Muingereza akamatwa uganda kwa ushoga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
120913190603_uganda_muingereza_ushoga_304x171_internet_nocredit.jpg



David Cecil katika mahakama ya Makindye


Msanii moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madia ya kuandaa na kuonyesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushuga.

Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi na kupuuza amri ya serikali. Polisi wanasema kuwa Muingereza huyo alionyesha mchezo huo

wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga marufuku kwa muda onyesho hilo.

Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil alionyesha mchezo huo kwa jina "The river and the mountain"

katika ukumbi wa Tilapia Cultural Center taraehe 17 Agosti na pia katika ukumbi mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.

Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza la Luzira hadi siku ya jumatatu ,Septemba 17 ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea.

CHANZO: BBC Swahili.
 
Waafrika wanaogopa sana ushoga..........in future hofu itawaondoka, its just a matter of time
 
Thread hii ilitakiwa iwe kwenye "Habari na matukio mchanganyiko", au vipi ?? na sio kwenye "Jamii photo" ??
 
Boflo, huyo rafiki yako adhabu yake inabidi akatwe dushelele maana haitumii kwa kazi yake iliyoumbiwa.
 
Last edited by a moderator:
Nimeshafika Mtukula nafunga mpaka, nazuia maovu kwa vitendo. Wapi kwingine nikafunge?
 
Back
Top Bottom