Muhidin ndolanga kwa hili umetia aibu kabisa embu wajibika usitie aibu na familia

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Tunaitaji vichwa vyenye akili kama hivi

michael richard wambura...labda mtajiuliza kwa nini nasema hivi soma vichekesho
kipindi cha michezo juzi alilizwa sheria zitakazotumika kupitisha wagombea akadai
moja wapo ni elimu kidato cha nne..ne ziniginezo

sasa basi mchakato umepita amepitishwa mtu anaitwa amin bakheresa ...nasikitika kweli hela yake kipindi hiki aitafanya kazi maana watanzania tumeamua atutaki kukaa na walevi wa madaraka ..huyu bwana ana miaka 30 kwenye uongozi pili hana elimu ya kidato cha nne ..tatu amekaa kwenye uongozi miaka 5 bila kuitisha uchaguzi...sita amekubali kukaa na kaimu katibu mkuu miaka 4 kwenye uongozi

nasema shame kwa nini mzee wetu huyu amejiaibisha ningekuwa mimi mwanae kesho yake ningeandika sick nikaondoka ..alipotaja majina akaulizwa bakhresa amepita kwa kanuni gani hana kidato cha nne ...akajibu amepita kwa historia ...akaambiwa unajua katiba ya drfa vizuri akaishia nasema hiviusiniulize we mtoto mdogo sana uwezi sumbua kichwa changu waambie waliokutuma wakaweke pingamizi kwa kufwata sheria ....gooooooooooodd

naamini this time mzee muhidin aibu itakushukua ameweka pingamizi si la bakheresa hadi na wewe utakiwi kuwa mwenyekiti hata kidogo na usanii wako
 
NDOLANGA NILISHAWAHI KUANDIKA HAPA SHULE INASUMBUA SANA VIONGOZI WETU NA NDIO MAANA SERIKALI ILITUMIA GARAMA ZOTE KUKUONDOA NA KUHAKIKISHA ANAKAA MTU MWENYE ELIMU YAKLE PALE JUU TFF SOMA SHULE HIYO MZEE NAAMINI WANAO WATAKUFIKISHIA UJUMBE

MICHAEL RICHARD WAMBURA
P.O. BOX 22557,
TEL. 0713/0754/O787 326 485
DAR ES SALAAM.

September 15, 2012
Mr A. Ndolanga
MWENYEKITI,
KAMATI YA Uchaguzi ya DRFA
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU- DSM(DRFA)

YAH: PINGAMIZI JUU YA KAMATI YA UCHAGUZI , WAPIGA KURA, NA WAGOMBEA KATIKA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA DAR-ES-SALAAM(DRFA) ULIOPANGWA KUFANYIKA OCT ,2012

Nimelazimika kuleta maombi ya pingamizi langu mbele yako na kamati yako kuhusiana na uchaguzi tajwa hapo juu wa DRFA kutokana na uvunjifu wa kanuni, maagizo na Katiba ya TFF sambamba na katiba ya DRFA na sheria za nchi katika mchakato mzima wa kuelekea katika uchaguzi huo , malalamiko yangu ambayo sehemu kubwa ni ya kisheria na kikatiba malalamiko yangu ni kama ifuatavyo.

