Elections 2010 MUHIMU: Wamemvisha Mbuzi Suti Wanatuambia ni mtu - SIYO MTU

kingwipa1

JF-Expert Member
Jul 2, 2008
334
51
Wamemvisha mbuzi suti na kuwaambia watanzania kuwa huyo ni mtu, sis itunasema SIYO MTU.

Hakuna shaka kuwa watanzani wengi wenye mapenzi mema na nchi hii wamefuatilia kwa karibu sana pilika pilika za uchaguzi tangu kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura, kampeni, kupiga kura mpaka kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, lakini ushindi ninaoufahamu mimi ni ule utokanao la na fair play, yaani kuzingatia kanuni zoote za mchezo husika.
Uchaguzi wa Tanzania umekuwa na kanuni zisizojulikana ambapo kuna kanuni jambazi zinazotumika kumfanya aliyeshindwa kutangazwa mshindi.
Kwa wale walioshinda kihalali nawapa pongezi na wale walioshindwa kilahali nawapa pole ila nawaomba wasife moyo. Wanaoniudhi ni wale wanaojua fika kuwa wao hawakushinda uchaguzi lakini kwa hila na mabavu wameamua kujitangaza kuwa washindi. Hao ndio mbuzi wangu. Watu wenye uchu wa madaraka ambao kwao cheo sio dhamana bali ni kichaka cha kufanya uovu. Wana-matabasamu mia mbili kidogo huku moyoni wakijua wazi kuwa ni wafiki. Wanatulazimisha watanzania tuamini kuwa wao ni binadamu ilhali wakijua kuwa ni mafisi-simba. Wamevaa suti na wamejipulizia pafyumu ili tuamini kuwa wao ni watu, sisi tunawaambia kuwa sio watu. Hata kama wakijipaka lipstick midomoni mwao sisi tunawaona kama mashetani kwani tunajua fika kuwa ni mbuzi, si watu.

Tume ya uchaguzi wa Tanzania, mmemvisha mbuzi suti na tai na kutaka kutuaminisha watanzania kuwa ni mtu, nasi tunasema siyo MTU.
Yeyote aliyejipa ushindi kwenye uchaguzi huu ilhali anajua hakushinda, SIYO MTU ni MBUZI.
 
Kuna hadithi naipenda sana nami leo naomba niwapigie humu jamvini. Kabla ya kuipiga hadithii hiyo naomba niwatahadharishe watanzania wenzangu kuwa wapo wengi wanaamini mtu katika kuaminishwa tu, na si kutambua kihalali. Kuna mtu anaweza kuwekewa mbuzi mbele yake na kuaminishwa kuwa ni mtu naye akasema kuwa kweli ni mtu.

Hadithi hadithi....
Palitokea bwana mmoja aliyeishi kijiji kimoja huko Tanzania. Mtu huyo alibahatika kuwa mbuzi mmoja ambaye alimpenda sana. Mbuzi huyo alimpeleka machungoni kila siku hata akawa na afya hakuna mfano wake pale kijijini. Watu wengi walimuonea wivu yule ndugu nakumshawishi amchinje ili wamle wote kwa pamoja. Yule ndugu alikataa katakata kuwa hawezi kumchinja mbuzi wake kipenzi. Baada ya kuzongwa sana na majirani zake aliamua kumuuza yule mbuzi lakini hakutaka mtu wa pale kijijini kwao amnunue hivyo aliaimia kumpeleka kwenye mnada uliokuwa unafanyikambali na kijiji chao. Siku ilipofika alimfunga mbuzi wake kamba shingoni na kuanza safari kuelekea kwenye mnada. Akiwa njiani alikutana na mtu mmoja ambaye baada a kusalimiana alimuuliza anapokwenda. Mwenye mbuzi alimjibu kuwa anakwenda kuua mbuzi wake mnadani. Yule jamaa akamuuliza kwani huyo mbuzi yuko wapi na yule ndugu akamwambia si huyu hapa nimemfunga kamba. Yule mtu asiyejulikana akamwmbia mbona huyo ni mbwa? Yule mfugaji akakasirika na kuendelea na safari yake. Mbele tena akakutana na mtu mwingine ambaye mazungumzo yao hayakutofautiana na yale ya yule mtu wa kwanza na hapo jamaa akaanza kujiuliza maswali mengi kichwani lakini akandelea na safari yake. Mwishoni alikutana na mtu wa tattu, halikadhalika maongezi yao yakawa kama yale ya waliotangulia. Yule masikini mfugaji akaanza kujiuliza maswali mengi kichwani kuwa huenda kweli nimebeba mbwa badala ya mbuzi. Alimfunga kamba mbuzi wake kwenye kisiki cha mti na kukaa kwa mbali ili kumchunguza kwa makini na kujua ni nini alichobeba. Akiwa anatafakari kichwani alianza kuamini kuwa wale ndugu watakiuwa kweli wamemuona mbwa na si mbuzi. Alikaapale akimtazama mbuzi wake na kisha kuamua kumuacha pale kwenye kisiki na kurudi zake nyumbani kwake akiamini kuwa watu wamemchezea kwa kumbadilishia mbuzi wake na mbwa.

Moral of the Story: Never Trust NEC and its organs
 
Kuna watanzania wengi hawaamini kile wanachokifanya na hudhani kile wanachokisikia ktoka kwa wengine ndicho sahihi na hasa inapotekea kitu hicho kusemwa redioni ama kwenye televisheni. Kuna wengi wataamini kuwa wale mbuzi waliovishwa suti na tai ni watu. Hao ni sawa na yule mkulima alietelekeza mbuzi wake porini akidhani aliyoambiwa na wahuni ni kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom