbunge wa Nzega, yupo hapa kwa jina lake waziwazi na picha yake akiwa kavaa Gamba la CCM. Sasa hapa usichoelewa ni nini wee THE LORD OF THE RINGS??
 
hawa watu sio makini hata kidogo......mbona mimi wamenisahau wamenisahau wakati ni mmliki wa JF ??na hata simu hawajanipigia,lol...!!
 
Jesuit,

Vipi Mkuu? Kubenea alitembeza ubabe wake kwa Mwanamke gani aliye karibu na wewe?

Naona unamchukia sana tu bila kuwa na ushahudi wowote.

Ukiona Mwanaume anabwabwaja ovyo basi ujuwe ni vitu vitatu tu: Sex, Power and Money.

Nafahamu kuwa Kubenea huwa kuna mambo anachemka na kuonekana kama Mpuuzi fulani hivi lakini huwa ana malengo yake. Mfano aliposema Mtanzania au Mwakalinga ni Mwanafunzi wakati jamaa kamaliza shule zaidi ya miaka 10 huko nyuma na kumwita KIJANA wakati jamaa kashavuta miaka 40.

Pamoja na mapungufu yake, huwezi kumwita MJINGA. Hii inaanza kunipa imani kabisa kuwa na wewe unaweza kuwa moja ya wale watu waliohusika kumwagia ACID/Tindikali na kisa KAWAMEGEA. Pole sana Mkuu kama ntakuwa nimekutonesha kidonda cha ..............

Hii habari ni nzuri sana. Kumbe Mtani wangu Malecela WIlliam ni Chadema la NGUVU? Ni Vuvuzela la Slaa kama wengine wanavyosema? Sasa hili TAWI la CCM hapo NY ni Chadema au CCM? Au yeye ni Kibaraka aliyetumwa na Slaa/CDM kuja kuivuruga CCM huko majuu?

Ukweli ni mmoja, Dr. Slaa kweli ni Vuvuzela na tangu ameanza kupiga honi (piii Piiii) CCM hawaelewani.....

Dr Slaa, umewashika pabaya, hebu ongeza LIST zaidi ili waanze kutoboana macho.

- Mkuu heshima yako sana, mbona kwa kawaida tunaheshimiana sana sasa vipi tena mbona unaenda nje ya mstari, I mean hii habari inajaribu sana kuondoa hisia kwamba huu ni mtandao wa Chadema, sasa kwa nini usiheshimu hoja ya msingi badala yake unataka kuanzisha mapya ambayo huwezi kuyathibitisha!

- I mean Great Thinkers tuwe tunaongea kisayansi zaidi kuliko kimtaani mtaani, kwani sheria ya Jamhuri inasema nini kuhusu umilikaji wa mashirika kama hili la JF, na kama kuna sheria iliyovunjwa hapo ndipo kunaweza kua na ishu, I mean sisi wamiliki wote tuwe au tusiwe na affiliations zozote za kisiasa it does not matter, cha muhimu ni kama sheria imefuatwa katika kulianzisha na kulimiliki hili shirika, sasa kwa maneno hayo mekundu hunitendei haki, ungfanya ustaarabu kama hawa media ya Tanzania walionipigia majuzi na kuniuliza na wameripoti kama nilivyosema, hiyo ndio haki sio kunisngizia maneno bila kuwa na uhakika sio ustaarabu ndugu yangu!

- Binafsi I am proud to be one of the owners ni kilichonisukuma kushiriki umiliki ni kujali taifa langu zaidi kuliko anything, CCM niliwafahamisha mapema sana wakati tunaaanzisha hii kitu, kuhusu umuhimu wa hii kitu mbele ya safari na wao kuja hapa kujibu hoja officially, hawakunisikiliza mpaka majuzi tu nimewaonya sana kwamba wabunge wote wapya wa Chadema wanatoka kwenye huu mtandao na wao wajitahidi kuja hapa, nikawapa mfano wa Obama Rais wa Dunia, ambaye naye anashiriki kwenye mitandao, sasa ndio wameamka ninawakaribisha sana, lakini tusitafutane uchawi kwa sababu wao sasa ndio wameamka!