  1. Uundwaji wa kamati ya chaguzi ya DRFA umevunja kanuni ya uchaguzi wa wanachama wa TFF (TFF MEMEBERS STANDARD ELECTROL CODE) Ibara ya 3(2) inakataza mtu mmoja kuwa mjumbe wa kamati mbili za uchaguzi za wanachama wa TFF au wanachama washiriki wa TFF "The members of the Committee shall under no circumstances be member of the executive body of TFF or Executive body of the Association or Executive of other TFF member Association or the Elections Committee of the other member association of TFF or Executive body /Elections Committee of a subordinate" kwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Muidin Ndolanga Pia Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya FRAT(taifa ambao wote ni wanachama wa TFF basi uhalali wake wa kuwa m/kiti wa kamati ya Uchaguzi wa DRFA unakuwa haupo kwa kuwa unavunja kanuni za uchaguzi , kwa maana hiyo naomba tamko la kuwa mchakato mzima wa uchaguzi ufutwe na kuanza upya kwa kuwa haukufuata taratibu na kanuni husika .
  2. Katiba ya DRFA toleo la 2008 ibara ya 1(6) inatamka kuwa "DRFA itaheshimu Katiba, Kanuni Maagizo na Maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake" TFF kupitia barua yake kumbukumbu TFF/ADM/EC/36 ya tarehe 22/7/2011 yenye kichwa cha habari " Katiba za Wanachama na Wanachama wao" kwenda kwa makatibu ambapo iliagiza kufanyika mabadiliko katiba zao ili ziendane kikamilifu na katiba ya mfano ya TFF aidha TFF kupitia barua yake ya tarehe 12/12/2012 yenye kumbukumbu TFF/TECH?GC11/115 kwenda kwa makatibu wa wilaya ikikumbushia kurekebisha katiba zao ili ziendane na Katiba ya mfano ya TFF, Kwa kuwa Katiba za wanachama wa DRFA na DRFA hazijafanyiwa marekebisho na wahusika ni wazi hawajatekeleza maagizo ya TFF hivyo kwenda kinyume na Katiba ya TFF 12(d)(e) & (n) na Ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi za TFF na Wanachama wake. Na hata kama marekebisho yamefanyika ni wazi hayatakuwa yamezingatia matakwa ya kisheria na maamuzi ya TFF kwani katiba hiyo haijapitishwa na kamati ya sheria, Katiba na hadhi za wachezaji kama maagizo ya awali ya TFF yalivyo agiza.
  3. KUKIUKWA KWA KATIBA YA DRFA
Marekebisho ya Katiba yanayodaiwa kufanywa hayakuzingatia katiba ya DRFA "kazi mojawapo ya Mkutano mkuu wa DRFA ni kufanya na kupitisha marekebisho ya katiba" kwa kuwa marekebisho hayajapitishwa na mkutano mkuu wa DRFA" kama katiba inavyo elekeza basi marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa katiba ya DRFA

  1. Kwa kuwa wilaya wanachama wa DRFA hawakufuata kanani za Uchaguzi za TFF na Wanachama wake, kumepelekea baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutokuwa na sifa ikiwemo ya Elimu isiyopungua kidato cha Nne ikiambatana na Cheti cha Matokeo kama ilivyoagizwa na TFF katika barua yake kwa wanachama wake na wilaya, kwa kuwa viongozi hao wa wilaya wanakosa sifa ya kuwa viongozi ni wazi pia wanakosa sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, itakumbukwa katika Uchaguzi wa Chama cha mpira Mkoa Mara(FAM) ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Nd Lyato) alikuwepo ambapo Nd MAGOTI ambaye alikuwa Katibu wa Chama cha mpira Wilaya ya Bunda aliondolewa katika kugombea na hakurusiwa kupiga kura baada ya kuonekana hakuwa na sifa ya kuwa Katibu wa wilaya kutokana na tatizo la Elimu halikadhalika Katibu wa Wilaya ya Serengeti Ombeni Magati nae aliondolewa katika kugombea ujumbe wa kamati ya Utendaji na pia hakuruhusiwa kupiga kura na nafasi walizokuwa wanazishikilia kutangazwa kuwa ziko wazi, hivyo ni matumaini yangu hata katika DRFA na wanachama wake mkondo utafuata huo huo.
  2. kiongozi anaemaliza muda wake atakuwa na haki ya kutetea nafasi yake ili mradi awe na sifa kwa mujibu wa Katiba na kanuni za DRFA na TFF , itakumbukwa kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Mzee Hasan Dalali aliondolewa kugombea kwa sababu ya kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne huku Mwenykiti wa sasa wa DRFA ndugu Amin (AKA Bakhresa) na Nd Damas Ndumbaru wakiwa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyotekeleza na kuzingatia Kanuni za uchaguzi za TFF, aidha Nd A. Bulembo nae aliondolewa kwa vigezo hivyo hivyo katika uchaguzi wa timu Villa Squad ya DSM, kanuni haikuishia hapo iliendelea mpaka kwa timu ya Coastal Union ya Tanga, kwa misingi hiyo ni wazi kamati hii haitafumbia macho kwenye hili la DRFA.
Aidha ninapenda kuikumbusha kamati yako kuwa Kamati ta uchaguzi ya TFF hivi karibuni ilisitisha chaguzi za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kutokana na dosari za Vyeti vya elimu kwa wagombea kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF
6.0 PINGAMIZI KWA MGOMBEA AMIN MOHAMED SALIM (AKA BAKHRESA

