kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Issa bin Shaaban Simba amewataka Waislamu kuwaombea dua wenzao waliouawa katika vita inayoendelea Libya na wengine wanaodhulumiwa haki zao duniani.
Alitoa mwito huo kwenye hotuba yake katika Msikiti wa Gaddafi mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Alisisitiza waumini wamwombee Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Waislamu duniani na wanyonge katika nchi zote bila kujali kama ni za Kiislamu.
Mufti Simba alisema maadui wa Waislamu wanachochea watu wakorofi kuanzisha fujo na vurugu kwa kuwaunga mkono ili misaada inayotolewa na kiongozi wa Libya duniani kote ifikie mwisho.
Sisi hapa Dodoma tumepata msaada mkubwa kutoka Libya ni huu msikiti tuliuomba na tukaupata bila matatizo, alisema Mufti Simba.
Hata hivyo, alisema maombi yamewezesha maadui wa Gaddafi waliolenga kupiga nyumba yake kumkosa kwa kuwa ana hifadhi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa ibada anazofanya ni kubwa na ni mtu aliyehifadhi Kurani katika mwili wake.
Aliyashutumu mataifa makubwa ya Magharibi kwa kuelekeza vita nguvu zao kuipiga Libya kwa kutoa mali kuwasaidia waasi.
Wakati huo huo, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaaban aliwahimiza waumini kulinda utamaduni na kuenzi ustaarabu wa Kiislamu kwa kuepuka sera na utamaduni wa nchi za Magharibi unaolenga kutumia nguvu kuathiri mila na desturi za Kiafrika.
Alisema utamaduni wa Magharibi unalenga kuvuruga tabia za vijana kwa kuwafanya waige mambo yanayokiuka maadili.
Alitoa mwito wa kuiga mfano wa China na Japan zilizokataa kufuata sera na utamaduni wa nje na hivyo kuweza kupiga hatua ya maendeleo.