- I am a CCM member na very independent member na human being, na majuzi nimewaambia tena CCM kwamba wamechelewa sana kuja hapa sasa hivi sio rahisi ku-catch up na kasi ya Wapinzani hapa, mengi wanaoshauriwa hapa ni ukweli mtupu na wa wazi ambao hauwezi kupingwa cha muhimu ni CCM kurekebisha uozo ambao umekua mwingi sana katika chama chetu na sio kutafutana nani mchawi anayemiliki huu mtandao, cha muhimu ni kusoma hoja hapa bila kujali imetolewa na nani wala JF inamilikiwa na nani. Mimi siogopi anything ndio maana the media waliponihoji majuzi sikuficha anything, mimi siku zote ni muwazi na nitaendelea kuwa hivyo hivyo, ndio maana nimesema wazi kwamba ninajitayarisha kufungua tawi la CCM New York City na sio DC Washington, ni kwasbabu moja tu ya kuona CCM wamenuia kujivua gamba. Sijatumwa na mtu wala kumiliki huu mtandao sijatumwa na yoyote na siamini kwa 100% kwamba huu ni mtandao wa chama chochote cha siasa Tanzania, huu ni wakati wa CCM kuanza kuangalia wamefikaje mpaka kuwa na magamba, I mean ukiangalia historia ya huu mtandao utagundua kwamba mimi na Mkuu sana wa Dunia Mwanakijiji at onetime tulikua ndio watetezi wakubwa wa CCM hapa, sasa leo MMJ ni bingwa wa Dunia wa kuikosoa CCM, unawakuta wanashangaa ni kwa sababu wengi hawana historia, sasa swali ni kwa nini watu muhimu kama kina MMJ walitutosa CCM na kuanza kutukosoa kwa nguvu ya ajabu na kukubalika na Dunia nzima? Ni makosa yetu wenyewe CCM, sasa tusitafutane uchawi wa nani mmiliki nani hamiliki, tujali hoja za wananchi hapa na kujirekebisha.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA WANANCHI WAKE!

William @ NYC, USA.

-Otherwise,
 
Maelezo ya Wiliam Malecela yamenitosheleza, na yamekata kiu yangu yote niliyokuwa nayo. sihitaji tena ufafanuzi wa INVISIBLE. iLA USHAURI WANGU KWA MALECELA JR NI HUU.
I value to differ, lakini kwa watu wa kariba yako nadhani hawatakiwi ndani ya ccm Tanzania, sifa kuu ya kuwa mwanaccm mwenye mafanikio hapa Tanzania basi ni lazima uwe mnafki, mtu wa majungu, kujipendekeza ili upendekezwe, ushirikina na kila aina ya uozo. kama hauna Great mision inayokufanya uendelee kuisupport ccm nadhani unapaswa kujifikiria mara mbilimbili kukiunga mkono chama ambacho kinaendesha siasa za kuviziana. tukitaka kupata maana halisi ya gamba ndani ya ccm hii hakuna msafi hata mmoja.
 
Malecela,

Nimeandika kwa KINYUME na ukitulia vizuri utanielewa. Ukisoma haraka haraka utapata maana hiyo hapo juu ila maana hasa iko ndani zaidi. Nimekuwa nikiandika kwa aina hiyo mara nyingi na nilijua utanielewa na ndiyo maana hata nikaweka neno MTANI. Mengine yote uliyoandika chini ndiyo haswaa ambayo nilikuwa nikimaanisha........

Sikujua na wewe ni mmoja ya Wadhamini wa JF. Inabidi niseme wazi kuwa HONGERA kwa hilo.

Msimamo wako umekuwa ukijulikana hapa kwa sisi wenyeji. Umepigana vita na ufisadi kwa miaka mingi na huku ukiwa bado unajitambulisha kama CCM. Hujajificha na kila kitu uliweka wazi na hii ulikuja kuandika kuwa ilikuletea matatizo (nina kumbuka). Sasa kwangu mie ilikuwa kichekesho nilipounganisha hizo factors mbili na kuja na jawabu kuwa "Kumbe mtani Willy ni CDM" according to Mkama/Msekwa.

Nitasikitika sana kama CDM siku moja ikishika hatamu na CCM ikafa maana tutaishia kuwa na CDM kama Chama kipya cha Magamba Tanzania. Ingelikuwa heri CDM na CCM wagawane bunge nusu kwa nusu na hapo ndiyo msuguano wa kweli bungeni utakuwa. Kila la kheri katika kuhakikisha CCM haifi kifo cha Mende kama akina KANU.
 
