Muheshimiwa Jussa, siasa zako zimepitwa na wakati

Tatizo hawa watu rangi ya bagachori tumewalea mno kiasi kwamba wanajiona kama watanzania. huyu jamaa ana udini sana na hafai ndo maana wazanzibari baada ya katiba waondoke wakaolewe na ccm! ana uwezo mdogo wa kufikiri (kiraza). huwa namfananisha na mbwa aliyeziba masikio!
 
wazanzibari kama alivyoeleza alioandika makala wanajua kuwa muundo wa muungano wetu una matatizo, na wanapenda sana kuona kuna mabadiliko ambayo utatoa fursa kwa pande zote mbili kuufaidi muungano wetu. na sio kweli wazanzibari wanachotaka kwenye muungano ni upendeleo. bali kuona haki inatendeka.

ila wakati huo huo wananchi wazanzibar wamewashtukia ziongozi wao kuwa ni wananafiki, watu wasio na uchungu wa ukweli na wanachi wao. bali hutumia shida zao kujipandisha kisiasa. wao kwa maslahi yao wako tayari hata kuwajengea chuki baina yao ( Unguja na upemba) au na ndugu zao wa bara (watanganyika).

kuna mengi ambayo wazanzibari wameshtuka kuwa viongozi wengi wa zanzibar wawe CUF au CCM hawako kwa kuangalia maslahi ya wazanzibar.

kwa kweli zanzibar kuna nguruma na wananchi wanasubiri kwa hamu hio mikutano ya kutoa maoni ya kuanza kwa katiba mpya
 
Mpuuzi Mtu wa Pwani.

Umefikiria ukimsema Jussa hapa tutaanza kuichukia zanzibar.
Issue ni kua sheria inasema lazima awe mtanzania; ndio wawakilishi wote CCM, CUF wamesema ibadilishwe iwe mzanzibari.
Ukumbuke kwamba kuna zanzibar na wazanzibari (HAKUNA TAIFA LINALOITWA TANZANIA; ILIYOKUWEPO NI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA). Vitu viwili aidha ibaki wazanzibari au iseme afrika mashariki (kwavile tuna muungano mkubwa zaidi sasa hivi wa afrika mashariki). Sasa mnataka wazanzibari watupendelee sisi tu; hem kuweni wakweli; wacheni unafiki. Si ni sisi tu hapa hatutaki wakenya waje wahodhi ardhi ya tanganyika; kwa nini, si tuwaachie tu waje; kwani sisi sote sio ndugu! Mmasai wa Arusha na wa kenya kuna tofauti gani.

Wacheni pumba; ujinga umetuzidi kichwa.




haya ndio wanayosema wazanzibari, kwa kweli ni maneno mazito na yenye ukweli wa kutosha kwa ndugu yetu hyu na baadhi ya wachache wenziwe


MUHESHIMIWA JUSSA SIASA ZAKO ZIMEPITWA NA WAKATI

Tunajuwa kila Mzanzibari angependelea kuona kuna mabadiliko katika Muungano,wengine wanapenda kuona kuna serikali tatu na wengine wanataka muungano uvunjike kabisa,na hi ndio maana ya demokrasia kuwa kila mtu awe na uhuru wa kuchaguwa.

Kila unapopita kwenye maskani mazungumzo ni Muungano hakuna habari nyengine,na baadhi ya viongozi wameona watumie muda huu kwa kujipa umaarufu kwa manufaa yao wao wenyewe na sio kwa manufaa ya wananchi.

Muheshimiwa Jussa wewe ni mmoja kati ya watu ambao tunakupa heshima ya juu kwa vile una elimu kushinda wawakilishi wengi lakini kitendo chako cha kutunga mswada wa kuwataka Watanganyika wasiajiriwe katika sekta ya utalii kilikuwa ni kitendo cha kijinga na upumbavu,mtu yoyote yule anaejuwa ukweli basi anajuwa kuwa huu ulikuwa mswada wa kujitafutia umaarufu kwa sababu hata wewe mwenyewe ulikuwa unajuwa kuwa mswada hauendi popote na ndio maana hata baadhi ya viongozi wenzako wa CUF pia hawajakusaidia kwa sababu walijuwa ni mswada wa kipuuzi na wa kijinga.

Japokuwa umepata waafuasi wengi ambao wamependa ulichokifanya lakini watu hao ni wale mambumbumbu ambao kutwa wanakaa maskani na wako tayari kudanganywa na viongozi kama nyie,na watu hawa wa maskani hata uwape kazi hawatofanya kwa sababu kazi kwao sio kitu wanachokijuwa,na wewe Jussa baada ya kufahamu hivi ndio umeona uwaingie katika vichwa vyao kwa manufaa yako ili uonekane kwamba unafanya la maana.

Hata kama hatukubaliani na Muungano lakini kwa sasa Muungano umedumu na hii ni nchi moja,sasa inakuwaje umwambie mwananchi asiweze kuajiriwa?Wewe huoni kitendo hicho kinaweza kusababisha madhara makubwa,umefikiria kama watu wa Bara wakisema na Wazanzibari wasiajiriwe katika kazi fulani je hali hii itakuwaje, je wewe utakuwa tayari kuchukuwa majukumu ikiwa kutatokea fujo kwa chuki za kijinga unazozipandikiza? La ukweli tuseme Bara kuna Wazanzibari wengi wenye biashara na wanaofanya kazi kuliko watu wa Bara wanaofanya kazi Zanzibar, tembelea kariakoo katizame nani anamiliki maduka wengi wao ni wageni tukiwamo sisi Wazanzibari.

Muheshimiwa kama unataka kuwasaidia Wazanzibari basi kuna mengi ya kuwasaidia la kwanza waambie wasikae na kudehenyeka maskani waambie wakatafute riziki, Kuna vijana wengi wana vipaji vikubwa vya kutumia mikono yao,kwa nini serikali haiwaendelezi, unaonaje ukapitisha mswada wa kuwabana wizi na wabadhirifu wa mali ya umma katika serikali, unaonaje ukapeleka mswada wa kuimarisha kiwango cha elimu Zanzibar vijana wakanufaika, Au unaonaje ukapitisha mswada wa kuweza kuwakamata wala rushwa na wafanya biashara ya madawa ya kulevya?

Lakini yote haya wewe hujayaona umeona upeleke ule muswada wa kipumbavu, tunakuomba usianzishe siasa za chuki kwani mwisho wa chuki ni fitna na baada ya fitna ni kuingiana mwilini,wewe umesoma kwa hiyo weka siasa pembeni na wasaidie wananchi kama kweli unataka usaidie na kama huna nia ya kusaidia basi tunakushauri ukae kimya,la mwisho Zanzibar inategemea utalii mpaka leo hakuna website ya serikali inayotangaza utalii unaonaje ukapeleka mswada huu ili ianzishwe website ya kuitangaza Zanzibar?

Na sisi wananchi lazima tukae macho na kujuwa na kupambanuwa lipi zuri na lipi baya tutumie akili zetu sio unakubali na kupiga makofi kila unaloambiwa na kukaa maskani tupunguzeni! Mwenyezi Mungu anampa kila mja wake riziki lakini lazima hiyo riziki uitafute


source: Group ya FB ya Wazanzibari "VOICE OF ZANZIBAR "
 
Mpuuzi Mtu wa Pwani.

Umefikiria ukimsema Jussa hapa tutaanza kuichukia zanzibar.
Issue ni kua sheria inasema lazima awe mtanzania; ndio wawakilishi wote CCM, CUF wamesema ibadilishwe iwe mzanzibari.
Ukumbuke kwamba kuna zanzibar na wazanzibari (HAKUNA TAIFA LINALOITWA TANZANIA; ILIYOKUWEPO NI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA). Vitu viwili aidha ibaki wazanzibari au iseme afrika mashariki (kwavile tuna muungano mkubwa zaidi sasa hivi wa afrika mashariki). Sasa mnataka wazanzibari watupendelee sisi tu; hem kuweni wakweli; wacheni unafiki. Si ni sisi tu hapa hatutaki wakenya waje wahodhi ardhi ya tanganyika; kwa nini, si tuwaachie tu waje; kwani sisi sote sio ndugu! Mmasai wa Arusha na wa kenya kuna tofauti gani.

Wacheni pumba; ujinga umetuzidi kichwa.

mkuuu taratibu sio mm nilioiandika mm nimeileta kwa kujadiliwa tu, japokuwa nnaona mawazo ni mjarabu
 
Tatizo hawa watu rangi ya bagachori tumewalea mno kiasi kwamba wanajiona kama watanzania. huyu jamaa ana udini sana na hafai ndo maana wazanzibari baada ya katiba waondoke wakaolewe na ccm! ana uwezo mdogo wa kufikiri (kiraza). huwa namfananisha na mbwa aliyeziba masikio!

Pole pole Ahali yangu.

Lakin si umesikia Rais wenu amekataza kuujadili muungano katika zoezi la kuandika katiba mpya?
Sasa wewe unasema katiba gani hiyo?

Fikiria kabla kunena.


 
Back
Top Bottom