Mufti Simba una hoja ya kuwajibu Watanzania

Kwanza kamwite Askofu wenu Laizer na Askofu mkuu wa katoliki watueleze kwanini walikuwa wanatuambia tuwachague Chadema mwaka jana?

Acha kutuletea hoja za kimasaburi hapa. Nchi nzima imepoteza dira. Huyo DC ni muislamu as long as akiwa hajabadili dini yake kwa kuritadi (kutamka amejitoa katika uislamu). Hivyo basi inamlazimu avae hijabu au mtandio kusitiri nywele zake. Kaulize wajuzi wote wa dini watakuambia.

Ama kuhusu kuolewa na mkristo hilo swala jengine ila kiislamu hapo hakuna ndoa bali wanazini ila yule mwanamke ataendelea kuwa muislamu kama kawa!!!! Acheni udini wenu nyie watu mnaipeleka nchi pabaya na ubaguzi wenu wa kijinga. Tuliachie jambo lijadiliwe mahakamani kwanza ndio tuseme lolote.
Mkuu hapa unafanya makosa makubwa kutoa habari za uongo.

Imani ya dini sio jina wala kukiri kwa ulimi pekee bali ni kuamini na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu..Ipo mifano mingi ktk Uislkaam inayoonyesha watu wakati wa Mitume wakivaa mahijab, wakiitwa majina ya kiarabu hawakuwa Waislaam na Manasara na Wayahudi walioitwa waislaam.

Jua moja kubwa sana ktk Uislaam linasema tofauti baina ya Muislaam na Kafir ni SALA.. Sasa kama kuran imesema hivyo utamwita vipi mtu aliyekiuka mengi zaidi ya sala!..Hijab ni vazi la staha kwa mwanamke ni ustaarabu wa vazi ambao unafanywa na Wakristu, Wayahudi, Budha, Wapagan na Waislaam.
 
Mkuu hapa unafanya makosa makubwa kutoa habari za uongo. Imani ya dini sio jina wala kukiri kwa ulimi pekee bali ni kuamini na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu..Ipo mifano mingi ktk Uislkaam inayoonyesha watu wakati wa Mitume wakivaa mahijab, wakiitwa majina ya kiarabu hawakuwa Waislaam na Manasara na Wayahudi walioitwa waislaam. Jua moja kubwa sana ktk Uislaam linasema tofauti baina ya Muislaam na Kafir ni SALA.. sasa kama kuran imesema hivyo utamwita vipi mtu aliyekiuka mengi zaidi ya sala!..Hijab ni vazi la staha kwa mwanamke ni ustaarabu wa vazi ambao unafanywa na Wakristu, Wayahudi, Budha, Wapagan na Waislaam.

Mkuu,

Suala la DC mie nimesema sitaki comment hadi litolewe hukumu mahakamani ila inashindikana kuvumilia wakati watu wanapomkebehi mufti aje awajibu watu wakati maaskofu wakitoa matamko yasiyowahusu siwasikii wakisema wanamuomba Askofu Laizer au Askofu wa Katoliki aje kujibu humu jamvini huu unafiki siukubali. Mufti hana muda huo na simshauri ajibu lolote awaache wenyewe mjijibu au tutamsaidia kuwajibu kuwa kamuulizeni Askofu wenu yale matamko ya kusema tuwachague Chadema vp yako katika biblia?

Ama kuhusu DC kuna watu wanaomjua vizuri huyo mama na ni kweli muislamu achana na habari za akina Kubenea wanaopotosha mambo. Kuna watu wa karibu wa huyo mama wanasema ni muislamu. Hivyo suala la hijabu kwake ni lazima na wajibu hata kama ameshazaa na mkristu au la. Hivyo mkuu nina uhakika na ninalolisema kuwa huyu mama ni muislamu kweli na sio mkristo kama baadhi ya watu wanavyodai. Nimefuatilia kwa ukaribu kufahamu zaidi.
 
ni msimamo wa waislamu wote, wewe unasema aje? Mufti ni kiongozi wetu akisema wote tunaunga mkono.

uislamu si dini inayoendeshwa kwa maoni na ushauri wa mtu fulani, bali ni dini ya hoja na dalili, huwezi kusema "akisema sisi twaunga mkono" je, hata kama anachokisema ni uozo wake yeye binafsi? Huo ni upumbavu na wala sio uislam. Uislamu uko mbali na majukwaa ya kisiasa! Na wala waislamu hawapaswi kusogelea majukwaa hayo. "cha uislam upewe uislam, cha simba apewe simba!"
 
Mkuu,

Suala la DC mie nimesema sitaki comment hadi litolewe hukumu mahakamani ila inashindikana kuvumilia wakati watu wanapomkebehi mufti aje awajibu watu wakati maaskofu wakitoa matamko yasiyowahusu siwasikii wakisema wanamuomba Askofu Laizer au Askofu wa Katoliki aje kujibu humu jamvini huu unafiki siukubali.

Ama kuhusu DC kuna watu wanaomjua vizuri huyo mama na ni kweli muislamu achana na habari za akina Kubenea wanaopotosha mambo. Kuna watu wa karibu wa huyo mama wanasema ni muislamu. Hivyo suala la hijabu kwake ni lazima na wajibu hata kama ameshazaa na mkristu au la. Hivyo mkuu nina uhakika na ninalolisema kuwa huyu mama ni muislamu kweli na sio mkristo kama baadhi ya watu wanavyodai. Nimefuatilia kwa ukaribu kufahamu zaidi.
Nakuelewa katika hilo lakini Mufti ndiye kalifanya swala hili kuwa la dini.. haya ni makosa ambayo wewe kama Muislaam hutakiwi kuyaunga mkono. Sasa kama Askofu alisema hivyo nasi tunatakiwa tuseme hivyo? Haya Askofu kawaambia wanywe pombe sii haramu wee utamtaka Mufti atangaze kwa waislaam..Yamekuwa mashindano?

Makosa yalifanyika kumvua mama yule vazi lake la staha kama utakavyovuliwa wewe nguo yoyote ile ya kiume hata ikiwa kofia ni makosa na Uislaam unapinga kuvuliwa binadamu vazi lake na dini zote sii Uislaam pekee unapinga matumizi ya nguvu. Mufti anaposimama na kusema waislaam wasikipigie kura Chadema kwa sababu walimvua mwanamke hijab ili hali mhusika tayari kisha kamatwa na kupelekwa mahakamani, hii sii kwa mapenzi na mafundisho ya dini, ni UDINI ili kujenga chuki za wananchi dhidi ya chama. Kuna zaidi ya mauaji ya Mwembechai ama kuvunjwa kwa Balukta na viongozi wake kutiwa ndani wengine kuuawa, hakuna kesi wala serikali kuomba msamaha! Mbona sijasikia hawa viongozi wakisema tusikichague chama cha CCM!

Mkuu wangu msipende sana kuwashabikia hawa watu ambao wamewekwa kwa ajili ya kukitumikia chama. Kesho itakuwa Idd Alhaj watakwambia hutakiwi kusherehekea Idd hadi Mufti atoe idhini hata kama jana yake waumini walisimama Araf..Yaani Mufti amekabidhiwa mamlaka ya Kiungu?.. Acheni ushabiki mkuu wangu, hautaweza kuwasaidia waislaam isipokuwa kuwaondoa zaidi ktk Uislaam.
 
punguani ni wewe na familia yako huwezi kujumuisha waislamu wote bloodyfoooool!!!!!!

Soma vizuri alichoandika sio kukimbilia matusi,kinachojadiliwa ni hoja na si matusi ,iwapo wewe unawatetea kila wanaounga mkono lolote linalotamkwa na bakwata kuhusu waislam basi nawe unahusika,vinginevyo huusiki na alichokieleza
 
Nakuelewa katika hilo lakini Mufti ndiye kalifanya swala hili kuwa la dini.. haya ni makosa ambayo wewe kama Muislaam hutakiwi kuyaunga mkono. Sasa kama Askofu alisema hivyo nasi tunatakiwa tuseme hivyo? Haya Askofu kawaambia wanywe pombe sii haramu wee utamtaka Mufti atangaze kwa waislaam..Yamekuwa mashindano?

Makosa yalifanyika kumvua mama yule vazi lake la staha kama utakavyovuliwa wewe nguo yoyote ile ya kiume hata ikiwa kofia ni makosa na Uislaam unapinga kuvuliwa binadamu vazi lake na dini zote sii Uislaam pekee unapinga matumizi ya nguvu. Mufti anaposimama na kusema waislaam wasikipigie kura Chadema kwa sababu walimvua mwanamke hijab ili hali mhusika tayari kisha kamatwa na kupelekwa mahakamani, hii sii kwa mapenzi na mafundisho ya dini, ni UDINI ili kujenga chuki za wananchi dhidi ya chama. Kuna zaidi ya mauaji ya Mwembechai ama kuvunjwa kwa Balukta na viongozi wake kutiwa ndani wengine kuuawa, hakuna kesi wala serikali kuomba msamaha! Mbona sijasikia hawa viongozi wakisema tusikichague chama cha CCM!

Mkuu wangu msipende sana kuwashabikia hawa watu ambao wamewekwa kwa ajili ya kukitumikia chama. Kesho itakuwa Idd Alhaj watakwambia hutakiwi kusherehekea Idd hadi Mufti atoe idhini hata kama jana yake waumini walisimama Araf..Yaani Mufti amekabidhiwa mamlaka ya Kiungu?.. Acheni ushabiki mkuu wangu, hautaweza kuwasaidia waislaam isipokuwa kuwaondoa zaidi ktk Uislaam.

Mkuu,

Unajua kila jamii ina kiongozi wake na muongozo wake na ndio maana wenzetu wakristo wana maaskofu na sisi waislamu tuna masheikh. Mufti alichokosea kujiingiza katika siasa ila kuhusu kuvuliwa mwanamke staha yake ni jukumu lake lazima alikemee kwani asipolikemea kiti chake kitakuwa cha moto. Kosa alilolifanya Mufti ni kusema wasipigiwe chama fulani kura kwani pengine amewagusa wapenzi wa chama fulani ila kulikemea na kulitoea fatwa suala la kumvua mwanamke wa kiislamu hijabu ni sehemu ya kazi yake. Hata wewe ungelikuwa Mufti hilo jambo linakulazimu ulitolee muongozo.

Kwa ufupi niliwahi kusema huko zamani kwa maaskofu wetu na masheikh wetu wakitaka kuingia katika siasa wavue majoho yao waingie katika siasa ama sivyo wakae mbali nayo. Mufti ni kiongozi wa waislamu hivyo lazima akitoa tamko lina uzito wake hata kama baadhi hatukubaliani na taasisi anayoisimamia ya Bakwata ni wajibu wa kila muislamu. Ndio maana Sheikh Hassan bin Ameir (R.A) aliogopewa na Nyerere akamuhamisha kwenda zanzibar amtoe katika kiti chake kwani angelitoa tamko lolote kipindi kile Tanzania ingelichafuka.
 
Hii hapa chini ni post moja iliyotoka kwa mchangiaji wa thread moja kuhusu sakata la yule DC wa Igunga. Naibandika hapa kwani naona ni relevant sana katika thread hii pia.

Hivi bakwata inawafanyia nini Waisilamu kama siyo kutumiwa tu na CCM?

Mimi ni Muisilamu lakini nakerwa sana na chombo hiki kinachodaiwa ni mwavuli wa Waisilamu wote nchini.

Hakina faida yoyote kwa Waisilamu na sasa hivi viongozi wake wanatia aibu kwa kukubali kutumiwa na wanasiasa na viongozi wa serikali ya CCM, tena bila hata ya faida yoyote kwao, achilia mbali shukurani.

Na kinachosikitisha zaidi ni kwamba haya ‘mateke ya punda’ wanayapata chini ya uongozi mkuu wa nchi aliye madarakani ambaye ni Muisilamu.

Hivyo kinachoonekana ni kwamba baadhi ya viongozi hawa wa bakwata huhongwa kwa hela za muda mfupi tu.
Hapa nitatoa vielelezo vya kuonyesha kile ninachokisema:

Pamoja na kwamba ni juzijuzi tu JK alipigilia msumari wa mwisho kuhusu mahakama ya kadhi, Bakwata si tu imeufyata kabisa, bali pia inakubali kutumiwa na hiyo hiyo CCM kufanya ‘cheap’ campaign kwa niaba yao kule Igunga.

Suala la DC wa igunga na Bakwata kukurupuka kumtetea ni mojawapo ya mambo yanayoonyesha ‘ubaraka’ wa viongozi wake, sijui kwa sababu ya umasikini? Suala la DC lilikuwa la kisiasa, lakini Bakwata wakaingilia kulifanya la kidini, na kama vile nilivyosema hawatapata shukurani yoyote kutoka CCM, bali mateke ya punda tu katika madai yao yote halali.

Kuna suala la OIC kadhalika – Bakwata ilishafungwa mdomo tangu zamani, lakini wanaume bado wamo tu na CCM!

JK aliwakera sana Waisilamu kwa kumleta Rais George W Bush wa Marekani mapema 2008. Waisilamu wengi duniani wnamlani Bush aliyesababisha vita Iraq na Afghanistan ambapo maelefu ya Waisilamu wamekufa na kuendelea kufa.

Kwanza wakati wa ujio wa Bush serikali ilipiga marufuku maandamano yoyote ya Waisilamu kuupinga ujio huo, lakini baadaye akina Kundecha walisimama kidete na yakaruhusiwa.

Mwaka 2007 JK alikwenda Vatikan kuonana na Papa Benedict, kuna picha ikimuonyesha akipiga magoti na kuubusu mkono wa Papa. Jee ilikuwa lazima aende huko? Mkapa, Mkatoliki, katika miaka yake 10 ya uongozi hakufikiria kufanya ziara ya namna hiyo.

Tukienda nyuma zaidi wakati wa Mzee Ruksa, Rais wa kwanza Muisilamu wa nchi hii. Serikali yake nayo ilikuwa na maudhi yake mengi dhidi ya Waisilamu:

Alimleta papa John Paul II mwaka 1990, kitu ambacho hata Nyerere mwenyewe Mkatoliki hakufikiria kukifanya katika miaka yake yote ya uongozi.

Mwaka 1993 wakati serikali hiyo ya Mwinyi iliporekebisha siku za kazi kwa watumishi wa serikali kuwa siku 5 kwa wiki (yaani kuondoa Jumamosi kama siku ya kazi) pia alirudisha Sikukuu ya Boxing Day (December 26) hivyo Wakristu kuwa na jumla ya sikukuu nne za kidini kwa mwaka (e.g. Pasaka siku 2, Christmas na Boxing Day) – hivyo kwenda sambamba na Waisilamu ambao tangu zamani za Nyerere walikuwa na sikuu 4 za kidini kila mwaka (yaani Id el Fitr siku 2, id el-Hajj na Maulidi).

Lakini hapo hapo Mwinyi pia alirudisha Januari mosi kama sikukuu ambayo ilikuwa haipo tangu enzi hizo za Nyerere. Swali hapa: Kama aliweka Januari mosi kuwa siku ya mapumziko, siku ambayo ni mapumziko katika ulimwengu wa nchi za Kikristo, kwa nini, pia asiweke siku ya mwanzo wa mwaka wa Kiisilamu (tarehe mosi Muharram - Mfungo Nne) kuwa pia ni sikukuu ya kupumzika? Mwaka jana Waisilamu walisikika wakiiomba serikali nayo pia iiweke siku hiyo iwe ya mapumziko.

Tukiacha hilo kuna suala lile lenye mgogoro la Memorandum of Understanding (MoU) kati ya serikali na Makanisa. Waisilamu hawakuona ajabu kwamba hili lilianza chini ya utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi Muisilamu? Wangemuuliza kwa nini aliwasahau Waisilamu katika MoU?

Kwa ujumla pamoja na mambo yote haya yote hasi (negative) dhidi ya Waisilamu niliyotaja – bado Waisilamu wanaing’ang’ania CCM na kuitetea hata katika mambo cheap kabisa.

Wako wap akina Mponda, Kundecha na Sheikh Khalifa, viongozi machachari wa Kiisilamu waliokuwa wakiihenyesha serikali huko nyuma (eg katika sakata la mauaji ya Mwembe Chai)? Au tayari kwisha nunuliwa na CCM?

Toilet paper: Ukishaitumia .......!!!!
Poleni sana.

bob tusitukanane hapa tunaeleweshana kuhusu matamko ya viongozi wetu,kwani si maaskofu au masheikh huwa wanatoa matamko ambayo wanaingiza ubinadamu wao hivyo tuvumiliane
 
Kura za Waislamu zimeweza kuifanya Chadema ishindwe ktk uchaguzi wa Igunga. Sasa ni wakati wa Chadema kubadilika ktk uongozi wao- ambao hauna demographic ya TZ.

Chadema lazima mjue hamwezi kushinda bila ya Waislamu. Kwa hiyo badilikeni.
 
Mkuu katika wapiga kura wa Igunga Waislamu walikuwa asilimia ngapi hadi useme kuwa CHADEMA wameshindwa kwa nguvu ya waislamu?
 
Ni msimamo wa waislamu wote, wewe unasema aje? Mufti ni kiongozi wetu akisema wote tunaunga mkono.
Toa takwimu za waislamu wa Igunga walivyoitikia mwito huo, halafu linganisha na takwimu za wakristo walioipigia CDM. Kiufupi wewe ndiye uliyesababisha waislamu wasiipigie CUF na CCM kura. Maana mpango mzima ulikuwa CDM itoke kapa sasa hizo asili mia 44 yz CDM mbona nyingi sana ukilinganisha na 4% ya CCM B.
 
Kura za Waislamu zimeweza kuifanya Chadema ishindwe ktk uchaguzi wa Igunga. Sasa ni wakati wa Chadema kubadilika ktk uongozi wao- ambao hauna demographic ya TZ.

Chadema lazima mjue hamwezi kushinda bila ya Waislamu. Kwa hiyo badilikeni.

Mbona unatazama mambo kihuni? Hivi huyo Dalali wa Magamba alikuwa Mwislamu?
 
Mr. Right anapofanya wrong analysis.........

Hawa vijana waliotekwa na magamba wana matatizo makubwa sana.
 
Kura za Waislamu zimeweza kuifanya Chadema ishindwe ktk uchaguzi wa Igunga. Sasa ni wakati wa Chadema kubadilika ktk uongozi wao- ambao hauna demographic ya TZ.

Chadema lazima mjue hamwezi kushinda bila ya Waislamu. Kwa hiyo badilikeni.

Matapishi
 
Back
Top Bottom