- Mkuu uko sawa sawa, maneno yako yananikumbusha sana maneno ya mheshimiwa Shibuda, mwaka jana wakati wa Bajeti, nilienda kuhudhuria bunge Dodoma, nikafanya sana mazungumzo naye na hayo uliyoyasema ni baadhi ya usia alionipa, baada ya kumsikia Spika wa bunge Mzee Sita akiniomba sana nichukue fomu ya ubunge wa Mtera.

- HOWEVER: As much as I have a problem na some of CCMs ideas na baadhi ya viongozi wake wabovu, badio sijaweza kushawishika na chama chochote cha siasa nje ya wao, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema wa sasa ni rafiki yangu wa karibu sana toka utotoni, tumekaa chini na kuongea sana hizi ishus kwa wakati mbali mbali, I respect the man kwa sababui sijawahi kuona aki-betray his beliefs kuhusu what needs to be done kuhusu Tanzania, lakini bado sijawa convinced on the alternative bado nina imani na CCM kwamba soon tutakwua tunaelekea kunakotakiwa. Chadema are doing a hell of a job na ndio hasa sababu ya CCM kufikia kujivua, lakini naomba niwe mkweli siwaamini viongozi wengi wa Chadema, ambao ninawajua sana kwa karibu sana, ingawa pia siwaamini viongozi wengi wa CCM pia, lakini nina imani kubwa sana sasa hivi na viongozi wapya, hasa Nape na Januari, I mean ninasikitika pia kwamba it has to come to watoto wa viongozi, waliolifikisha taifa lilipo sasa, lakini it what we have, ninaamini kwa imani kubwa sana kwamba hawa ndio the future ya CCM na kwamba soon tutawaondoa wale wote walioshiriki kutufikisha taifa hapa na kuendelea na vijana wenye mawazo mapya. Na ni matumaini yangu kwamba wale wote wenye matatizo ya kisheria tutawafikisha kwenye sheria.

- Otherwise, ninakushukuru sana mkuu kwa mawazo yako, sio kwamba ninayanfumbia masikio no ninayaweka kama akiba ya mbele ya safari, bado ninarudia tena kwamba Mwaka 2005 wakati tuna fanya transition ya kutoka BCS ambako pia nilikuwa mmiliki, na kuwa Jamboforums niliwaonya sana CCM, kwamba huuu mtandao kuna siku utakuja kuwapa taabu sana kama hawakuwahi kujiunga hapa na kujibu hoja nyingi, najua tu kuna kiongozi mmoja tu aliyetuma mtu wake ambaye he was doing a hell of ajob ya kumsafisha hapa, infact he was way ahead of the game here at one point, mpaka ilipokuja Richimonduli ikammaliza na yule bwana sikumuona tena.

- Mkuu ninashukuru sana kwa ushuari wako na samahani sana kwa maelezo marefu sana.

William @ NYC, USA.
 
Dr plus naye awe anachanganya ya kuambiwa na akili zake....kwa PHD zote tatu kwanini asifanye walau utafiti mdogo wa kupima watendaji wake na aina ya taarifa wanazompa?
 
Malecela,

Nimeandika kwa KINYUME na ukitulia vizuri utanielewa. Ukisoma haraka haraka utapata maana hiyo hapo juu ila maana hasa iko ndani zaidi. Nimekuwa nikiandika kwa aina hiyo mara nyingi na nilijua utanielewa na ndiyo maana hata nikaweka neno MTANI. Mengine yote uliyoandika chini ndiyo haswaa ambayo nilikuwa nikimaanisha........

Sikujua na wewe ni mmoja ya Wadhamini wa JF. Inabidi niseme wazi kuwa HONGERA kwa hilo.

Msimamo wako umekuwa ukijulikana hapa kwa sisi wenyeji. Umepigana vita na ufisadi kwa miaka mingi na huku ukiwa bado unajitambulisha kama CCM. Hujajificha na kila kitu uliweka wazi na hii ulikuja kuandika kuwa ilikuletea matatizo (nina kumbuka). Sasa kwangu mie ilikuwa kichekesho nilipounganisha hizo factors mbili na kuja na jawabu kuwa "Kumbe mtani Willy ni CDM" according to Mkama/Msekwa.

Nitasikitika sana kama CDM siku moja ikishika hatamu na CCM ikafa maana tutaishia kuwa na CDM kama Chama kipya cha Magamba Tanzania. Ingelikuwa heri CDM na CCM wagawane bunge nusu kwa nusu na hapo ndiyo msuguano wa kweli bungeni utakuwa. Kila la kheri katika kuhakikisha CCM haifi kifo cha Mende kama akina KANU.

- Ahsante sana ndugu yangu, I mean wewe tunatoka mbaali sana na this game, na ninakuheshimu sana na samahani sana kama sikukuelewa niwie radhi sana, otherwise I mean Media waliponipigia simu majuzi they were very upfront kwamba waliowatuma kunipigia wamewaambia in advance kwamba kwangu watapa ukweli mtupu, and I did na kuwambia ukweli mtupu kama kawaida yangu hapa JF. Well, sikuitaka sana hii bragging right ya umiliiki wa hapa kuwa in public, lakini ninaamini kwenye maisha kila kitu hutokea kwa sababu, rohoni nina amani sana kuona utabiri wangu umekua kama nilivyotabiri 2005, nilimwambia wazi Waziri Sophia Simba kwamba kama CCM hawakuja hapa mapema, siku moja huuu mtandao utawatesa sana na watalia kama watoto wadogo, exactly what is happening now! and I am proud of that!

- Sasa cha muhimu ni sisi wote wananchi washiriki wa huu mtandao, kuulinda kwa nguvu zetu zote ili usiharibiwe na wapuuzi wachache ambao sio siri naona wamekua wengi sana siku hizi, tuwaelimishe ili waondokane na siasa za utumwa na again jamani tuuulinde sana huu matandao maana sasa umekua ni tatizo sana kwa watawala wetu wasiotaka kubadilika na wakati!

Mungu Aibariki Tanzania na Aibariki JF!

William @ NYC, USA.
 
Hapa kwenye RED nimepapenda sana sana......

Inanikumbusha Wimbo wa zamani watoto wakiimba "Bwana Hamisi, mtu wa Tanga, muulizeni akija, kaupataje Mbeleko".

YES, CCM waulizwe/wajiulize, Wameyapataje Magamba?
....... Sijatumwa na mtu wala kumiliki huu mtandao sijatumwa na yoyote na siamini kwa 100% kwamba huu ni mtandao wa chama chochote cha siasa Tanzania, huu ni wakati wa CCM kuanza kuangalia wamefikaje mpaka kuwa na magamba, I mean ukiangalia historia ya huu mtandao utagundua kwamba mimi na Mkuu sana wa Dunia Mwanakijiji at onetime tulikua ndio watetezi wakubwa wa CCM hapa, sasa leo MMJ ni bingwa wa Dunia wa kuikosoa CCM, unawakuta wanashangaa ni kwa sababu wengi hawana historia, sasa swali ni kwa nini watu muhimu kama kina MMJ walitutosa CCM na kuanza kutukosoa kwa nguvu ya ajabu na kukubalika na Dunia nzima? Ni makosa yetu wenyewe CCM, sasa tusitafutane uchawi wa nani mmiliki nani hamiliki, tujali hoja za wananchi hapa na kujirekebisha.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA WANANCHI WAKE!

William @ NYC, USA.

-Otherwise,
 
- Mkuu heshima yako sana, mbona kwa kawaida tunaheshimiana sana sasa vipi tena mbona unaenda nje ya mstari, I mean hii habari inajaribu sana kuondoa hisia kwamba huu ni mtandao wa Chadema, sasa kwa nini usiheshimu hoja ya msingi badala yake unataka kuanzisha mapya ambayo huwezi kuyathibitisha!

- I mean Great Thinkers tuwe tunaongea kisayansi zaidi kuliko kimtaani mtaani, kwani sheria ya Jamhuri inasema nini kuhusu umilikaji wa mashirika kama hili la JF, na kama kuna sheria iliyovunjwa hapo ndipo kunaweza kua na ishu, I mean sisi wamiliki wote tuwe au tusiwe na affiliations zozote za kisiasa it does not matter, cha muhimu ni kama sheria imefuatwa katika kulianzisha na kulimiliki hili shirika, sasa kwa maneno hayo mekundu hunitendei haki, ungfanya ustaarabu kama hawa media ya Tanzania walionipigia majuzi na kuniuliza na wameripoti kama nilivyosema, hiyo ndio haki sio kunisngizia maneno bila kuwa na uhakika sio ustaarabu ndugu yangu!

- Binafsi I am proud to be one of the owners ni kilichonisukuma kushiriki umiliki ni kujali taifa langu zaidi kuliko anything, CCM niliwafahamisha mapema sana wakati tunaaanzisha hii kitu, kuhusu umuhimu wa hii kitu mbele ya safari na wao kuja hapa kujibu hoja officially, hawakunisikiliza mpaka majuzi tu nimewaonya sana kwamba wabunge wote wapya wa Chadema wanatoka kwenye huu mtandao na wao wajitahidi kuja hapa, nikawapa mfano wa Obama Rais wa Dunia, ambaye naye anashiriki kwenye mitandao, sasa ndio wameamka ninawakaribisha sana, lakini tusitafutane uchawi kwa sababu wao sasa ndio wameamka!

- I am a CCM member na very independent member na human being, na majuzi nimewaambia tena CCM kwamba wamechelewa sana kuja hapa sasa hivi sio rahisi ku-catch up na kasi ya Wapinzani hapa, mengi wanaoshauriwa hapa ni ukweli mtupu na wa wazi ambao hauwezi kupingwa cha muhimu ni CCM kurekebisha uozo ambao umekua mwingi sana katika chama chetu na sio kutafutana nani mchawi anayemiliki huu mtandao, cha muhimu ni kusoma hoja hapa bila kujali imetolewa na nani wala JF inamilikiwa na nani. Mimi siogopi anything ndio maana the media waliponihoji majuzi sikuficha anything, mimi siku zote ni muwazi na nitaendelea kuwa hivyo hivyo, ndio maana nimesema wazi kwamba ninajitayarisha kufungua tawi la CCM New York City na sio DC Washington, ni kwasbabu moja tu ya kuona CCM wamenuia kujivua gamba. Sijatumwa na mtu wala kumiliki huu mtandao sijatumwa na yoyote na siamini kwa 100% kwamba huu ni mtandao wa chama chochote cha siasa Tanzania, huu ni wakati wa CCM kuanza kuangalia wamefikaje mpaka kuwa na magamba, I mean ukiangalia historia ya huu mtandao utagundua kwamba mimi na Mkuu sana wa Dunia Mwanakijiji at onetime tulikua ndio watetezi wakubwa wa CCM hapa, sasa leo MMJ ni bingwa wa Dunia wa kuikosoa CCM, unawakuta wanashangaa ni kwa sababu wengi hawana historia, sasa swali ni kwa nini watu muhimu kama kina MMJ walitutosa CCM na kuanza kutukosoa kwa nguvu ya ajabu na kukubalika na Dunia nzima? Ni makosa yetu wenyewe CCM, sasa tusitafutane uchawi wa nani mmiliki nani hamiliki, tujali hoja za wananchi hapa na kujirekebisha.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA WANANCHI WAKE!

William @ NYC, USA.

-Otherwise,
William kutokana na haya maelezo yako uliyoyatoa hapa baada ya kumjibu sikonge , haihitaji mtu kuwa na PHD kujua upeo wako, wewe jamaa nakupa big up sana , haya maelezo yamejitosheleza na ushauri mzuri sana umewapa hawa CCM sasa hivi naona wamepoteana njia huku wakiwa wamesahau kuwa ulishawapa taarifa kama hii, lakini ndugu yangu wewe hujui kuwa wafuasi wengi wa ccm ni wale wenzangu na mimi wa ndio mzee? % kubwa ya wafuasi wao wapo vijijini, na huo ndio mtaji wao, na hizi shule za kata zinazoibukia ndio kifo chao believe me, nakuhakikishia itafika wakati chama chenu kitapotea kabisaaa kwa sababu kila anayeelimika anakimbia ,na anayebaki ndani ya ccm ujue ana maslahi fulani(hapa sikuongelei wewe) nawaongelea vijana wengi ambao ndio wameajiriwa tu na sasa hivi wanatumia masaa manne au matano kwenda kazini kutokana na foleni,sasa huyu kijana utamwambia aje hapa JF kuitetea ccm akuelewe? kama mimi nikija hapa kuipigia debe then jioni nikiondoka kwenda nyumbani nakaa barabarani kwa mda wa masaa 4 na joto zaidi ya nyuzi 30 , mimi si nitakuwa taahira? kwa hiyo ndugu yangu ccm huu moto wameuwasha wenyewe na jinsi tunavyozidi kwenda mbele na jinsi vijana wengi wanavyozidi kupata elimu ndio ccm nayo itazidi kupotea na kudidimia , kinachotakiwa ni kuwasikiliza wananchi from the botom thats all, na kuwawajibisha watu thats all, mtu akifanya masikhara kazini anapigwa chini ,thats all
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom