Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
"Tangu tulipoachana rafiki yangu mwaka ule tukijifunza sanaa ya michoro pale Itigi RC misheni ulikuwa mdogo sana. Sasa umekua mtu mzima hata mimi naonekana mdogo kwako. Mbona unazeeka mapema hali ya kuwa kila kitu kinapatikana katika nchi yenu? Nakumbuka tulipoachana ilikuwa mwaka 1987. Sikupata nafasi ya kuja tena katika nchi hii niliyokuwa naipenda sana. Sasa nimekuja mara hii kama mtalii. Nimepita maeneo mengi na kushudia nchi yenu ilivyo na mabadiliko pamoja na utajiri wa kutisha. Pori na vichaka pekee bila shaka ni utajiri wa kutosha. Naambiwa nchi hii ni kati ya zile zinazoshikilia nafasi za juu kwa umasikini duniani, siamini hata kidogo..naitizama Somali, Ethiopia na nyingine nyingi. Nashindwa kuelewa maana ya umasikini huu. Jambo moja tu limenishangaza, pamoja na umasikini huo. Magari yote hapa Dar es salaam yanamilikiwa na nani? Majumba ya kifahari pia?" Jamaa anashangaa kama nchi ni masikini, mbona watu wake wanafanya kufuru ya anasa? Magari ya kifahari, starehe, watu wanakesha klabu usiku kucha. Hicho ndicho alichokiona huyu bwana. Ambacho kimenifanya nikae kimya, Je umasikini wa watanzania uko wapi? Je umasikini wa Tanzania uko wapi? Au kuna tabaka la wavivu wanaolia njaa na wachapakazi watendao anasa? Haya si maswali yangu, ni maswali ya Mike Bhusto. Mgeni kutoka Verona Italy.