Muhogo mbichi wapoteza maisha ya mtoto

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTOTO Lawrence Gervas [4] amefariki dunia baada ya kumaliza kutafuna muhugo mbichi unaosadikiwa kuwa na sumu na watu wengine wawili kuugua kutokana na kutafuna mihogo hiyo.
Akitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Aprili 19, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni huko Kata ya Igoma, Wilayani Nyamagana.

Kamanda huyo amesema kuwa mtoto huyo alifariki, baada ya kutafuna mihogo mibichi waliyokuwa wakitafuta na wenzake.

Katika tukio hilo wengine wamenusurika na kifo hicho na wanaendelea na matibabu hospitali ya Bugando kutokana na kutafuna mihogo hiyo.

Gervas alifariki dunia wakati akikimbizwa katika hospitali ya Bugando.

Taarifa hiyo imendelea kusema kuwa, “Tayari mihogo hiyo tumeipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mwanza kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili pia kujua kiasi cha sumu iliyomo katika chakula hicho,” alisema Kamanda Komba.
 
duh..pipi za wachina zinatumaliza..mpaka hii mihogo ya shamba la bibi nayo ni kimeo...twende wapi sasa?
 
yaah watoto hawashibi majumbani mwao baadhi yao

Sijui kama ushawahi kulea.? Mtoto anaweza kutoka hom ameshiba, ukaenda nae ugenini akaanza kufakamia misosi kama hajala. Afu kipande cha muhogo mbichi hata watu wazima huwa tunakula kwa hamu...
 
ni kweli hiyo pia sio kulea tu nakumbuka hata mwenyewe yameshanitokea ni hamu tu inakuja autimatically

Yep, ni ajali kama ajali zingine. Hata sisi ni mungu hutuepusha men... Huwezi kuwa na uhakika wa usalama kwa kila unachotia mdomoni.
 
Back
Top Bottom