6.1 Mgombea mtajwa hapo juu ni mmoja wa wagombea ambae jina lake limetajwa kupitishwa kugombea nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi wa DRFA, Katiba ya DRFA ibara ya 29(3) inamtaka mgombea kuwa na sifa zilizo ainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Elimu ya kidato cha Nne, aidha ibara ya 9 ya kanuni za Uchaguzi wa wanachama wa TFF inatamka ibara ya 9(2) amboyo ina tamka wazi kuwa mgombea yoyote lazima awe na Elimu ya kidato cha nne inayo ambatana na cheti cha matokeo any person contesting any position " Must have minimum academic qualification of form Four and holder of a certificate of ordinary Secondary Education" . Kwa kuzingatia maelezo na sifa za kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF, Katiba na maagizo mbalimbali ya TFF na katiba ya DRFA Mgombea mtajwa Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) anakosa sifa ya kuwa mgombea Mwenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana Elimu ya Kidato cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo hivyo jina lake liondolewe katika orodha ya wagombea waliopitishwa kugombea uongozi wa DRFA.
6.2 Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) hana sifa ya
kugombea kwa mujibu wa ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF "The person contesting any position in the association must have integrity and the capacity of performing fulfilling and implementing Association obligations and objectives" kwa sababu zifuatazo:
1. 20/01/1993 aligombea uongozi kwa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya FAT. Alijaza form ya maombi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutoa maelezo ya uongo ya kuwa ana elimu ya kidato cha nne na kutoa kiapo huku akijua maelezo yake ni ya uongo ANNEXED "A" Aidha pamoja na form hiyo Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA aliasilisha cheti cha kugushi kuwa amemaliza kidato cha Nne katika shule ya sekondari Tambaza (school living Certificate)mwaka 1974 huku akijua kuwa Hasemi ukweli ANNEXED "B"
6.3 Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) huku akijua hasemi ukweli mwaka 1994/Dec/17 Katika form yake ya kuomba uongozi FAT alieleza ya kuwa Amehitimu Darasa la Nane(STDVIII) mwaka 1965 na mwaka huo huo akawa mchezaji wa Cosmopolitan akipingana na barua aliyoiwasilisha mwaka 2000 kutoka Wizara ya elimu ya Serekali ya mapinduzi Zanzibar ANNEXED "C" inayosema kuwa Amemaliza miaka 8 ya mafunzo katika shule ya Msingi Darajani 1965 uhalali wa barua hiyo unatia shaka hivyo inahitaji kuhakikiwa uhalisia wake.
6.4 Mwaka 2005 Ndugu AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) alifunguliwa jarada la mashtaka ya kugushi maandishi na Nd OPIYO jalada CD/RB/6236/05 na CD/IR/2707/05 la kosa la kugushi vyeti jambo ambalo mlalamikaji yuko tayari kuwaslisha ushahidi mbele ya kamati yako
7.0 PINGAMIZI DHIDI YA WAPIGA KURA WAFUATAO
1. ABEID MZIBA –KINONDONI
2. SALEH NDONGA-TEMEKE
3. PETER MUHINZI- TEMEKE
4. DAUDI KANUTI- ILALA
5. GUNGULUGWA TAMBAZA-ILALA
6. Na wengine

Majina niliyo yataja hapo juu ni wajumbe na wanawakilishi wilaya zao katika mkutano mkuu wa DRFA, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF , maagizo mbalimbali ya TFF, katiba za mfano zilizotolewa na TFF pamoja Katiba ya DRFA nilio wataja hapo juu wanakosa sifa za kuwakilisha wilaya katika mkutano mkuu wa DRFA kwa kukosa Elimu ya Kidato cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo.
Naomba kamati yako itamke kuwa viongozi hao walichaguliwa kimakosa bila kuzingatia kanuni za uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe ziko wazi ili wapatikane watu wenye sifa za kikanuni kugombea, pia wasiruhusiwe kushiriki kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, aidha ninapenda ufahamu jambo kama hili lilifanyika katika Uchaguzi wa Mkoa wa Mara(FAM) ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF taifa ilishiriki na ilitoa mwongozo na kusimamia utekelezaji wake.

Kwa kuzingatia Maelezo hayo hapo, Ninawasilisha pingamizi langu lenye sehemu tatu(3) pamoja na nakala za maagizo mbali mbali ya TFF kwa wanachama wake:
8.0 Kwa kuzingatia Maelozo hayo hapo, Ninawasilisha katika maombi ya dharura kama ifuatavyo:

(a) Tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ivunjwe na kuundwa upya.
(b) Tamko kuwa Mchakato mzima wa uchaguzi uanze upya mara baada ya Kamati mpya kuundwa.
(c) Tamko katiba ya DRFA ina kinzana na katiba Kanuni na Maelekezo ya TFF hivyo ifanyiwe marekebisho. yanayostahili kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.
(d) Tamko la kufanyika kwa Uhakiki wa sifa za viongozi wa wanachama na wanachama washiriki wa DRFA ili kuridhia matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba za Mfano za wiliya zilizotolewa na TFF.
(e) Tamko kuwa kuiruka kamati ya sheria na Katiba ya TFF katika kuipitisha katiba ya DRFA ni ukiukwaji wa maagizo ya TFF
(f) Jina la Mgombea Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) liondolewa kwenye orodha ya wagombea
(g) Wapiga kura wote wasio na sifa ambao wamegombea waondolewe kwenye orodha ya wagombea.
(h) Jambo au uwamuzi mwegine wowote ambao kamati itaona unafaa kwa maendeleo DRFA na taifa kwa Ujumla

………………………………….
MICHAEL RICHARD WAMBURA
MLALAMIKAJI/MPINGAJI
15[SUP]th[/SUP] Sept, 2012

CC:Nd L.C Tenga Rais shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF)
CC: Nd D. Lyatto M/kiti Kamati ya Uchaguzi ya –TFF
CC: A Mgongolwa - Mwenyekiti-kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi
za wachezaji

Ni vigumu kuchukua haki ya mtu kinachofanyika ni kuchelewa tu ....yetu macho mkuu
 
Mkuu hivi ni wewe ile majuzi kipindi cha michezo manake nilicheka mpaka basi Bakhresa hana elimu na amekaa madarakani miaka 30 na kuifanya DRFA kuwa ni ya familia yake dah ulimuua kinoma sasa imekuweje washakurejesha kwenye nafasi ya kugombea? huko DRFA?

Ila kuna watu hawataki kuondoka kwenye soka japo vipindi vyao havikuwa na lolote walilofanya hata el-mamry anaboa tokea tupo watoto kila siku yeye yeye tu Bakhresa Toka its time now kung'atuka
 
Hata sijui niseme nini, hiyo barua ya pingamizi inajibu yote kwa nini Wambura hatakiwi! Anajua, ana msimamo usioyumba hivyo atawasumbua sana pale watakapohitaji kufunika kombe ili mwanaharamu apite, Tenga keshashiba na hajishughulishi kuona TFF inaendeshwa kwa mujibu wa katiba! Shame...!
 
Potelea mbali liwalo na liwe kwa ujeuri ujinga anaouonyesha Ndolanga katika soka la bongo, naomba niungeni mkono niende mahakama kuu kuishtaki TFF na Ndolanga wake liwalo na liwe bora nifungiwe mimi binafsi
 
Tunaitaji vichwa vyenye akili kama hivi
Join Date : 20th September 2010
Posts : 1,075
Rep Power : 621
Likes Received150
Likes Given150

Nimependa sana ulivyolinganisha likes zako na zile unazowapa watu. safi sana mkuu

Back
Top Bottom