Mufti Lion adaiwa kuifilisi BAKWATA

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,703
3,653
Hii imekaaje kulikoni Bakwata kumgeuka Mufti na kumuambia ameifilisi yaani siku zote kuanzia alipoanza hadi kamaliza ndio wanastuka !!!

Wamsamehe tu mambo ya wanadamu hata kuwa Mufti mkuu sio wamba hawezi kufanya makosa....

Au pengine hawajafanya utafiti kabla ya kutoa tamko la kumshutumu Mufti..

Itakuwaje kama Watamshitaki? au Mufti anakinga ya kutoshitakiwa?

Source Magazeti ya 25/12/2012
 
Lakini akikutikana kweli nae amefanya ufisadi naamini hana kinga lazima ashitakiwe, na tutarajie kwa kuwa hizi ni kashfa nzito na kaziona basi nae haraka afunguke bayana kwa utetezi wake na akikaa kimya itakuwa kweli atakuwa ameufanya ufisadi wake apo bakwata.
 
Rushing to media with such allegations pointed to him isn't moral at all.
I thought religious caucus has its ways of digesting that in respectful manners!
 
hata mie nimeshangaa, itafikaje magazetini?

Hakuna mabaraza ya dini?
Afu kiongozi mkubwa kama huyo?

Duh, kwa kuwa si muumini huko nikatoa tu poleni kwa wahusika ila inaacha maswali mengi

How, hadi anafanya yote hayo walikuwa wapi?

Rushing to media with such allegations pointed to him isn't moral at all.
I thought religious caucus has its ways of digesting that in respectful manners!
 
Duh Huu nao ni Ufisadi hii inaonesha mkuu wa nchi anaacha au anaupuuzia ufisadi sasa umeoa hadi kwenye mabalaza ya Dini wakiamini nchi haiana sheria za kuwafanya kitu....

Wadau tudokezeeni Mufti kafilisi kiasi gani isije kuwa kamzadi Shimb0
 
mimi kama muhumini wa wa dini ya kiislam ntasikitika sana kama hizi kashfa zitaishia magazetini tu, kweli dunia imekwisha na itabidi niyaamini haya na lapa lazima hatakuwa peke yake aende keko au ukonga iwe fundisho kwa wengine.huu ushabiki wa bakwata kwa chama tawala wakijua madudu yalojaa umo ccm hasa kugubikwa na ufisadi wa kutisha ni dhahiri hawa bakwata yote imejaa watu wasokuwa wema, hii bakwata imekuwa wakala wa ccm, kumbuka madudu iloyafanya uko igunga kutupotosha waislam wote wakati imedhihirika yule mama hakuwa mwislam.na walivyofasta katika vyombo vya habari nawataraji leo watujulishe kulikoni ata sadaka na kadhalika zinafisadiwa tena na mkuu mufti simba, ndo ata tunaendelea kuwa duni kumbe hiki chaweza kuwa moja ya chanzo. nasisitiza hatua zichukuliwe mapema vinginevyo bakwata watakuwa wanalinda na kufumbia macho maovu.
 
Watasema wangekuwa na mahakama ya "KADHI" wangemshitaki huko!! Mhamishieni Zenj mkamshitaki huko kwani dini si ile ile !
 
WanaJF,

Hivi anapatikanaje au anachaguliwaje huyu mufiti??

Tafadhali nielewesheni.

Lakini ni aibu!!
 
Kuna machafu Mengi Sana Ndani ya Bakwata Hata Sheikh Yahya Alishawahi kufukuzwa ila hii ya Sasa ya Mufti ni Kali...

Zanzibar nako mmh! Walishawahi kupokea Tende za Msaada Wakauza... Nadhani Mahakama ya Kadhi Inahitajika Fasta Kufunika hizi aibu na Watu watakuwa Waoga ....
 
Inasemekana amekula hela ya kuendeleza ujenzi wa misikiti iliyotolewa na serikali ya JK
 
Hii imekaaje kulikoni Bakwata kumgeuka Mufti na kumuambia ameifilisi yaani siku zote kuanzia alipoanza hadi kamaliza ndio wanastuka !!!

Wamsamehe tu mambo ya wanadamu hata kuwa Mufti mkuu sio wamba hawezi kufanya makosa....

Au pengine hawajafanya utafiti kabla ya kutoa tamko la kumshutumu Mufti..

Itakuwaje kama Watamshitaki? au Mufti anakinga ya kutoshitakiwa?

Source Magazeti ya 25/12/2012

Nani aliyekuambia kuwa Bakwata imefilisika? Bakwata haifilisiki kama ilivyo Serikali ya Fisadi Kikwete. Na hata kama Bakwata haina pesa tutapata bailout kutoka Serikalini, kumbukeni kuwa Bakwata ni Kitengo kidogo cha Propaganda katika CCM, na CCM ndio inayoongoza Serikali legelege iliyokosa maadili na heshima katika Jamii. Kama kweli mufti wetu ni Fisadi basi atakuwa amerithi Ufisadi kutoka kwa Lowassa, Kikwete, Chenge na mafisadi wengine, maji hufuata mkondo. Iweje muwe mnapiga kelele kuhusu Mufti wetu? alichochukuwa ni vijisenti tu.

Waislamu tupo legelege kama ilivyo serikali ya CCM, hatujui kuhoji mambo ya Ufisadi ndani ya Bakwata kazi kutetea ujinga wa Serikali ya Kikwete iliyoshindwa kuongoza nchi na kulinda Rasilimali zetu, too sad to handle the truth kwa Waislamu wenzangu. Wengi wetu ni wanafiki kutetea upumbavu wa hawa Bakwata na kusifia ujinga wa Kikwete.
 
Kuna machafu Mengi Sana Ndani ya Bakwata Hata Sheikh Yahya Alishawahi kufukuzwa ila hii ya Sasa ya Mufti ni Kali...

Zanzibar nako mmh! Walishawahi kupokea Tende za Msaada Wakauza... Nadhani Mahakama ya Kadhi Inahitajika Fasta Kufunika hizi aibu na Watu watakuwa Waoga ....

Mahakama ya Kadhi itakuwa na Ufisadi kama Mahakama za tanganyika zilivyo, nyie subirini tu zikianza kazi mtasikia, tutachekwa sana. Wee angalia kwenye Tende mashekhe wa misikitini wengi wanatiana makonde kwa ajili ya Tende. Hata kusalisha misikiti pia tunapigana, sijui njaa ndio zinazotusumbua, aibu kwa kweli nikielezea tabia ya hawa mashekhe wetu.
 
mimi kama muhumini wa wa dini ya kiislam ntasikitika sana kama hizi kashfa zitaishia magazetini tu, kweli dunia imekwisha na itabidi niyaamini haya na lapa lazima hatakuwa peke yake aende keko au ukonga iwe fundisho kwa wengine.huu ushabiki wa bakwata kwa chama tawala wakijua madudu yalojaa umo ccm hasa kugubikwa na ufisadi wa kutisha ni dhahiri hawa bakwata yote imejaa watu wasokuwa wema, hii bakwata imekuwa wakala wa ccm, kumbuka madudu iloyafanya uko igunga kutupotosha waislam wote wakati imedhihirika yule mama hakuwa mwislam.na walivyofasta katika vyombo vya habari nawataraji leo watujulishe kulikoni ata sadaka na kadhalika zinafisadiwa tena na mkuu mufti simba, ndo ata tunaendelea kuwa duni kumbe hiki chaweza kuwa moja ya chanzo. nasisitiza hatua zichukuliwe mapema vinginevyo bakwata watakuwa wanalinda na kufumbia macho maovu.

Mimi wala sitetei ujinga wao hawa watu wa Bakwata na CCM, lakini watakuja wakina faiza foxy na malaria sugu watatetea huu ujinga na upumbavu wa Bakwata.
 
Unafiki hauwezi kumsitiri mtu mbele ya aibu anayoitengeneza. Tatizo sioi Bakwata kama chombo. Tatizo ni watu wanaoziongoza taasisi hizi. Njaa kali halafu wanatetea hata makosa ambayo dini zetu zinasema bayana kuwa ni dhambi mbele ya mungu. Ndo hapo sasa unafiki unaposhindwa kutusitiri!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom