Muhingo Rweyemamu on Amina's Death

Na picha za BBC zaonyesha mchana au sio..na JK ndiye alifungua hizo sherehe!

Sasa wewe umesema mchana alikuwa huko Serengeti sijui akifungua kituo gani cha umeme, mara yuko Dar umepishana na msafara wake. Wewe tena umekuwepo wakati msafara ukienda kwa marehemu!... mkali sana kwa data mjomba nakuheshimu itabidi nianze kupitia kwako kila mara, maanake source ni wewe mwenyewe hudanganywi na mtu.
Poa vile vile! mshindi wewe!

Yes, timeline yangu iko consistent. JK alitua Serengeti akitokea Tanga late afternoon, June 26, akafungua mradi wa umeme Serengeti asubuhi ya June 27, akapata lunch Mugumu baada ya kufungua mradi wa umeme, then aka-fly Dar. Mitaa ya kumi, anatoka airport kwenda State House, tunasimamishwa Mandela Rd. Kumi na mbili unusu anaingia Kempenski kufanya shughuli ya BBC. Baada ya hapo, kwenye saa mbili usiku, anaelekea Mikocheni kwa Mzee Chifupa...mie nakata Ndovu baridi kwenye patio ya Milennium Towers. Kubali kaka.
 
Kama tunasema tunampenda Amina kwasababu alikuwa ni mkweli basi walau tusiseme uongo kwenye jambo linalomhusu. Ukweli unabakia palepale:

(i) Rais hakwenda kumuona Amina Lugalo siku aliyofariki, na (ii) Rais alikwenda kuhani baada ya sherehe ya BBC, sio akitokea airport au "akiwa njiani kutoka Ikulu kwenda Kempenski".

Heshima ya Forum na iwe mbele. Kama unataka tuendelee nalo hili, na tuendelee. Kama unataka tu-move on sasa kwenye mjadala wa maana wa nani anahusika na kifo cha Amina, basi na tufanye hivyo.
 
Haa imekuwa siku tena baada ya kufungua mradi yaani ina maana tarehe 28 alikuwa bado Mugumu?....Haya ama kweli tupo mjini Kiswahili lugha kubwa!
Sawa nimekubali naona hata lile la kuwa walisoma Albadr inabidi nianze kulitazama! maanake kasema mtu mwenye data!...
 
duh bob mkandara haifai hivyo

ndio umekula dongo ww kidume usikubali kuwa laini namna hivyo kama unaona jamaa hayuko right lete data zilizoenda shule kumpinga na yy aje kimtindo huo.

sasa ukikosolewa au kupingwa unavimba hapo no
 
Haa imekuwa siku tena baada ya kufungua mradi yaani ina maana tarehe 28 alikuwa bado Mugumu?....Haya ama kweli tupo mjini Kiswahili lugha kubwa!
Sawa nimekubali naona hata lile la kuwa walisoma Albadr inabidi nianze kulitazama! maanake kasema mtu mwenye data!...

Unataka kuendelea? Haya tuendelee. Unajichanganya sasa kaka. Wapi pameandikwa Rais alikuwa Mugumu June 28?
 
Haa imekuwa siku tena baada ya kufungua mradi yaani ina maana tarehe 28 alikuwa bado Mugumu?....Haya ama kweli tupo mjini Kiswahili lugha kubwa!
Sawa nimekubali naona hata lile la kuwa walisoma Albadr inabidi nianze kulitazama! maanake kasema mtu mwenye data!...

Komaa hivyo hivyo "babu ubishi" How can u easily be dethroned ur title? Kanyaga twende...
 
there is no substance-whatsoever in the latest postings in this thread! Evidence, evidence, evidence for trivialities....Let us move on lads.

We have a heap of important and unsolved issues........
 
Duh mara umesha badikisha!.. haya... kosa langu.

Mtumwitu,
Niseme mara ngapi? nasema sawa mimi MUONGO na mzushi wa story..... sii basi? nakubali zenu bado tu mnataka mimi nitoe source yangu ili iwe nini, maanake naona sasa imekuwa Mkandara ndio mada. Nilitoa ahadi kama ataweza kunipa source ya maelezo yake. Yeye amekazania TVT sijui google nipe link nipate hata kijimwanga! kisha naweza kujenga imani kuwa nilidanganywa! lakini sio huyu MugongoMugongo anayekuwepo ktk msafara wa JK kwa bahati za ajabu!
Mtu alonipa habari za JK kuwepo Lugalo ni mtu wa maana sana na namheshimu. kweli nimepata shida kulitoa jina lake hapa, hiyo sio uongo na mtu yeyote mwenye kufikiri ataelewa hivyo.
Nilitaka kuona ukweli wa huyu jamaa unaopingana na habari zile lakini hadi sasa nazipata toka mdomoni mwake. Ni habari ambazo siwezi kumwondolea heshima mtu wangu labda kama nitazipata toka kwa huyo mpiga picha wa rais kwa sababu alonambia alikuwepo wakati JK kaingia Lugalo.
Muda mfupi uliopita nilijaribu kupata time hasa alokuwepo pale lakini jamaa walikuwa kwenye tafrija.. hatukuweza kuongea ama mimi kuingiza issue hii.
 
Mkandara huna haja ya kutoa source yako ambayo unaiheshimu. Hata ukileta jina la "source" itakuwa useless kwasababu hakuna anayeweza kumtafuta. Sasa kama uliona source yako ni sensitive, mbona uliahidi kuitoa kama mimi ningetoa yangu. Mimi nimetoa sources zangu kwamba ni picha za TVT na ITV, Magazeti yote ya June 25, 26, 27, na 28, taarifa za habari za RTD, Mpiga Picha wa Rais (aliyekuwepo kwenye msafara wa Rais - tena na jina lake nimekupa kama unataka kumtafuta), zote zikithibitisha whereabouts za Rais kama nilivyozionyesha (in Tanga and Serengeti - siku Chifupa alipofariki). Sooner baada ya mimi kutoa sources zangu, unashindwa kutimiza ahadi yako kwa kusema your source is sensitive! Why did you promise in the first place? Didn't you know that?

Haya ya source tuyaache. Umeshindwa kujibu swali dogo sana nililokuuliza: JK aliingia mchana huo saa ngapi Lugalo hiyo June 27? Unaogopa kunipa muda kwasababu waweza nipa muda aliokuwa anahutubia Tanga?
 
Mzee Bob
Tuendelee na mada nyingine. Kuna mengi ya kuongelea.....Mimi binafsi bado nakuamini....maana nakufahamu toka siku nyingi.
 
Mzee Bob
Tuendelee na mada nyingine. Kuna mengi ya kuongelea.....Mimi binafsi bado nakuamini....maana nakufahamu toka siku nyingi.

Invincible,

Hata mimi hivyo hivyo. Nilikuwa namuamini huyu bwana kwasababu nimeanza kumsoma siku nyingi. Lakini katika hili, hapana. Anaongopa or, to be polite, kadanganywa.

By the way, this is funny. Why the rush ya kutaka kumaliza upesi upesi wakati credibility ya Forum is on the line?
 
Invincible,

By the way, this is funny. Why the rush ya kutaka kumaliza upesi upesi wakati credibility ya Forum is on the line?

Suala la credibility linaweza kuwa na utata......Wewe mwenyewe uliwahi kusema Mbowe anaandikiwa makala zake na Ngurumo. Na hukuleta evidence...Ngurumo mwenyewe akaja kukanusha....forum ikaendelea.

Pia majuzi umesema gazeti la TD wamepunguza uzalishaji kwa asilimia 50, bila evidence....forum inaendelea.....na watu wengi zaidi wanajiandikisha.

Kwa ujumla bado forum iko credible, pamoja na kwamba baadhi ya posts zinaonekana kuishusha hadhi...uongo na udaku.
 
I am happy unasoma michango yangu.

Look, habari ya Tanzania Daima kupunguza print order, nobody challenged asked me to bring "the evidence"...a couple of people only challenged whether a drop from 20,000 to 10,000 copies represents a 100% or 50% drop - and I conceded that Bush is smarter than me! Watu wa TD wamo humu, na ni wanachama wa JF, they should have brought up a different figure. Now you blame me because people didn't dispute my figures? Give me a break!

Ya Ngurumo kumuandikia Mbowe papers na makala, hiyo habari alileta mtu mmoja anaitwa Chinga...and it made sense to me knowing Mbowe's level of intellect. So, what did you expect Ngurumo to say? Kwamba ni kweli anamuandikia? Geez!

I find ridiculous hii idea kwamba tusi-challenge falsehood hapa JF kisa you may have unknowingly presented false information in the past.

And I find disturbing the comfort kwamba watu wanadanganya hapa JF na bado Forum ni credible. Well, up to a point.
 
Kama tunasema tunampenda Amina kwasababu alikuwa ni mkweli basi walau tusiseme uongo kwenye jambo linalomhusu. Ukweli unabakia palepale:

(i) Rais hakwenda kumuona Amina Lugalo siku aliyofariki, na (ii) Rais alikwenda kuhani baada ya sherehe ya BBC, sio akitokea airport au "akiwa njiani kutoka Ikulu kwenda Kempenski".

Heshima ya Forum na iwe mbele. Kama unataka tuendelee nalo hili, na tuendelee. Kama unataka tu-move on sasa kwenye mjadala wa maana wa nani anahusika na kifo cha Amina, basi na tufanye hivyo.

It is not a far fetched notion...."Kama unataka tu-move on sasa kwenye mjadala wa maana wa nani anahusika na kifo cha Amina."

From what I have seen here in this JF, I think it is possible to narrow down (credibly), the potential culprits.

Who casts the first stone:
1. Wazazi wa marehemu
2. Mme wa marehemu
3. Waliokuwa hawamtaki mema kisiasa(some names known)
4. Wenye biashara zao za madawa ya kulevya
5. Serikali ya Tanzania, na hasa viongozi hawa waliotishiwa maslahi yao
6. Wapenzi wa pembeni
7. Yeye mwenyewe kwa kujilipua
8. Marafiki zake waliomuonea gere kwa mafanikio aliyoyapata
9. Who else?
 
This is a much more useful exercise. Na tuanze. The dominant "theory" hapa JF ni kwamba Nchimbi kampa sumu.
 
Bellow is my evidence to this matter. Huwa napata news kutoka ikulu. so ukidownload picture, kwenye properties utaona picha imepigwa na camera gani na saa ngapi. so bellow is my evidence to the show SAGA
 
Here we start.. tunanza tarehe 22/07/2007

jk2th8.jpg

1.Kapteni ya timu ya netiboli ya ikulu Christina Mande akimkabidhi kombe Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati ya hafla ya kuzipongeza timu za ikulu zilizofanya vyema katika mashindano ya Mei Mosi na kuibuka washindi.Timu za ikulu zilinyakua vikombe katika michezo ya netiboli,riadha,kuvuta kamba na karata.sherehe hizo ziifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.

Date Picture Taken - 6/22/2007 2:21PM

jk3wg2.jpg

2.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bwana Fanuel Kuzilwa aliyekuwa mnikulu ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.Katika sherehe hizo Rais Kikwete alitoa vyeti kwa wafanyakazi wengine wa ikulu ambao pia wanastaafu na kutoa pia vyeti vya pongezi kwa wafanyakazi bora.Bwana Antony Itatiro ndiye aliyeteuliwa kuwa mnikulu mpya(Picha na Freddy Maro).

Date Picture Taken - 6/22/2007 2:26PM
 
Back
Top Bottom